Mhubiri: Mh. Mwl. Given Lemway
Maandiko: Muhubiri 3:1 - 22; Matendo 1:8
Kweli Kuu: "Kwa kila Jambo na majira, nyakati na wakati wake chini ya mbingu ambalo Mungu amemwekea mwanadamu, kuzaliwa, kuishi na kufa kimwili na kiroho pia"
I. UTANGULIZI: Maana ya Maneno Muhimu
1. Kizazi:
> Ni kundi la watu waliozaliwa katika wakati unaofanana. Mfano 1940 - 1950; 1950 - 1960; 1970 - 1980 n.k
> Tangu Kanisa la T.A.G lianze miaka 75 iliyopita kuna kama vizazi vitatu vimepita hadi sasa. Kizazi cha kwanza ni cha miaka ya 1940 - 1950 miongoni mwao ni akina Askofu Lazaro ambao kimsingi walikabidhi kijiti kwa kizazi kilichofuata chja miaka ya 1950 - 1960 ambao ndio wanaomalizia kazi kwa sasa. Kizazi hicho cha pili kinatakiwa kukabidhi kwa kizazi cha miaka ya 1970 - 1980 ambacho ni Vijana wengi wenye nguvu kwa sasa. Swali, Je, kizazi hiki cha tatu kinatimiza wajibu wake ipasavyo katika kuhubiri Injili!!??
2. Wakati:
> Ni kiwango cha muda, nukta, saa hadi miaka. Daniel 7: 12 - 25.
> Kila mtu anapaswa kuutambua wakati wake.
3. Nyakati:
> Ni vipindi vya hesabu za kibiblia vinavyo onesha miaka na vizazi na utendaji wake.
> Mfano: katika kukua mwanadamu hupitia nyakati mbalimbali. Mfano Utoto, Ujana, Uzee.
4. Majira:
> Ni vipindi vya misimu vinavyo onesha matukio mbalimbali yaliyopita au yaliyotokea katika vizazi vilivyo pita.
> Mfano: Majira ya Sikukuu za idara kanisani kama CA's, WWK, CMF n.k kilka Idara inakuwa na majira yake kila mwaka.
> Kila kizazi kinapaswa kujitambua katika wakati, nyakati na majira mbalimbali.
> Kizazi hiki cha sasa (kizazi cha tatu) kinapaswa kujitambua kinafanya nini katika kumtumikia Mungu. Kizazi cha sasa kimekuwa bize sana katika facebook na blogs kuliko kumtumikia Mungu, Je ndilo agizo tulilopewa. Hivyo basi kizazi hiki kinapaswa kutumia teknolojia ya kisasa katika kuhubiri injili. Pia kutumia uwezo wa akili ambao Mungu kajaalia katika kuwaleta mataifa kwa Yesu.
> Imefika hatua sasa, Kanisa linaongezeka kibailojia na si kuhubiri watu injili na kuokoka. Kukua kibailojia maana yake kama Baba kaokoka, basi watoto wake nao wamezaliwa katika dini hiyo na kuendelea kuwa wafuasi wa dini kwa kuwa wamezaliwa humo. Hivyo kazi ya ziada inabidi ifanyike ili Kanisa lisiongezeke kibailojia tu bali kwa kuhubiri injili na kuwageuza mataifa waikubali kweli kuu.
> Kizazi cha sasa kimekuwa ni cha kutumwa zaidi kuliko kutumika. Lengo sio kutumwa bali kutumika nyumbani mwa Bwana. Hivyo basi kila Kijana anapaswa kuwa na ndoto ili amtumikie Mungu kutokana na ndoto yako, badala ya kuwa mtumwa. Leo utatumwa kafunge projector screen, kesho kafagie kanisa n.k badala ya kumtumikia Mungu.
II. MAKUNDI YA WATU WALIOTUMIA WAKATI WAO VIBAYA KATIKA BIBLIA:
i. Mfalme Sauli: 1 Samweli 15: 1 - 35
> Katika kipindi hiki Taifa la Israel liliongozwa na Mungu kupitia kwa Nabii wake Samweli. Samweli ndio alikuwa Kuhani Mkuu , hivyo Taifa lilipokea maagizo yote kutoka kwa Mungu kupitia kwake.
> Baada ya Samweli kuzeeka, watoto wake walianza kuhudumu katika madhabahu ya Bwana, lakini watoto hao walijawa na rushwa na kufanya mambo kinyume na Mungu.
> Taifa la Israel likadai kupatiwa Mfalme, ndio wakapewa Sauli awaongoze.
> Sauli hakuwa na roho ya utii, hakuonekana kukubaliana na maelekezo aliyokuwa akipewa na Samweli.
> Sauli aliutumia wakati wake mwingi kulipiza kisasi dhidi ya Daudi. Kwa kutoutambua wakati wake vyema Mungu alimkataa asiwe Mfalme.
> Sauli alipoteza uhusiano wake na Mungu kwa kuwa hakufuata maelekezo ya Mungu, Mungu akamkataa. Ikafika hatua Sauli alienda kwa waganga wa kienyeji (wapunga pepo) kuulizia mustakabali wake.
> Mwishowe Sauli alijiua mwenyewe kwa kuangukia upanga wake.
Mh. Mwl. Given Lemway akiendelea kushusha dozi ya ukweli kwa Vijana, yaani leo yalikuwa ni makavu live.
> Kutoka kwa Mfalme Sauli kuna mambo mengi ya kujifunza;
* Kizazi cha sasa tunapaswa kuutumia muda (Nyakati, wakati na majira) vizuri ili kutimiza agizo kuu la Bwana Yesu.
* Kizazi cha sasa tunapaswa kuwa watii wa maneno/maagizo ya Mungu.
* Tusipofuata maelekezo ya Mungu, Mungu atatukataa.
* Kizazi cha sasa tusipotambua nafasi zetu katika kumtumikia Mungu tutapoteza uhusiano wetu na Mungu.
* Endapo tutapoteza uhusiano na Mungu, tutakufa kiroho.
TAFAKARI, CHUKUA HATUA.
* Semina hii itaendelea tena Jumatatu wiki Ijayo Tarehe 14/07/2014. Karibuni wote.
Vijana wakisikiliza kwa umakini mkubwa, Ya leo ngumu kumeza haina kuremba mwandiko, yaani ni chungu lakini dawa.
Mkurugezi wa Idara ya Vijana (CA's) ICC Mr. Ezekiel Fungo akisisitiza jambo baada ya mafundisho ya leo.
Mh. Mwl. Given Lemway akiwa amepoz na Vijana baada ya somo.
No comments:
Post a Comment