Siku ya leo Mungu ameendelea kusema na Watu wake kupitia kwa Mtumishi wa Mungu Mch. Ephraim Mahondo kutoka Kanisa la T.A.G Kiwele. Somo alilofundisha katika Ibada ya Pili ni "Mambo Matatu Yatakayokusaidia Kupokea Muujiza Wako".
Mchungaji Ephraim Mahondo akihudumu katika Madhabahu ya ICC Siku ya leo.
Kwa kawaida katika Kanisa la ICC huanza na Ibada ya Kusifu na Kuabudu ndipo hufuata kipindi cha kusikiliza Neno la Mungu. Timu ya Kusifu na Kuabudu ilitimiza jukumu lake kikamilifu la kuwaongoza Waamini wote katika Ibada hii.
Timu ya Kusifu na Kuabudu ya ICC ikiwaongoza Waamini wote kumsifu na kumwabudu Mungu katika Roho na Kweli
Mchungaji Kiongozi wa ICC, Mch. Raphael Kitine akiwa sambamba na Timu ya Kusifu na Kuabudu wakati wa maombezi
Waamini wa ICC wakiwa katika Ibada ya Kusifu na Kuabudu
Baada ya Ibada ya Kusifu na Kuabudu, Ibada ya Neno la Mungu ikafuata.
Mhubiri: Mch. Ephraim Mahondo (T.A.G - KIWELE)
Maandiko: Yohana 9:1-12; Zaburi 34:19
* Siku ya Leo Mungu kasema na Kanisa Lake kupitia kwa Mtumishi wake ujumbe muhimu sana kuhusu mambo ya msingi ya kuzingatia ili kupokea muujiza. Amefundisha kuwa watu wengi siku hizi wamekuwa wepesi sana kukimbilia maeneo mbalimbali kukimbilia miujiza bila ya kujua mambo ya msingi. Kwani Biblia haituambii tufuate miujiza na baraka, bali miujiza na baraka vitatufuata.
Waamini wa ICC wakifuatilia mafundisho ya Neno la Mungu kwa umakini.
Kwa kifupi mambo matatu ya msingi ya kuzingatia yaliyofundishwa leo ni;
1. Yesu:
> Tukifuata na kutii maagizo yake, bila shaka ni lazima utapokea muujiza wako.
2. Mchungaji wako anayekulea Kiroho:
> Mchungaji anayekulea Kiroho, hasa wa Kanisa la mahali pamoja ni kiungo muhimu sana kwa muamini kupokea baraka na muujiza wako. Hivyo tunapaswa kuwasikiliza kwa umakini.
3. Mtu Mwenyewe Binafsi:
> Kila mtu binafsi anawajibu mkubwa sana katika kuhakikisha anapokea muujiza wake. Ukifatilia watu wote katika Biblia waliopokea Miujiza yao, kuna wajibu walioutimiza. Hivyo mpendwa, unashauriwa kutimiza wajibu wako ili upokea muujiza wako.
Ubarikiwe, Karibu ICC.
NB: Jumamosi hii ijayo ya Tarehe 06/12/2014 ni Siku Maalumu ya Vijana ambao hawajaoa/hawajaolewa au kwa kifupi ni ICC Single's Day. Siku hiyo itafanyika katika eneo la Mkwawa Magic Site, Manispaa ya Iringa. Kwa Vijana wote ambao watapenda kushiriki naomba tuwasiliane kupitia namba zifuatazo za waratibu wa Siku hii.
1. Mr. Chanai Emmanuel - 0755930595;
2. Ms. Joyce Senje - 0764858736