Katika Nyumba ya Bwana ICC uwepo wa Nguvu za Mungu umeendelea kujidhihirisha kupitia Ibada mbalimbali; Ibada ya Kusifu na Kuabudu, Ibada ya Neno la Mungu pamoja na Ibada ya Maombi na Maombezi. Karibu sana katika Nyumba ya Bwana ICC uweze kupokea haja ya moyo wako.
Zifuatazo ni baadhi ya picha za Ibada ya Jumapili iliyopita.
Mchungaji Kiongozi wa ICC Mch. Raphael Kitine, akishusha uwepowa Mungu katika Ibada.
Kama kawaida ya ICC, Ibada ya Kusifu na Kuabudu huanza kwanza maana Mungu anapendezwa na Sifa, na tumeagizwa kila mwenye pumzi na Amsifu Bwana. Zaburi 150:1-6.
Mrs. Adder Mkea akiongoza Timu ya Kusifu na Kuabudu katika Ibada ICC
Mr. Petro Ng'ondya akiongoza Ibada ya Sifa katika uwepo wa Nguvu za Mungu ICC.
Kanisa zima pia lilishiriki kikamilifu katika Ibada hii ya Kusifu na Kuabudu.
Pongezi nyingi zimuendee Mchungaji Kiongozi wa ICC, Mch. R. Kitine kwa kulea vyema huduma za watoto hadi kufikia hatua ya kuanza kutumika Madhabahuni. Jionee picha zifuatazo ni watoto wadogo kabisa lakini wanamtumikia Mungu katika Madhabahu ya Bwana. Ni Wachungaji wachache sana wenye moyo huu wa kulea vipaji vya watoto na kuwapa nafasi ya kutumika katika Madhabahu.
Binti mdogo kabisa Rebecca akiongoza Timu ya Kusifu na Kuabudu katika Ibada ICC.
Vijana wadogo kabisa James (Keyboard) na Amani (Gitaa) wakihudumu katika Ibada ICC.
Mwl Alpha aliongoza vyema jahazi la wapiga vyombo vya muziki na dawati la IT alisimama vyema Mr. Yohana Lemway. Mungu awabariki kwa kukitikia wito wa kumtumikia Mungu.
Baada ya Ibada ya kusifu na kuabudu, ilifuatia Neno la Mungu ambapo Mch. Omega Kipemba alifundisha Neno la Mungu.