Na. Mch. Raphael Kitine
Andiko kuu: Mathayo 19:14-15.
Mch. Raphael Kitine akifundisha kuhusu kuwekwa wakfu watoto wadogo na kuwabariki kabla ya kuanza Ibada hiyo Maalumu.
Katika Siku ya Jumapili ya kwanza ya mwaka 2015 (04/01/2015), Mchungaji Kiongozi wa ICC, Mch. Raphael Kitine ameongoza zoezi la kuwaweka wakfu na kuwabariki watoto wadogo ili wakue chini ya uongozi wa Yesu Kristo. Ibada hii ni muhimu sana kwani watoto wadogo hawabatizwi bali wanawekewa mikono kufanyiwa maombi, kama ishara ya kubarikiwa na kuwekwa wakfu mbele za Bwana.
Zifuatazo ni picha mbalimbali za Ibada ya kuwekwa wakfu watoto wa waamini wa ICC.
No comments:
Post a Comment