Tuesday, 23 December 2014

KAZI ZA ROHO MTAKATIFU KATIKA MAISHA YA MWAMINI

Na. Mch. Raphael Kitine (Mchungaji Kiongozi ICC)
Andiko Kuu: Yohana 16:5-15

I. UTANGULIZI:
  • Yohana 16:5-15 ni mistari ya msingi kuhusu Roho Mtakatifu.
  • Katika mistari hii, Yesu anawaambia Wanafunzi kwamba mambo yatakuwa magumu mara tu akitoweka na ya kwamba watu watawachukia.
  • Hivyo anawafariji kwa Ujumbe wa Roho Mtakatifu kwa kuwaambia kuwa "... ni faida kwao ikiwa ataondoka maana atatuma msaidizi..".
Waamini wa ICC wakifatilia Mahubiri Ibadani.
II. NAMNA 5 ROHO MTAKATIFU ANAFANYA KAZI KATIKA MAISHA YA MWAMINI:
1. Roho Mtakatifu Hujua udhaifu wetu.
  • Roho Mtakatifu haishii kutujua tu, hutusaidia pia katika udhaifu wetu. Rumi 8:26;
  • Hutuwezesha kufanya mambo tusingeweza kufanya kwa uwezo wetu wenyewe. Kama linampa Yesu Utukufu na linahusu watu wake na Kanisa lake, Roho Mtakatifu anatutaka tuangalie hilo na atafanya kazi nasi na kututia nguvu.
2. Roho Mtakatifu Hutufundisha.
  •  Roho Mtakatifu hufanya kazi kupitia Maandiko na watu kubadilisha mioyo yetu. Yohana 14:26; Rumi 8:14; 1 Kor 2:6-14;
  • Tunaposhindwa kuelewa fungu fulani katika Biblia, Roho Mtakatifu hutufundisha kulielewa na namna ya kulitumia katika maisha yetu. Rumi 10:14-16.
 3. Roho Mtakatifu Hufanya kazi kupitia maombi.
  •  Roho Mtakatifu hutuombea kupitia maombi. Rumi 8:26;
  • Hutuombea hasa tunapoweka mkazo katika kumpa Yesu Utukufu na kupenda watu wake;
  • Iwapo hujui nini cha kuomba, muombe Roho Mtakatifu maana Yeye ni "Msaidizi" atakayewasaidia wote wampendao.
  • Mara nyingi Mungu hutumia maombi kubadili mioyo yetu ili tuzidi kumuelekea Yeye.
 4. Roho Mtakatifu Hufunua kusudi la Yesu kwetu.
  •  Mungu hutoa vipawa. Alitupa Yesu, aliyefia dhambi zetu msalabani. Alitupa Roho Mtakatifu;
  • Alitupa mwongozo wa namna ya kuishi maisha yetu kupitia Biblia. 2 Tim 3:16-17;
  • Asilimia 95 ya kusudi la maisha yetu tunaipata kwenye Biblia;
  • Kusudi la maisha yetu ni kumpa Yesu Utukufu kwa Nguvu za Roho Mtakatifu na kuwapenda watu;
  • Roho Mtakatifu atatufunulia undani wa kusudi letu - mfano tufanye kazi gani na wapi, utaoa/kuolewa na nani, utaishi wapi n.k kadri tunavyosoma Biblia na kuishi kwa Imani.
 5. Roho Mtakatifu Hutushuhudia juu ya dhambi.
  • Yohana 15:8-11 inatufundisha kwamba Roho Mtakatifu hutushuhudia dhambi ilituvae taswira ya Yesu;
  • Tunavyokaa zaidi ndani ya Roho Mtakatifu, dhambi huwekwa wazi katika maisha yetu. Galatia 5:16, 18;
  • Hii hutuwezesha kutubu na kuhitaji kubadilishwa na Yesu ili tuvae ufanano wake.
III. HITIMISHO:
  • Kama wewe ni Mwamini Roho Mtakatifu Huishi ndani yako.
  • Jiachilie huru kwa Nguvu za Roho Mtakatifu.
  • Yesu anamwita Msaidizi kwasababu nzuri. Kwa hakika ni faida kuwa maishani mwetu; kumpa Yesu Utukufu ndio hasa sababu ya kutumwa kwetu. Yohana 15:26-27.

Mchungaji Raphael Kitine akihitimisha somo hili, huku Timu ya Kusifu na kuabudu ikiongoza katika kuabudu.

Zifuatazo ni Picha mbalimbali za Ibada ICC:
Mch. R. Kitine akiongoza maombezi ya Roho Mtakatifu, akiwa sambamba na Wachungji wasaidizi wa ICC; Kutoka kushoto ni Mch. R. Kyando akifuatiwa na Mch. O. Kipemba.


Waamini wa ICC wakati wa Ibada ya Kusifu na Kuabudu.


Kwaya ya PATMO ikihudumu katika madhabahu ya Bwana ICC

1 comment: