Friday, 8 August 2014

KANUNI ZA UINJILISTI

Na Mch. Omega Kipemba (ICC)
Maandiko: Marko 6:7-13
 Mch. Omega Kipemba akihudumu ICC


UTANGULIZI:
1. Katika maandiko hayo (Marko 6:7-13) ni “Agizo lenye mipaka
a) Waliagizwa wakati wa huduma yao duniani. Math 10:1-6.
b) Ni agizo lenye mipaka kwa kuwa aliwaagiza kwa Waisrael tu. Math 10;5-6.

2. Kanuni za uinjilisti; Kwa maandiko hayo tunapata kanuni nne.
I. Kanuni ya Wawili-Wawili (Synergy)
II. Kanuni ya Uchaguzi (Selection)
III. Kanuni ya Somo (Subject)
IV. Kanuni ya Kutegemeza (Support)

I.KANUNI YA WAWILI-WAWILI (SYNERGY)
1. Hii imetajwa kwenye Mk 6:7.

2. Jambo lililoendelea nyakati zingine kama vile;
a) Bwana Yesu alipotuma wale sabini Luka10:1
b) Roho mtakatifu alipowatuma Paulo na Barbaba. Matendo13:2.

Umuhimu
1. Wawili hutiana moyo na kusaidiana. Mhubiri 4:9-10.
2. Ushuhuda wa wengi unaleta maana. Yon 8:17
  “...Ushuhuda wa watu wawili ni kweli”
Inapobidi fanya jitihada upate Mhudumu mwenza.

II. KANUNI YA UCHAGUZI (SELECTIVE)
1. Kuhubiri kwa wanaotamani kusikia. Marko 6:10.

2. Kukung'uta mavumbi kwa waliowakataa. Marko 6:11.

3. Hii ni kanuni ya uchaguzi
    a) Paulo alitamani kuhubiri tena kwa watu waliotamani. Mdo13:42-44
    b) Walipokataa Injili aligeukia kwingine. Mdo13:45-46.

III. KANUNI YA SOMO
> Mitume walipewa somo.
1.Katika agizo hilo lenye mipaka”somo lilikuwa tubuni” Mark 6:12

2. Pia ujumbe ulihusisha ufalme wa mbinguni.

3. Katika agizo kuu ikajumuisha injili ya Yesu.
a) Mwinjilisti filipo alihubiri Samaria. Mdo 8:12
b) Paulo alihubiri kwenye masinagogi na nyumba kwa nyumba.
Mdo19:8, 20:18-21, 25; 28:23, 30-31

IV. KANUNI YA KUTEGEMEZA
1. Waliwategemea wengine wawategemeze. Marko 6:8-10

2. Walitegemezwa na wale waliopenda huduma.

3.Hii inaonyesha kanuni ya kuwategemeza watenda kazi.
  a) Ilitetewa na Paulo. 1kor 9:4-14    
  b) Ilitumika kwa wazee walioongoza vizuri. 1Tim5:17-18
  c) Iliungwa mkono na Yohana miaka mingi baadaye 3Yoh 5-8.

Hivi ndivyo injili ilivyoenea kote ile karne ya kwanza.


No comments:

Post a Comment