Saturday, 7 October 2017

MATESO YA MWENYE HAKI [SEHEMU YA I]

MUHUBIRI: 
Mch. Raphael Kitine
[Mchungaji Kiongozi, T.A.G ICC Lugalo]
[+255767354777; +255784354777; +255719354770]
E-mail: raphaelkitine@yahoo.co.uk
ANDIKO KUU: 
ZABURI 34:19
“Mateso ya mwenye haki ni mengi, Lakini Bwana humponya nayo yote.”

I. UTANGULIZI
(i) Maana ya Mwenye Haki
> Ni hali ya Mtu kuwa na Ukamilifu kimaadili na kiroho ili kukubalika na Mungu katika Ufalme wake.
(ii) Nani Mwenye Haki?
1. Ni Mtu anayeishi kwa Imani na kumtegemea Mung katika mambo yote. Ebr 10:38
2. Ni Mtu aliyekubali kuacha uovu na kuepukana na anasa za Dunia. Ayubu 1:8
3. Ni Mtu aliyepata kibali machoni kwa Bwana. Mwanzo 6:8
4. Ni Mtu anayeishi maisha Matakatifu. Ayubu 12:4
(iii) Maana ya Mateso
1. Maana ya Neno Mateso
>Ni hali ngumu anayopitia Mtu na kumsababishia mauimivu ya kimwili au kisaikolojia.
2. Mifano ya Mateso:Rum 8:35-36;Mdo 14:19;16:22-23
>Mateso ya mwili kama Magonjwa, njaa n.k
>Mateso ya Kisaikolojia kama msongo wa mawazo kutokana na kukosa pesa, migogoro katika familia, n.k
(iv) Biblia Inasemaje Kuhusu Mateso ya Mwenye Haki?
Tujapopita katika mateso ya Dunia hii tutambue kuwa:
1. Mungu ni mwema na Mwaminifu Yeye atatuponya na kutuvusha. Zab 34:19; 1Kor 10:13
2. Mateso hayapaswi kututenga sisi na Upendo wa Mungu Baba. Rum 8:35-36
3. Hatuko peke yetu bali Mungu yupo pamoja nasi. Mt 28:20
4. Mungu siye Mwenye makossa na hatupaswi kumkufuru Yeye. Ayubu 2:9-10
5. Inatupasa kuvumilia mpaka mwisho. Mt 10:16-22

II. KWANINI MUNGU AMERUHUSU MATESO?
i. Lipo swali la kale kama vile chozi la kwanza, na vilevile ni swali jipya kabisa kama vile habari za hivi punde:
Kwanini? Kwanini Mungu aruhusu mateso, huzuni, maumivu ya moyo, na mauti/kifo, hata miongoni mwa watoto wake?
ii. Swali hili liliulizwa na Ayubu, na limekuwa likiulizwa na kila Mtu aliyepita katika uso wa Dunia na aliyemwamini Mungu.
iii. Jibu nililolipokea kutoka katika Neno la Mungu lilikuwa lenye kutia moyo sana kwangu kiasi cha kujawa shauku ya kuwashirikisha..
1. MATESO HUUFANYA ULIMWENGU USIWE WENYE KUVUTIA 1Yoh 2:15
i. Biblia inatuambia kuwa “Tuwapitaji” na “Wasafiri”
>Ulimwengu huu sio makazi yetu ya kweli. 1Pet2:11
>Mungu Ametuandaa kitu chema kwa ajili yetu. 2Kor 5:1
ii. Kama kusingekuwepo Mateso
>Asingekuwepo hata mmoja anayetamani kuuacha Ulimwengu huu
>Kusingekuwa na mwenye shauku ya makazi ya milele (kudumu) na hivyo kujiandaa kwaajili yake.
2. MATESO YANATUFANYA KUTHAMINI YALE TULIYOTENDEWA NA MUNGU. Zab 95:2
i. Wote katika maaishaa yetu hupokea mengi mema kutoka kwa Mungu. Lk 17:14-17
>Ni rahisi kusahau kuwa tumepewa na Mungu
>Bila yaa kupokea kwa shukrani nyingi kwa Mungu
ii. Mateso hutufanya kushukuru na kuthamini Zaidi. Dan 4:33-34
>Kushukuru kwa ajili ya afyaa njema
>Na mafanikio yote katika maisha yetu
3. MATESO HUTOA NAFASI YA KUNYAMAZISHA MAADUI WA MUNGU. 1Pet 2:15
i. Unakumbuka kilichotokea kwa Ayubu. Ayubu 1:11
>Shetani alitaaka kumdhalilisha Mungu juu ya Ayubu, > kwamba anamtumikia Mungu kwa saabu tu Mungu Amembariki.
>Lakini uvumilivu wa Ayubu katika mateso ulimyamazisha shetani
ii. Kwa unyenyekevu kuvumilia, au kutenda mema wakati wa mateso..
>Thamani ya Ukristo hakika hung’aa katikati yake
4. MATESO YANATUFANYA TUMTEGEMEE MUNGU ZAIDI. Mith 3:5
5. MATESO YANATUWEZESHA KUOMBA KWA BIDII. Mdo 12:5
6. MATESO HUTUSAIDIA KUTUTAKASA. 1Pet 1:7
i. Zingatia umuhimu wa vifungu vya Maandiko haya:
> 1Pet 1:6-7 Mateso yaweza kuwa kama moto utakasao dhahabu
> Yak 1:2-5 Kukua na kuimarika kwa Mkristo kunaweza kutokea kutokana na majaribu anayopitia. Yak 1:3-4

SOMO HILI LITAENDELEA...
KARIBU SANA T.A.G ICC LUGALO KWANI SOMO HILI NDO LINAFUNDISHWA KWA SASA.
MUNGU AKUBARIKI.

