Wednesday, 28 March 2018

PRAISE AND WORSHIP OVERNIGHT CONCERT "THE NIGHT OF IMPACT SEASON II" 06/04/2018

Shalom!

HAYAWI HAYAWI SASA YAMEKUWA; NI IJUMAA TAREHE 06/04/2018!
Kwa mara nyingine tena Kanisa la T.A.G ICC Lugalo (Iringa Mjini) chini ya Mch. Raphael Kitine, kwa kushirikiana na New Life Band kutoka Arusha wanakuletea Tamasha kubwa la Mkesha wa Kusifu na Kuabudu linalotambulika kwa jina la "THE NIGHT OF IMPACT SEASON II". Karibu Tumsifu na Kumwabudu Mungu wetu. Zaburi 146:1 - 2; 147:1.

Tamasha hili kubwa la Kusifu na kuabudu litafanyika katika Ukumbi wa St. Dominic uliopo Iringa Mjini Siku ya Ijumaa Tarehe 06/04/2018 kuanzia saa 12:00 Jioni hadi 12:00 Asubuhi. Ibada ya Kusifu na Kuabudu itaongozwa na New Life Band kwa kushirikiana na Mass Choir inayojumuisha Timu ya Kusifu na Kuabudu ya T.A.G ICC Lugalo kushirikiana na Waimbaji toka Makanisa mbalimbali Iringa Mjini. Pia Vikundi mbalimbali vya Uimbaji vitakuwepo:Pizzicato, The Rhythm, Salvation Voices, Vessels of Praise, Faith Choir. Timu za Kusifu na Kuabudu toka Fellowship mbalimbali kama vile TAFES, PSA, TMCS, USCF, CASFETA, TAYOMI, TUCASA, CCT, toka Vyuo mbalimbali vya Iringa zitakuwepo kama vile Chuo Kikuu Mkwawa (MUCE), Chuo Kikuu Iringa (Tumaini), Chuo Kikuu cha Kikatoliki (RUCU), Chuo cha Maendeleo (CDTI), Chuo cha Afya (PHCI), VETA n.k. Kutakuwa na Fursa ya kujifunza Neno la Mungu kupitia kwa Mch. Yosiah Nehemia kutoka Arusha. Tafadhali usipange kukosa, kumbuka Mungu wetu anapendezwa na Sifa. Kila Mwenye Pumzi na Amsifu Bwana. HALELUYA. Zaburi 150:1 - 6.

USAFIRI WA BURE UTAKUWEPO KUTOKA VYUO MBALIMBALI KAMA VILE CHUO KIKUU MKWAWA, CHUO KIKUU CHA IRINGA (TUMAINI) na CHUO CHA MAENDELEO (CDTI)  IPOGOLO.
Watu wooootee mnaalikwa kushiriki. HAKUNA KIINGILIO.

KWA UFAFANUZI ZAIDI TUWASILIANE KWA NAMBA ZA SIMU ZIFUATAZO:
+255 767 354 777; +255 784 354 777; +255 354 770

No comments:

Post a Comment