Sunday, 27 April 2014

Uzinduzi wa Wiki ya Sikukuu ya Ushirika wa Wanaume (CMF) ICC

SALAMU NA KAULI MBIU YA USHIRIKA WA WANAUME (CMF):
WANAUME!!! Taifa Kubwa;
CMF!! Eee Bwana fufua kazi Yako.
Habakuki 3:2

Hakika leo Bwana kaifufua kazi yake katika Kanisa letu la ICC hususani Idara ya Ushirika wa Wanaume wa Kikristo (Christian Men's Fellowship). Leo umefanyika uzinduzi rasmi wa Wiki ya CMF ambayo kilele chake ni Jumapili Ijayo 04/05/2014.

Zifuatazo ni baadhi ya picha chache za uzinduzi siku ya Leo.
Zoezi kamili liliongozwa na Mchungaji Kiongozi wa ICC ambaye ndiye Mlezi wa Idara hii ya CMF Mch.Raphael Kitine.

Mwenyekiti wa CMF ICC Mr. Emmanuel Damalo akizungumza jambo katika Ibada ya leo, kwambaali mlezi wa Idara Mchungaji Raphael Kitine akimsikiliza Kijana wake kwa umakini.

Uzinduzi rasmi ulifanyika kwa maandamano yaliyosindikizwa na sebene kali la Pastor Wambura linaloitwa Yakobo. Palikuwa hapatoshi leo ndani ya ICC, Wanaume walisebeneka kiukweliii..

Baada ya Wanaume kusebeneka, Kanisa lote likashiriki katika Ibada ya Kusifu na Kuabudu, Leo Wanaume wa ICC tumeandika historia mpya.

Baada ya kusifu na kuabudu, Mtumishi wa Bwana Joseph Fungo akifurahia jambo

Baada ya kipindi cha Kusifu na Kuabudi, kilifuatia kipindi cha Mahubiri kilichoongozwa na Mmoja wa Wanaushirika wa Idara ya CMF hapa Kanisani ambaye ni Mchungaji Mwanafunzi Mpakwa Mafuta wa Bwana Omega Kipemba. Alifundisha Ujumbe unaosema "WANAUME NA UAMSHO". Lilikuwa somo zuri sana, Mtumishi wa Bwana alikata shule ya Ukwelii.

Katika Ujumbe wa Leo alianza kwa kueleza maana ya Neno Uamsho:
Uamsho ni hali ya kuamka kiroho kutoka katika hali ya kudumaa au kutokukua katika maisha ya Muamini. Isaya 57:15

Baada ya hapo akaeleza Matokeo ya Uamsho:
1. Uamsho unampa Nguvu Mwanaume/Mwanamke;
2. Uamsho huongeza kina cha Imani ya Mwanaume/Mwanamke;
3. Uamsho unafungua macho katika Ukweli;
4. Uamsho huzalisha Nguvu na Uwezo wa kuishi katika Dunia, wala si kuifuatisha Dunia inavyokwenda;
5. Uamsho huvunja hirizi na nguvu za Ulimwengu ambazo humpofusha Mwanaume.

Akamalizia kwa kufundisha Sifa za Mwanaume/Mwanamke aliyepokea Uamsho:
1. Ana maono. Nehemia 1:1-2, 2:17-18;
2. Ni Jasiri kama Simba;
3. Ana bidii ya kufanya kazi. Nehemia 4:21 -22;
4. Hutamani mafanikio. Nehemia 2:19-20.
Akahitimisha kwa kipindi cha Maombi na Maombezi.

Katika kuhakikisha mambo yanakwenda sawa, Wadau wa miundo mbinu nao hawakucheza mbali;

Saturday, 26 April 2014

Mazoezi ya CMF Sehemu ya Iringa

Mazoezi ya mpira wa miguu yamefanyika leo katika viwanja vya Kleruu, ikiwa ni maandalizi ya Maadhimisho ya Sikukuu ya Ushirika wa Wanaume wa Kikristo CMF katika sehemu ya Iringa. Mungu awabariki wote mliofika siku ya leo.