Monday, 29 September 2014

IJUE CA's - IDARA YA VIJANA

Muh: Mwl. Ezekiel Fungo
Mkurugenzi wa Idara Ya Vijana (CA’s) - Iringa Central Church (ICC):

UTANGULIZI: 2 Kor 5:20
CA’s ni ufupisho wa maneno ya Kiingereza CHRIST AMBASSADORS, maana yake kwa Kiswahili ni MABALOZI WA KRISTO au WAJUMBE WA KRISTO.
Mkurugenzi wa Idara ya Vijana (CA's) ICC, Mwl. Ezekiel Fungo akiwa Madhabahuni ICC

MAKUSUDI YA IDARA YA VIJANA (CA’s):
1. KUSHUHUDIA;
2. KUABUDU;
3. KUJIFUNZA NENO;
4. KUTUMIKA;
5. USHIRIKA;
6. KUJIFUNZA UONGOZI;
7. KUTEKELEZA DIRA YA MAENDELEO YA KANISA LA TAG.

1. KUSHUHUDIA.  MATH 28:19-20
> Idara ya Wajumbe wa Kristo itawaandaa Wajumbe wa Kristo kwa mafunzo mbalimbali na kuwahamasisha ili kwa kutumia mbinu na njia mbalimbali waweze kufanya Uinjilisti wenye nguvu utakaowawezesha kuwaleta watu wenye dhambi kwa Yesu, ambao nao wataandaliwa ili wawe wavuna roho za watu na kulitimiza Agizo Kuu. Math 28:19-20.

A. KUSUDI HILI LITATEKELEZWA KWA NJIA ZIFUATAZO:
i). Ushuhudiaji wa mtu kwa mtu;
ii). Ushuhudiaji wa nyumba kwa nyumba;
iii). Ushuhudiaji katika maeneo mbalimbali; kama vile Masokoni, Mashuleni, Vyuoni, Hospitalini, Magerezani na maeneo yote ya mikusanyiko inayoweza kufikiwa.
iv). Kushuhudia kwa kugawa tracts, machapisho mbalimbali ya Neno la Mungu na njia nyinginezo kama Roho Mtakatifu anavyowaongoza kufanya.

> Ili Kijana aweze kuishi maisha yanayo mlingana Yesu Kristo na kuwa shahidi wa Yesu lazima awe ameandaliwa.       Luka 2:41-52; Luka 3:23.

B. SIFA ZA KIJANA/MTU ANAYESHUHUDIA:
i). Awe amezaliwa mara ya pili na amejazwa na Roho Mtakatifu. Mdo 1:8; Mdo 2:37 – 41; Mdo 4:13.
ii). Awe anaishi maisha matakatifu (Nuru ya Ulimwengu).        Math 5:14 - 16.
iii). Awe mwombaji mwenye mzigo kwa watu ambao hawajaokolewa.  Mdo 17:16 – 23.
 iv). Awe amejaa Neno la Mungu. 1Tim 2:1 – 4.
 v). Awe na mwenendo mzuri katika maisha yake.
 vi). Awe ameandaliwa. Mdo 8:14 – 17.
vii). Awe na ujasiri wa kumuhubiri/kumtangaza Yesu Kristo.     Mdo 4:8 – 13.

C. SABABU ZA KUSHUHUDIA WENYE DHAMBI:
1) Wenye dhambi wamekufa wametenganishwa na Mungu.
 > Wanahitaji ufufuo au kuzaliwa mara ya pili. Ef 2:1-2
2) Wenye dhambi wamepotea wanahitaji Wokovu (Ukombozi). Luka 15:11-24.
 > Hawako mikononi mwa Mungu;
> Hawajui jinsi ya kumrudia Mungu.
3) Wenye dhambi wanahitaji kurudi mikononi mwa Mungu, wanahitaji Wokovu. Luka 19:10.
4) Wenye dhambi ni watumwa wanahitaji kununuliwa na damu ya Yesu. Yn 8:34.
5) Wenye dhambi wanamilikiwa na kuongozwa na shetani.        Rm 6:16, 20.