Tuesday, 26 September 2017

"Mateso ya Mwenye Haki" By Mch. Raphael Kitine (T.A.G ICC Lugalo)

SEMINA SEMINA SEMINA T.A.G ICC LUGALO

KANISA LA TANZANIA ASSEMBLIES OF GOD - ICC LUGALO, LINAKULETEA SEMINA YA NENO LA MUNGU KATIKA WIKI YA SIKUKUU YA VIJANA. SEMINA ITAANZA JUMATANO TAREHE 27/09/2017 HADI JUMAPILI TAREHE 01/10/2017 MUDA WA KUANZA NI SAA 10:00 JIONI. 

YESU KRISTO HANA UPENDELEO, KARIBUNI WATU WOOOTE MNAKARIBISHWA, NI WIKI YA KUPOKEA MUUJIZA WAKO. MATHAYO 11:28

SEMINA ITAFANYIKA KATIKA KANISA LA T.A.G ICC LUGALO, LILILOPO JIRANI NA UKUMBI WA KOICA WA SEKONDARI YA LUGALO IRINGA.

2KOR 5:20
“BASI TU WAJUMBE KWA AJILI YA KRISTO, TUHUBIRI INJILI, TUTAVUNA MPAKA KIELEWEKE”.

KWA MAWASILIANO PIGA: 0767354777; 0755974279
KARIBU SANA, YESU KRISTO ANAKUPENDA.


Tuesday, 9 May 2017

TAFRIJA YA KUWAAGA WANAFUNZI WA KIDATO CHA SITA 2017 WA LUGALO SEKONDARI, IRINGA

Siku ya Jumapili Tarehe 30/04/2017 Kanisa la T.A.G ICC Lugalo; linaloongozwa na Mch. Raphael Kitine liliandaa Tafrija fupi ya Kuwaaga Wanafunzi wa Kidato cha Sita kutoka Shule ya Lugalo Sekondari ambao wamekuwa wakiabudu T.A.G ICC Lugalo wakati wa masomo yao hapa Iringa. Huu ni Utaratibu ambao Kanisa limekuwa nao kuwaaga Wanafunzi na Wanavyuo baada ya kuhitimu masomo yao au wanapoelekea kumaliza masomo yao. Hakika ilikuwa ni tukio zuri la kupendeza ambapo Wanafunzi na baadhi ya Viongozi wa Kanisa waliketi pamoja; kula, kunywa na Wanafunzi kupewa nasaha. Mungu Awabariki wote walioshiriki na kufanikisha Tafrija hii.

Wanafunzi/Wanavyuo wote mliopo Iringa mnakaribishwa sana kuabudu T.A.G ICC Lugalo. Tunakaribisha Wanafunzi wa Sekondari na Wanavyuo wote bila kujali Madhehebu yao huko wanakotoka. Tunashirikiana na fellowship zote za Wanafunzi; PSA, CASFETA, TAYOMI, TAFES, USCF, TMCS, TUCASA n.k

Karibu sana Iringa Central Church, the Right Place to Worship, at the Right Time, with Right People in the presence of the Almighty God and Saviour Jesus Christ. Stay blessed.

Mchungaji Kiongozi wa T.A.G ICC Lugalo; Mch. Raphael Kitine katika Picha ya Pamoja na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Lugalo; Viongozi wa Kanisa, na Wageni Waalikwa.

Mch. Raphael Kitine akiwa katikati ya Mch. Omega Kipemba na Mkewe Mrs. Sophia Kipemba

Wanafunzi wa Kidato cha Sita kutoka Shule ya Sekondari Lugalo katika picha ya Pamoja

Wadau walioshiriki kutoa Nasaha kwa Wanafunzi

Barikiwa kwa picha za matukio mbalimbali katika Tafrija hiyo

Tuesday, 11 April 2017

THE NIGHT OF IMPACT 2017; Praise & Worship Explosion

Hakika Historia imeandikwa katika Mji wa Iringa Ukumbi wa St. Dominic Usiku wa Ijumaa Tarehe 07/04/2017. Ni katika Mkesha Mkubwa wa Kusifu na Kuabudu ulionadaliwa na Kanisa la T.A.G ICC Lugalo kwa kushirikiana na New Life Band (NLB) kutoka Arusha. Sifa na Utukufu kwa Mungu Muumba wa Mbingu na Nchi maana ni Yeye aliyewezesha Mkesha huu uwe wa Mafanikio.

Mungu Awabariki wote mlioshiriki katika Mkesha huu wa Kusifu na Kuabudu, naamini hakuna anayejutia kushiriki. Huu ni mwanzo wa Matamasha mengine mengi kama haya, this is just Chapter One of the The Night of Impact, Praise & Worship Explosion Series. So stay tuned..

Barikiwa kwa baadhi ya picha za matukio ya Siku hiyo.
Mchungaji Kiongozi wa T.A.G ICC Lugalo, Mch. Raphael Kitine akiwe na Mkewe katika Mkesha

 Kutoka kushoto ni Askofu Jonas Mkane, Mchungaji Raphael Kitine na Mama Mchungaji Kitine

Mass Choir kutoka T.A.G ICC Lugalo ikihudumu katika Mkesha huu  wa The Night of Impact 2017

New Life Band (NLB) toka Arusha wakilitendea haki Jukwaa katika Mkesha wa The Night of Impact

New Life Band toka Arusha na Mass Choir toka T.A.G ICC Lugalo Wakihudumu kwa pamoja

Mwalimu Makwaya toka Arusha alikuwepo kufundisha katika Mkesha huu