Saturday, 7 October 2017

MATESO YA MWENYE HAKI [SEHEMU YA I]

MUHUBIRI: 
Mch. Raphael Kitine
[Mchungaji Kiongozi, T.A.G ICC Lugalo]
[+255767354777; +255784354777; +255719354770]
E-mail: raphaelkitine@yahoo.co.uk
ANDIKO KUU: 
ZABURI 34:19
“Mateso ya mwenye haki ni mengi, Lakini Bwana humponya nayo yote.”

I. UTANGULIZI
(i) Maana ya Mwenye Haki
> Ni hali ya Mtu kuwa na Ukamilifu kimaadili na kiroho ili kukubalika na Mungu katika Ufalme wake.
(ii) Nani Mwenye Haki?
1. Ni Mtu anayeishi kwa Imani na kumtegemea Mung katika mambo yote. Ebr 10:38
2. Ni Mtu aliyekubali kuacha uovu na kuepukana na anasa za Dunia. Ayubu 1:8
3. Ni Mtu aliyepata kibali machoni kwa Bwana. Mwanzo 6:8
4. Ni Mtu anayeishi maisha Matakatifu. Ayubu 12:4
(iii) Maana ya Mateso
1. Maana ya Neno Mateso
>Ni hali ngumu anayopitia Mtu na kumsababishia mauimivu ya kimwili au kisaikolojia.
2. Mifano ya Mateso:Rum 8:35-36;Mdo 14:19;16:22-23
>Mateso ya mwili kama Magonjwa, njaa n.k
>Mateso ya Kisaikolojia kama msongo wa mawazo kutokana na kukosa pesa, migogoro katika familia, n.k
(iv) Biblia Inasemaje Kuhusu Mateso ya Mwenye Haki?
Tujapopita katika mateso ya Dunia hii tutambue kuwa:
1. Mungu ni mwema na Mwaminifu Yeye atatuponya na kutuvusha. Zab 34:19; 1Kor 10:13
2. Mateso hayapaswi kututenga sisi na Upendo wa Mungu Baba. Rum 8:35-36
3. Hatuko peke yetu bali Mungu yupo pamoja nasi. Mt 28:20
4. Mungu siye Mwenye makossa na hatupaswi kumkufuru Yeye. Ayubu 2:9-10
5. Inatupasa kuvumilia mpaka mwisho. Mt 10:16-22

II. KWANINI MUNGU AMERUHUSU MATESO?
i. Lipo swali la kale kama vile chozi la kwanza, na vilevile ni swali jipya kabisa kama vile habari za hivi punde:
Kwanini? Kwanini Mungu aruhusu mateso, huzuni, maumivu ya moyo, na mauti/kifo, hata miongoni mwa watoto wake?
ii. Swali hili liliulizwa na Ayubu, na limekuwa likiulizwa na kila Mtu aliyepita katika uso wa Dunia na aliyemwamini Mungu.
iii. Jibu nililolipokea kutoka katika Neno la Mungu lilikuwa lenye kutia moyo sana kwangu kiasi cha kujawa shauku ya kuwashirikisha..
1. MATESO HUUFANYA ULIMWENGU USIWE WENYE KUVUTIA 1Yoh 2:15
i. Biblia inatuambia kuwa “Tuwapitaji” na “Wasafiri”
>Ulimwengu huu sio makazi yetu ya kweli. 1Pet2:11
>Mungu Ametuandaa kitu chema kwa ajili yetu. 2Kor 5:1
ii. Kama kusingekuwepo Mateso
>Asingekuwepo hata mmoja anayetamani kuuacha Ulimwengu huu
>Kusingekuwa na mwenye shauku ya makazi ya milele (kudumu) na hivyo kujiandaa kwaajili yake.
2. MATESO YANATUFANYA KUTHAMINI YALE TULIYOTENDEWA NA MUNGU. Zab 95:2
i. Wote katika maaishaa yetu hupokea mengi mema kutoka kwa Mungu. Lk 17:14-17
>Ni rahisi kusahau kuwa tumepewa na Mungu
>Bila yaa kupokea kwa shukrani nyingi kwa Mungu
ii. Mateso hutufanya kushukuru na kuthamini Zaidi. Dan 4:33-34
>Kushukuru kwa ajili ya afyaa njema
>Na mafanikio yote katika maisha yetu
3. MATESO HUTOA NAFASI YA KUNYAMAZISHA MAADUI WA MUNGU. 1Pet 2:15
i. Unakumbuka kilichotokea kwa Ayubu. Ayubu 1:11
>Shetani alitaaka kumdhalilisha Mungu juu ya Ayubu, > kwamba anamtumikia Mungu kwa saabu tu Mungu Amembariki.
>Lakini uvumilivu wa Ayubu katika mateso ulimyamazisha shetani
ii. Kwa unyenyekevu kuvumilia, au kutenda mema wakati wa mateso..
>Thamani ya Ukristo hakika hung’aa katikati yake
4. MATESO YANATUFANYA TUMTEGEMEE MUNGU ZAIDI. Mith 3:5
5. MATESO YANATUWEZESHA KUOMBA KWA BIDII. Mdo 12:5
6. MATESO HUTUSAIDIA KUTUTAKASA. 1Pet 1:7
i. Zingatia umuhimu wa vifungu vya Maandiko haya:
> 1Pet 1:6-7 Mateso yaweza kuwa kama moto utakasao dhahabu
> Yak 1:2-5 Kukua na kuimarika kwa Mkristo kunaweza kutokea kutokana na majaribu anayopitia. Yak 1:3-4

SOMO HILI LITAENDELEA...
KARIBU SANA T.A.G ICC LUGALO KWANI SOMO HILI NDO LINAFUNDISHWA KWA SASA.
MUNGU AKUBARIKI.