6) Yesu Kristo alitoa fidia maisha yake kwa wote wenye dhambi. 1 Kor 6:20; Gal 3:13; 1 Pet 1:18.
7) Yesu yuko tayari kuwa weka huru wenye dhambi wanaomwendea. Gal 5:1.
8) Wenye dhambi ni vipofu wanahitaji mwangaza.    2 Kor 4:4; Mdo 26:18; Kol 1:13.
9) Wenye dhambi ni waasi wanahitaji kupatanishwa.
> Wenye dhambi ni maadui wa Mungu. Rm 5:10; Tito 3:3; Yak 4:4.
10) Mungu hafurahishwi na kifo cha mtu mwenye dhambi. Ez 33:11.
11) Wenye dhambi wanahitaji kutubu kwa Bwana Yesu. 2 Kor 5:19 – 21; Kol 1:20; Mdo 17:30 – 32.

Waamnini wa ICC wakifuatilia somo kwa umakini mkubwa.
NB: Somo hili litaendelea Jumapili ya kilele cha Wiki ya Sikukuu ya Idara 05/10/2014. Ibada itakuwa moja kuanzia saa mbili kamili hadi saa tano na nusu Kanisani ICC (Sabasaba), watu wote mnakaribishwa.

Sunday, 28 September 2014

Wimbo wa UZinduzi wa Wiki ya Sikukuu ya Vijana (CA's) ICC - Leo ni Siku Njema

IDARA YA VIJANA (CA's) ICC YAZINDUA WIKI YA SIKUKUU YA CA's:

Hatimaye Idara ya Vijana CA's imefanikiwa kuzindua Wiki ya Sikukuu ya Idara (Vijana) ambayo kilele chake ni Jumapili ijayo ya tarehe 05/10/2014. Makanisa mengi ya TAG huwa na taratibu ya kuadhimisha Sikukuu za idara Jumapili iliyopangwa Kitaifa. Ila kwa ICC kuna utaratibu wa tofauti ambapo huwa kuna siku ya uzinduzi na siku ya hitimisho.

Kwaya ya Idara ya Vijana (CA's) ICC ikiwa madhabahuni tayari kwa uimbaji siku ya leo.

Pia katika wiki nzima Idara husika hufanya shughuli mbalimbali zinazoendana na malengo ya Idara husika. Kwa upande wa Idara ya Vijana ICC siku ya Jumatatu na Jumanne (29 & 30/10/2014) tutakutana Kanisani Vijana wote, Siku ya Jumatano (01/10/2014) Kanisa lote tutakuwa na Ibada ya Ijue Biblia kama kawaida pia tutakuwa na Mkutano wa Injili utakaofanyika Eneo la Kihesa kuanzia siku ya Alhamisi (02/10/2014) hadi Jumamosi (04/10/2014). Watu wote mnakaribishwa.

Aliyehubiri siku ya leo ni Mkurugenzi wa Idara ya Vijana (CA's) ICC Mwl. EZekiel Fungo, alifundisha somo linalosema IJUE CA's; kwani inaonekana Waamini wengi hawaijui vizuri CA's. .
Mwl. Ezekiel Fungo (Mkurugenzi wa Idara ya Vijana ICC) akifundisha siku ya leo katika uzinduzi wa Sikukuu.

Waamini wa ICC walitulia kwa umakini mkubwa wakimfuatilia Mwl. E. Fungo akifundisha somo hili la Ijue CA's. Somo kamili litawajia hapahapa. Mungu akubariki

Sunday, 21 September 2014

HITIMISHO LA SOMO LA IMANI POTOFU - JINSI MWAMINI ANAVYOWEZA KUJIKINGA NA MADHARA YA IMANI POTOFU

Shalom!
Katika Ibada ya leo ICC (Sabasaba) Mchungaji Kiongozi Mch. Raphael Kitine amehitimisha somo la Imani Potofu ambalo amefundisha mfululizo kwa wiki kadhaa.
Mch. Raphael Kitine akiwa katika Madhabahu ya ICC kuhitimisha Somo la Imani Potofu.

Kama ilivyo kawaida ya Mch. R. Kitine huanza kufundisha kwa kufanya marejeo ya Somo lililopita ili kupata muendelezo mzuri wa Somo la leo.

Baada ya marejeo ya somo lililopita alianza Somo la leo kuhusu Imani Potofu katika kipengele cha "Jinsi Mwamini anavyoweza kujikinga na madhara ya Imani potofu".

