Monday, 2 March 2015

Sikukuu ya Wanawake Watumishi wa Kristo (WWK) ICC

Shalom!
Jumapili ya Tarehe 01/03/2014 ilikuwa ni Ibada Maalumu ya Kilele cha Wiki ya Sikukuu ya Wanawake (WWK) ICC. Ibada ilikuwa njema na ya kuyapendeza. Mungu awabariki Wanawake wote waliojitoa kwa hali na mali ili kufanikisha Sikukuu hii.

Zifuatazo ni baadhi ya picha za matukio ya siku hiyo.

Mwenyekiti wa WWK ICC, Mama Msola akizungumza jambo wakati wa Ibada

Mchungaji Kiongozi wa ICC, MCh. Raphael Kitine akizungumza na Wanawake na Kanisa kwa ujumla kuhusu WWK

 Aliyekuwa Mgeni Mualikwa na Muhubiri wa Siku hii, Mama Sanga akiwa madhabahuni.

Wanawake Watumishi wa Kristo (WWK)  ICC wakiimba shairi

Mrs. Gerald Malecela na Mrs. Foida Kimbavala wakisoma risala kwa niaba ya WWK ICC

WWK ICC wakiwa wamejipanga mbele ya Kanisa kwaajili ya Kumkabidhi zawadi Mchungaji Kiongozi wa ICC, Mch. Raphael Kitine.

Mgeni Mualikwa Mama Sanga, akinena jambo kisha kumkabidhi Mch. Raphael Kitine zawadi iliyoandaliwa na WWK ICC

Mch. Raphael Kitine akinena jambo baada ya kukabidhiwa zawadi, kisha akawafanyia maombi WWK ICC

Katika Ibada hii kulikuwa na Tukio Maalumu la Keki iliyoandaliwa na WWK kwaajili ya kutunisha mfuko. Zoezi hili liliendeshwa na Mrs. Msafiri kwa kushirikiana na Mrs. Kimbavala..