Saturday, 27 December 2014

SEMINA YA NENO LA MUNGU YA KUFUNGA MWAKA 2014

Shalom!

Mungu ni mwema wakati wote.

Kuelekea mwisho wa mwaka 2014, Kanisa la T.A.G - I.C.C limeandaa Semina ya Neno la Mungu katika kumaliza mwaka huu. Semina hii itaambatana na maombi ya kufunga na kuomba;  Ni kila Siku saa kumi kamili jioni kuanzia tarehe 26/12/2014 hadi tarehe 31/12/2014.
Tafadhali usikose Semina hii muhimu sana, MUNGU akubariki.

Mchungaji Kiongozi wa ICC Mch. Raphael Kitine akihudumu katika madhabahu ya ICC

Tuesday, 23 December 2014

KAZI ZA ROHO MTAKATIFU KATIKA MAISHA YA MWAMINI

Na. Mch. Raphael Kitine (Mchungaji Kiongozi ICC)
Andiko Kuu: Yohana 16:5-15

I. UTANGULIZI:
  • Yohana 16:5-15 ni mistari ya msingi kuhusu Roho Mtakatifu.
  • Katika mistari hii, Yesu anawaambia Wanafunzi kwamba mambo yatakuwa magumu mara tu akitoweka na ya kwamba watu watawachukia.
  • Hivyo anawafariji kwa Ujumbe wa Roho Mtakatifu kwa kuwaambia kuwa "... ni faida kwao ikiwa ataondoka maana atatuma msaidizi..".
Waamini wa ICC wakifatilia Mahubiri Ibadani.
II. NAMNA 5 ROHO MTAKATIFU ANAFANYA KAZI KATIKA MAISHA YA MWAMINI:
1. Roho Mtakatifu Hujua udhaifu wetu.
  • Roho Mtakatifu haishii kutujua tu, hutusaidia pia katika udhaifu wetu. Rumi 8:26;
  • Hutuwezesha kufanya mambo tusingeweza kufanya kwa uwezo wetu wenyewe. Kama linampa Yesu Utukufu na linahusu watu wake na Kanisa lake, Roho Mtakatifu anatutaka tuangalie hilo na atafanya kazi nasi na kututia nguvu.
2. Roho Mtakatifu Hutufundisha.
  •  Roho Mtakatifu hufanya kazi kupitia Maandiko na watu kubadilisha mioyo yetu. Yohana 14:26; Rumi 8:14; 1 Kor 2:6-14;
  • Tunaposhindwa kuelewa fungu fulani katika Biblia, Roho Mtakatifu hutufundisha kulielewa na namna ya kulitumia katika maisha yetu. Rumi 10:14-16.
 3. Roho Mtakatifu Hufanya kazi kupitia maombi.
  •  Roho Mtakatifu hutuombea kupitia maombi. Rumi 8:26;
  • Hutuombea hasa tunapoweka mkazo katika kumpa Yesu Utukufu na kupenda watu wake;
  • Iwapo hujui nini cha kuomba, muombe Roho Mtakatifu maana Yeye ni "Msaidizi" atakayewasaidia wote wampendao.
  • Mara nyingi Mungu hutumia maombi kubadili mioyo yetu ili tuzidi kumuelekea Yeye.
 4. Roho Mtakatifu Hufunua kusudi la Yesu kwetu.
  •  Mungu hutoa vipawa. Alitupa Yesu, aliyefia dhambi zetu msalabani. Alitupa Roho Mtakatifu;
  • Alitupa mwongozo wa namna ya kuishi maisha yetu kupitia Biblia. 2 Tim 3:16-17;
  • Asilimia 95 ya kusudi la maisha yetu tunaipata kwenye Biblia;
  • Kusudi la maisha yetu ni kumpa Yesu Utukufu kwa Nguvu za Roho Mtakatifu na kuwapenda watu;
  • Roho Mtakatifu atatufunulia undani wa kusudi letu - mfano tufanye kazi gani na wapi, utaoa/kuolewa na nani, utaishi wapi n.k kadri tunavyosoma Biblia na kuishi kwa Imani.
 5. Roho Mtakatifu Hutushuhudia juu ya dhambi.
  • Yohana 15:8-11 inatufundisha kwamba Roho Mtakatifu hutushuhudia dhambi ilituvae taswira ya Yesu;
  • Tunavyokaa zaidi ndani ya Roho Mtakatifu, dhambi huwekwa wazi katika maisha yetu. Galatia 5:16, 18;
  • Hii hutuwezesha kutubu na kuhitaji kubadilishwa na Yesu ili tuvae ufanano wake.
III. HITIMISHO:
  • Kama wewe ni Mwamini Roho Mtakatifu Huishi ndani yako.
  • Jiachilie huru kwa Nguvu za Roho Mtakatifu.
  • Yesu anamwita Msaidizi kwasababu nzuri. Kwa hakika ni faida kuwa maishani mwetu; kumpa Yesu Utukufu ndio hasa sababu ya kutumwa kwetu. Yohana 15:26-27.

