Na: Mch. Raphael Kitine
MAANDIKO YA SOMO:
Mt 7:15-18; 1Fal 18:21-40
I. UTANGULIZI
i. Maelezo kuhusu Imani potofu
Ø Imani potofu, kwa ufupi, ni Imani ambayo wanaoifuata hawawezi kumuona Mungu wakiwa hai na hata watakapokufa.
Ø Ziko Imani potofu ambazo ni rahisi kuzitambuwa kwa kuwa hupingana wazi wazi na mpango wa Mungu wa kumkomboa mwanadamu kupitia Yesu Kristo. Lakini zipo Imani zingine ambazo kwa haraka haraka unaweza kudhani ni kwa ajili ya kumsaidia binaadamu aweze kumuona Mungu. Hizi hutaja jina la Yesu na hufundisha baadhi ya mambo ambayo hata Bwana Yesu mwenyewe alifundisha. Lakini kwa undani wake kuna mengi ya kupotosha!
ii. Maana ya imani potofu
Ø Ni kikundi cha watu wanaoabudu kinyume cha kweli za Kibiblia Rm 1:18;24-25
Ø Ni watu wanaovaa nje ngozi ya kondoo lakini ndani ni mbwa mwitu wakali Mt 7:15
iii. Asili ya Imani potofu 2Kor 11:13-15
Ø Kutoka kwa shetani na majeshi yake Efeso 6:12
Ø Baada ya kuasi anafanya kila awezavyo kuipinga kazi halali ya Mungu Dan 10:12-13
II. MALENGO YA IMANI POTOFU
i. Kuidhohofisha imani sahihi Mt 13:24-30;36-39
Ø Kazi ya magugu ni kudhohofisha mmea halisi na kuufanya ushindwe kukua vizuri
Ø Imani potofu husababisha kanisa sahihi la Mungu lishindwe kukua vizuri
ii. Kupotosha ukweli wa maandiko 2Pet 3:16
Ø Mungu husema na watu wake kwa kutumia maandiko
Ø Kazi ya imani potofu ni kuvuruga mawasiliano kati ya Mungu na watu wake kupotosha maana ya halisi ya maneno ya Mungu
iii. Kuwafanya watu washindwe kumwona Mungu Mdo 12:20-23
Ø Kwa kuwapofusha macho ya Rohoni
Ø Kwa viongozi wa dini husika kujitukuza na kuchukua nafasi ya Mungu
III. JINSI YA KUZITAMBUA IMANI POTOFU
i. Kuujenga mwili kuliko roho Mt 6:31-33; Flp 3:17-20
Ø Maombezi ya kimwili huchukua sehemu kubwa kuliko ya Kiroho
Ø Mafundisho ya uponyaji wa kimwili huchukua nafasi kubwa zaidi kuliko ya kiroho
Ø Mafundisho ya mafanikio ya kimwili huchukua nafasi zaidi kuliko utakatifu
ii. Nguvu inayotumiwa siyo ya Mungu Mt 7:22-23
Ø Nguvu inayotumiwa inafanana kama ya Mungu lakini si Mungu
Ø Nguvu ya kishirikina inatumiwa kufanya miujiza mbalimbali
Ø Dalili ni matumizi haba ya jina la Yesu katika huduma
iii. Kuona dhambi si kitu (Minimize Sin) 1Kor 5:1-2
Ø Dhambi haipewi nafasi ya kukemewa
Ø Watu wanaachwa kufanya wapendavyo
Ø Hakuna hatua zinazochukuliwa kwa watenda dhambi
iv. Hupiga vita imani sahihi 1Kor 14:32-33
Ø Huzidhohofisha imani sahihi kwakuzipiga vita
Ø Hutumia lugha za matusi na kejeli juu watumishi wa imani sahihi
v. Humfanya Mungu kama mwanadamu (Humanize God) Rm 1:21-25
Ø Kuishusha hadhi ya Mungu
Ø Huduma hazimpi Mungu utukufu
vi. Kuwa kinyume na maandiko (Ostracize The Scriptures) Gal 3:10; 2Tim 3:5-7
Ø Hufundisha mambo yanayopingana na maandiko
Ø Hupotosha tafsiri sahihi ya neno la Mungu
vii. Watumishi kuchukua nafasi ya Mungu (Deify Man ) 2Thes 2:3-4; 2Timotheo 3:1-4
Ø Badala ya huduma kumtukuza Mungu huwatukuza watumishi binafsi
Ø Majina ya watumishi kuchukua nafasi ya jina la Mungu
viii. Kutoamini wokovu/au kuamini kwa njia isiyo sahihi 2Kor 6:14; Gal 1:6-9
Ø Mafundisho na mahubiri yao hayatoi msisitizo wa wokovu kwa wanadamu
Ø Mafundisho na mahubiri yao hayatoi msisitizo wa mtu kuisha maisha matakatifu
Ø Msisitizo wa mafundisho ni utowaji sadaka kuliko utakatifu
No comments:
Post a Comment