Tuesday, 22 March 2016

SIKU TATU ZA MATENDO MAKUU YA YESU T.A.G - ICC LUGALO



Shalom Wapendwa!

Mch. Raphael Kitine (Mchungaji Mwenyeji na Mchungaji Kiongozi T.A.G - ICC Lugalo)

Mch. Songwa Kazi (Mchungaji kutoka T.A.G Forest Kongowe Dar es Salaam)

HUDUMA YA LIFE CHANGING MINISTRY INTERNATIONAL (LCM) ILIYOPO CHINI YA MKURUGENZI NA MWASISI WA HUDUMA HII, MCHUNGAJI SONGWA KAZI  AMBAYE NI MCHUNGAJI WA KANISA LA TAG FOREST KONGOWE LILILOPO JIJINI DAR ES SALAAM AKIWA NA TIMU YAKE NZIMA YA LIFE CHANGING MINISTRY INTERNATIONAL (LCM).

WAKISHIRIKIANA NA KANISA LA TAG ICC LILILOPO LUGALO MANISPAA YA IRINGA WAMEANDAA SEMINA YA SIKU TATU  KWA WATU WOTE ITAKAYO  HUSU KUBOMOA MISINGI MIBAYA NA KUJENGA MISINGI MIPYA YA YESU KRISTO KATIKA ENEO LA MAHUSIANO(UCHUMBA), UTUMISHI NA  WITO WA MUNGU KWA MKRISTO.

SEMINA HIYO ITAANZA TAREHE 25/03/2016 SAA 9:OO ALASILI HADI 12:OO JIONI  NA ITAENDELEA  USIKU WA IJUMAA HIYO KATIKA MKESHA UTAKAOANZA SAA 3:00 USIKU, NA TAREHE 26/3/2016 SEMINA HIYO ITAANZA SAA  9:00 ALASILI HADI 12:00 JIONI   NA KUHITIMISHWA TAREHE 27/3/2016 KATIKA IBADA YA JUMAPILI YA  PASAKA KUANZIAA SAA 2:00 ASUBUHI HADI SAA 7:00 MCHANA.

SEMINA HIYO ITAFANYIKA KATIKA KANISA LA TAG-ICC LILILOPO LUGALO MANISPAA YA IRINGA KWA KATIBU WA TAG JIMBO LA IRINGA MCHUNGAJI RAPHAEL JARUFU KITINE AMBAYE NI MWENYEJI WA TIMU HIYO YA (LCM).

LENGO LA KONGAMANO NA SEMINA HIYO NI KUIJENGA MISINGI YA VIZAZI VINGI ISAYA 58:12-14 NA ZABURI 11:3.

KWAYA NA WAIMBAJI BINAFSI WATAHUDUMU KATIKA SEMINA HIYO,”NI SIKU TATU ZA MATENDO MAKUU YA MUNGU”.NJOO UPATE MAARIFA YA NENO LA MUNGU KWANI “UFAHAMU NI NGUVU”.

KWA MAWASILIANO ZAIDI PIGA SIMU NO 0757-567899/0767-354777 AU PIGA SIMU NO 0755-974279 KWA MKURUGEZI WA VIJANA CA’S SEHEMU YA MANISPAA YA IRINGA EZEKIELI FUNGO KWA MAELEKEZO ZAIDI JUU YA KONGAMANO NA SEMINA HIYO.