Mch. Ruth Kyando akihudumu katika madhabahu ya ICC wakati wa Ibada ya Pili (Ibada ya Kiswahili).
Kabla ya Mahubiri, kwa kawaida ICC hutangulia Ibada ya Nguvu ya Kusifu na Kuabudu ambayo huongozwa na Timu ya Kusifu na Kuabudu ya ICC. Ibada ya Kusifu na kuabudu ilikuwa njema sana iliyojaa uwepo wa Nguvu za Mungu. Zifuatazo ni baadhi ya picha wakati wa Ibada hii.
Timu ya Ufundi na mbiundo mbinu wakihakikisha mambo yanakwenda sawa.
Baada ya Kusifu na kuabudu, ukafuatia wasaa wa kusikiliza Neno la Mungu.
Mch. Ruth Kyando akihudumu Ibada ya Pili ICC
SOMO: KUWA WAKILI MWAMINIFU WA MALI ZA MUNGU:
YALIYOMO:
I. MAANA NA AINA ZA MATOLEO.
II. MATOLEO KATIKA KUMCHA MUNGU.
III. MATOLEO YANAGUSAJE MAISHA YA MWAMINI?
UTANGULIZI:
- Kiini cha somo ni jinsi gani matoleo yanavyoleta mahusiano kati ya Mwamini na Mungu.
- Jambo hili la uhusiano na Mungu kupitia matoleo ni la muhimu sana kulijua.
- Mara zote Mungu akitaka kuupima upendo na kujitoa kwa mtu anampima katika suala la matoleo. Kwa mfano: Abrahamu alipimwa katika kumtoa mwanae wa pekee Isaka, kipenzi cha moyo wake na tegemeo lake lote. Mwz 22:1 - 2. Kwa utii wa Abrahamu katika utoaji Bwana alimpa Baraka ya Kristo kuzaliwa katika ukoo wake. Math 1:1 - 17.
- Utoaji unafungua milango ya baraka za Mungu. Mwz 22:15 - 16.
- Jinsi matoleo yanavyohusiana na maisha ya rohoni. Mdo 10:1 - 4. Tunamuona Kornelio na familia yake.
- Wakili ni mtu aliyepewa dhamana ya usimamizi wa jambo fulani na mtu mwingine, kwa lengo la kusimamia kwa weledi kwa kadri ya thamani ya kile kitu alichopewa.
- Matoleo ni kitu kinachotolewa kwa hiari, lakini pia ni sehemu ya ibada.
> Kutoa kitu cha thamani.
> Hizi zilikuwa sadaka za wanyama ambao waliuwawa na kutoa maisha yao (damu zao - uhai wao).
> Dhabihu iliteketezwa kwa moto (Lawi 6:8 - 13) na damu ya mnyama iliifunika dhambi ya mtoa dhabihu ili awe na uhusiano na Mungu na kuruhusiwa amwabudu.
> Kuteketezwa kwa moto mwili wote wa mnyama ilikuwa ni ishara ya mtoa sadaka kutoa maisha yake yote kikamilifu kwa Mungu katika utakatifu na kutengwa na dhambi.
ii) Dhabihu ya dhambi.
> Dhambi zilizotendwa sio kwa kusudi ila katika ujinga zilihitaji matoleo ya dhabihu ya dhambi. Lawi 4:1 - 35; 6:24 - 30.
iii) Dhabihu ya hatia.
> Lawi 5:14 - 19; 6:7. Dhambi za kushindwa kumuheshimu Mungu katika matoleo au mambo matakatifu aliyo agiza Bwana.
> Dhabihu hizi zilikoma baada ya Yesu kuja (Ebr 9:1 - 12); njia ya kuingia patakatifu ilikuwa bado haijadhihirishwa kama ilivyo sasa.
> Yeye alifanywa upatanisho badala ya wanyama. Rum 3:23 - 25.
> Sadaka nyingine ilikoma ni ya mzaliwa wa kwanza. Kut 13:2.
> Baadae aliwatoa Walawi wafanye ukuhani badala ya wazaliwa wa kwanza. Hes 3:11 - 13, 44 - 51.
> Yesu alipelekwa hekaluni kuwekwa wakfu mbele za Mungu. Lk 2:22 - 24; lakini Wazazi wake hawakutoa sadaka kumkomboa mzaliwa wa kwanza.
> Luka alitaja sadaka ya kutakasikakutoka unajisi wa uzazi kwa sheria ya agano la kale sheria ya Musa. Lawi 12:1 - 8.
> Yesu ni mzaliwa wa kwanza na wote aliowanunua. Uf 5:9 - 10.
> Ebr 12:23, Mkutano mkuu na Kanisa la wazaliwa wa kwanza walioandikwa mbinguni.
II. MATOLEO KATIKA KUMCHA MUNGU
a) Kutoa ni ibada. Zab 50:23.
b) Kutoa ni kumcha Mungu. Ay 1:5.
c) Kutoa ni kutambua kuwa vitu vyote ni mali ya Mungu. Zab 24:1.
iv) Dhabihu ya amani na ushirika.
> Hii ilikuwa sadaka ya hiari, na zinandelea hata sasa. 1 Kor 9:13 - 14.
> Lengo kuu ilikuwa ni dhabihu ya chakula. Lawi 3:1 - 17; 22:21 - 25.
> Kulikuwa na aina tatu za dhabihu ya amani.
- Dhabihu ya shukrani au ya sifa na kuabudu: Hii ilitolewa ili kumshukuru Mungu kwa Baraka mtu alizobarikiwa na Mungu au Neema mtu aliyoipata kwa Mungu.
- Dhabihu ya upendo kwa Mungu (Lawi 22:23): Iliruhusiwa kutoa kitu chochote kulingana na uwezo wa mtu na Mungu alivyomjalia.
- Dhabihu ya malipo ya nadhiri (Lawi 22:21): Hii ilitegemea mtu alikuwa ameweka nadhiri kitu cha namna gani kwa Bwana.
* Kutoa fungu la kumi sio tendo la hiari bali ni sheria na agizo la Mungu kibiblia. Kumb 14:22; Lawi 27:30.
* Yesu anasema, zaka na matoleo mengine yasiachwe. Math 23:23.
* Mungu haangalii wingi wa sadaka bali anaangalia moyo ulioridhia na kukubali. Mwz 4:3 - 7.
* Tunatofautiana vipato, kila mtu anainuliwa hatua kwa hatua kulingana na viwango vya mapato yake. Na kila mtu anamtukuza Mungu.
* Mali ulizonazo ni za Mungu, sisi ni mawakili tu tunasimamia badala yake. Zab 24:1.
* Hatuna kitu tulichokuja nacho duniani wala hatutaondoka na kitu. Ay 1:21.
No comments:
Post a Comment