Monday, 29 September 2014

IJUE CA's - IDARA YA VIJANA

Muh: Mwl. Ezekiel Fungo
Mkurugenzi wa Idara Ya Vijana (CA’s) - Iringa Central Church (ICC):

UTANGULIZI: 2 Kor 5:20
CA’s ni ufupisho wa maneno ya Kiingereza CHRIST AMBASSADORS, maana yake kwa Kiswahili ni MABALOZI WA KRISTO au WAJUMBE WA KRISTO.
Mkurugenzi wa Idara ya Vijana (CA's) ICC, Mwl. Ezekiel Fungo akiwa Madhabahuni ICC

MAKUSUDI YA IDARA YA VIJANA (CA’s):
1. KUSHUHUDIA;
2. KUABUDU;
3. KUJIFUNZA NENO;
4. KUTUMIKA;
5. USHIRIKA;
6. KUJIFUNZA UONGOZI;
7. KUTEKELEZA DIRA YA MAENDELEO YA KANISA LA TAG.

1. KUSHUHUDIA.  MATH 28:19-20
> Idara ya Wajumbe wa Kristo itawaandaa Wajumbe wa Kristo kwa mafunzo mbalimbali na kuwahamasisha ili kwa kutumia mbinu na njia mbalimbali waweze kufanya Uinjilisti wenye nguvu utakaowawezesha kuwaleta watu wenye dhambi kwa Yesu, ambao nao wataandaliwa ili wawe wavuna roho za watu na kulitimiza Agizo Kuu. Math 28:19-20.

A. KUSUDI HILI LITATEKELEZWA KWA NJIA ZIFUATAZO:
i). Ushuhudiaji wa mtu kwa mtu;
ii). Ushuhudiaji wa nyumba kwa nyumba;
iii). Ushuhudiaji katika maeneo mbalimbali; kama vile Masokoni, Mashuleni, Vyuoni, Hospitalini, Magerezani na maeneo yote ya mikusanyiko inayoweza kufikiwa.
iv). Kushuhudia kwa kugawa tracts, machapisho mbalimbali ya Neno la Mungu na njia nyinginezo kama Roho Mtakatifu anavyowaongoza kufanya.

> Ili Kijana aweze kuishi maisha yanayo mlingana Yesu Kristo na kuwa shahidi wa Yesu lazima awe ameandaliwa.       Luka 2:41-52; Luka 3:23.

B. SIFA ZA KIJANA/MTU ANAYESHUHUDIA:
i). Awe amezaliwa mara ya pili na amejazwa na Roho Mtakatifu. Mdo 1:8; Mdo 2:37 – 41; Mdo 4:13.
ii). Awe anaishi maisha matakatifu (Nuru ya Ulimwengu).        Math 5:14 - 16.
iii). Awe mwombaji mwenye mzigo kwa watu ambao hawajaokolewa.  Mdo 17:16 – 23.
 iv). Awe amejaa Neno la Mungu. 1Tim 2:1 – 4.
 v). Awe na mwenendo mzuri katika maisha yake.
 vi). Awe ameandaliwa. Mdo 8:14 – 17.
vii). Awe na ujasiri wa kumuhubiri/kumtangaza Yesu Kristo.     Mdo 4:8 – 13.

C. SABABU ZA KUSHUHUDIA WENYE DHAMBI:
1) Wenye dhambi wamekufa wametenganishwa na Mungu.
 > Wanahitaji ufufuo au kuzaliwa mara ya pili. Ef 2:1-2
2) Wenye dhambi wamepotea wanahitaji Wokovu (Ukombozi). Luka 15:11-24.
 > Hawako mikononi mwa Mungu;
> Hawajui jinsi ya kumrudia Mungu.
3) Wenye dhambi wanahitaji kurudi mikononi mwa Mungu, wanahitaji Wokovu. Luka 19:10.
4) Wenye dhambi ni watumwa wanahitaji kununuliwa na damu ya Yesu. Yn 8:34.
5) Wenye dhambi wanamilikiwa na kuongozwa na shetani.        Rm 6:16, 20.

6) Yesu Kristo alitoa fidia maisha yake kwa wote wenye dhambi. 1 Kor 6:20; Gal 3:13; 1 Pet 1:18.
7) Yesu yuko tayari kuwa weka huru wenye dhambi wanaomwendea. Gal 5:1.
8) Wenye dhambi ni vipofu wanahitaji mwangaza.    2 Kor 4:4; Mdo 26:18; Kol 1:13.
9) Wenye dhambi ni waasi wanahitaji kupatanishwa.
> Wenye dhambi ni maadui wa Mungu. Rm 5:10; Tito 3:3; Yak 4:4.
10) Mungu hafurahishwi na kifo cha mtu mwenye dhambi. Ez 33:11.
11) Wenye dhambi wanahitaji kutubu kwa Bwana Yesu. 2 Kor 5:19 – 21; Kol 1:20; Mdo 17:30 – 32.

Waamnini wa ICC wakifuatilia somo kwa umakini mkubwa.
NB: Somo hili litaendelea Jumapili ya kilele cha Wiki ya Sikukuu ya Idara 05/10/2014. Ibada itakuwa moja kuanzia saa mbili kamili hadi saa tano na nusu Kanisani ICC (Sabasaba), watu wote mnakaribishwa.

2 comments: