Maandiko: Mdo 1:4-5.
I. UTANGULIZI -MAANA YA UBATIZO WA ROHO MTAKATIU
- Ni tendo la kuzamishwa na kujaa Roho Mtakatifu. Mdo 1:4, 2:4.
- Ni tofauti na kuzaliwa mara ya pili. Yn 20:22; Mdo 2:4, 8:12, 1:4.
- Ni kipawa cha Nguvu kutoka kwa Mungu. Lk 24:49; Mdo 1:8; Lk 1:35.
- Ni ahadi kwa wote waaminio. Mdo 2:4, 39.
- Imeagizwa katika maandiko. Ef 5:18, Mdo 1:4-5.
- Ni chanzo cha Nguvu za Kiroho:
- Katika Huduma ya Yesu Kristo. Mdo 10:38; Lk 4:1.
- Katika Huduma ya Kanisa la kwanza. Mdo 1:8, 2:4, 4:31, 33.
A. MASHARTI YA KUBATIZWA NA ROHO MTAKATIFU.
- Lazima uzaliwe mara ya pili. Yn 14:17; 3:5-7.
- Upende kujazwa na Roho Mtakatifu. Mt 5:6; Rm 15:16; 1Kor 6:11, 7:37.
- Mtii Mungu. Mdo 5:32.
- Karibia kwa ujasiri katika kiti cha neema. Ebr 4:16.
- Mwombe Mungu akujaze Roho Mtakatifu. Lk 11:10, 13.
- Msifu Mungu kwa Imani. Mk 11:24; Lk 24:53.
- Kunena kwa lugha. Mdo 2:3, 10:45-47, 19:1-6.
- Ishara hizi zitafuata ukitembea katika Roho:
- Kuwa na uwezo wa kutenda kazi za Yesu. Yn 14:16-18, 16:14.
- Kuhisi uwepo wa Mungu. Yn 14:16-18.
- Kusikia vibaya kuhusiana na dhambi. Yn 16:7-11.
- Kuwa na uwezo wa kushuhudia. Mdo 1:8.
- Kuwa na ujasiri. Mdo 2:14-41.
- Kujisikia kumpenda Mungu na watu. Rm 5:5.
- Kuwa na uwezo na hamu ya kuomba na kuwaombea wengine. Rm 8:26-27.
- Madhihirisho ya karama za Roho Mtakatifu. 1Kor 12:1-11.
- HAMU: Uwe na hamu ya kubatizwa na Roho Mtakatifu.
- IMANI: Amini kuwa unapokea Roho Mtakatifu sasa. Ebr 11:16; Mk 11:24.
- MSIFU BWANA: Bwana anaonesha uwepo wake wakati wa sifa. Mdo 4:31.
- JIWEKE CHINI YA MUNGU: Jitoe kwa Bwana kila kitu kiakili na kimwili. Rm 6:13, 12:1.
No comments:
Post a Comment