Mchungaji Raphael Kitine akihitimisha somo hili, huku Timu ya Kusifu na kuabudu ikiongoza katika kuabudu.

Zifuatazo ni Picha mbalimbali za Ibada ICC:
Mch. R. Kitine akiongoza maombezi ya Roho Mtakatifu, akiwa sambamba na Wachungji wasaidizi wa ICC; Kutoka kushoto ni Mch. R. Kyando akifuatiwa na Mch. O. Kipemba.


Waamini wa ICC wakati wa Ibada ya Kusifu na Kuabudu.


Kwaya ya PATMO ikihudumu katika madhabahu ya Bwana ICC

Sunday, 7 December 2014

AINA YA MTUMISHI MUNGU ANAMTENGENEZA

Na: MCh. Omega Kipemba (ICC)
Andiko Kuu: 2Tim1:7.
Mch. Omega Kipemba akihubiri na kufundisha katika Madhabahu ya ICC

Kama ilivyo ada, kabla ya kusikiliza Neno la Mungu, hutangulia Ibada ya Kusifu na Kuabudu.


Baada ya Ibada ya Kusifu na Kuabudu, muda wa kusikiliza Neno la Mungu ukawadia.

UTANGULIZI:
1. Uhusiano wa Paulo na Timotheo ulikuwa ni ule wa Baba na mtoto. 2Tim 1:1-2
2. Kama baba alimhamaisha Timotheo; 2 Tim 1:6-7

Swali la kujiuliza.
Mungu anakusudia mtumishi aweje?
Soma 2Tim 1:7

I. MOYO WA KIASI (SELF-CONTROL)
> MOYO WA KIASI-Inahusisha kujipa nidhamu mwenyewe,kujimudu mwenyewe kuwa aina ya mtu anayetembea na Mungu na wengine kwa namna ipasayo.
> Kusimama kwenye milango ya utu wetu kuruhusu au kukataa mambo fulani kupita.
> Kutupilia mbali ushawishi hatarishi wenye uwezo wakutuvamia na kutushinda.
> Tunachunga kitokacho,kile tusemacho,tuendako,tutendacho,au kile tunachokidhihirisha kwa wengine.

* Ni sifa ya Mkiristo aliyekua kiroho
i) Askofu (mzee)awe mtulivu(sober sophrone), Tito 3:2; Tito 1:8
ii) Wazee wawe watulivu(sophrone). Tito 2:2
iii) Akina mama wawafundishe (sophronizo) mabinti;
      (a) Kuwa watulivu (sophronizo). Tito 2:4
      (b) Kuwa makinifu(discreet) (sophrone). Tito 2:5

II.MTUMISHI ASIYE NA WOGA
A] Mtumishi wa Mungu haanzi mara nyingi na ujasiri. Mt 14:30; 26:69-75; Gal 2:11-12; 1kor 2:3
B] Hata hivyo ujasiri wa watumishi ulikua. Mdo 4:13; 20:24; 21:13

III. MTUMISHI IMARA

A] Watumishi huanza kwa udhaifu. Mt 26:40-41; 1 kor3:1
B] Hatimaye wanahamasishwa. 1kor16:13; Efeso 6:10

* Mungu humtengeneza mtumishi:
1.Kwa maombi. Mdo 4:29-31; Ef 6:18-19
2. Kukua kwa imani na upendo. 1Yohana 4:18;  Mt 8:26
3. Kwa kutupa silaha sahihi. Ef 6:10-17
4. kwa kutupa Roho mtakatifu. Ef 3:16,20
5. kwa kutupa uhusiano na mwanae. Yn15:5; Fil 4:13
6. Kwa kutupenda. 1Yn 4:10-11; 1 Thes 4:9-10
7. Kwa kumtoa Yesu kristo kama mfano wa upendo. 1Thes 3:16;   Yn 13:34-35.

Mungu akubariki.

SINGLE's DAY 2014

Shalom!

Mungu ni mwema wakati wote, hatimaye ile siku maalumu iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu, Siku ya Vijana ambao bado hawajaoa/hawajaolewa a.k.a Single's Day imefanyika jana Tarehe 06/12/2014.

Mungu awabariki Vijana wote mlioshiriki kikamilifu. Hitimisho la Single's Day mwaka huu 2014 ndio mwanzo wa Single's Day 2015, hivyo naomba tuendelee kushirikiana ili Single's Day ya mwaka 2015 iwe ya mafanikio zaidi kuliko ya mwaka huu au mwaka jana.

Zifuatazo ni baadhi ya picha za Siku hiyo.