Mch. Raphael Kitine akiendelea kufundisha somo la Imani Potofu. Somo kamili sehemu ya leo ni kama ifuatavyo.

Maandiko ya Somo:
Mathayo  7:15 - 18; 1 Wafalme 18:21 - 40.

Somo: JINSI MWAMINI ANAVYOWEZA KUJIKINGA NA MADHARA YA IMANI POTOFU.
i. Jiepushe kusikiliza au kuangalia mafundisho ya mtumishi usiyemjua undani wake kiimani.
ii. Jiepushe mijadara au malumbano ya kiimani na watu usio wajua undani wao kiimani.
iii. Jiepushe kusoma vitabu vya masomo ya kiroho vya mwandishi usiyemjua undaani wa imani yake.
iv. uwe mwamini mwenye kuongozwa na roho wa Mungu.
v. Uwe mwamini mwenye kujitegemea kimaandiko.
vi. Kuwa makini na watu wakwambiao yale upendayo kusikia tu, kwamba kila kitu ni shwari.
> Watu huchukulia udhaifu wa binadamu ili kuteka nafsi yako.
vii. Pima mafundisho kwa vipimo sahihi vya kiroho.
> Neno la Mungu linasemaje kuhusu hilo fundisho?
> Je, mtumishi huyo anafundisha lile analolitendea kazi?

HITIMISHO:
> Imani potofu zipo kwa ajili ya kuithibitisha Imani sahihi, "Katika Bwana tunashinda na zaidi ya kushinda".
Mch. Raphael Kitine akihitimisha Somo la Imani potofu.

Wakati wote wa mahubri Waamini wa ICC walikuwa katika hali ya utulivu na umakini wa hali ya juu kufuatilia somo.






Wednesday, 17 September 2014

IMANI POTOFU


Na: Mch. Raphael Kitine 

MAANDIKO YA SOMO:  
Mt 7:15-18; 1Fal 18:21-40
I.                   UTANGULIZI
i.         Maelezo kuhusu Imani potofu
Ø  Imani potofu, kwa ufupi,  ni Imani ambayo wanaoifuata hawawezi kumuona Mungu wakiwa hai na hata watakapokufa.

Ø  Ziko Imani potofu ambazo ni rahisi kuzitambuwa kwa kuwa hupingana wazi wazi na mpango wa Mungu wa kumkomboa mwanadamu kupitia Yesu Kristo. Lakini zipo Imani zingine ambazo kwa haraka haraka unaweza kudhani ni kwa ajili ya kumsaidia binaadamu aweze kumuona Mungu. Hizi hutaja jina la Yesu na hufundisha baadhi ya mambo ambayo hata Bwana Yesu mwenyewe alifundisha. Lakini kwa undani wake kuna mengi ya kupotosha!
ii.        Maana ya imani potofu
Ø  Ni kikundi cha watu wanaoabudu kinyume cha kweli za Kibiblia Rm 1:18;24-25

Ø  Ni watu wanaovaa nje ngozi ya kondoo lakini ndani ni mbwa mwitu wakali Mt 7:15
iii.       Asili ya Imani potofu 2Kor 11:13-15
Ø  Kutoka kwa shetani na majeshi yake Efeso 6:12

Ø  Baada ya kuasi anafanya kila awezavyo kuipinga kazi halali ya Mungu Dan 10:12-13

II.                 MALENGO YA IMANI POTOFU
i.         Kuidhohofisha imani sahihi Mt 13:24-30;36-39
Ø  Kazi ya magugu ni kudhohofisha mmea halisi na kuufanya ushindwe kukua vizuri

Ø  Imani potofu husababisha kanisa sahihi la Mungu lishindwe kukua vizuri
ii.        Kupotosha ukweli wa maandiko 2Pet 3:16
Ø  Mungu husema na watu wake kwa kutumia maandiko

Ø  Kazi ya imani potofu ni kuvuruga mawasiliano kati ya Mungu na watu wake kupotosha maana ya halisi ya maneno ya Mungu
iii.       Kuwafanya watu washindwe kumwona Mungu Mdo 12:20-23
Ø  Kwa kuwapofusha macho ya Rohoni

Ø  Kwa viongozi wa dini husika kujitukuza na kuchukua nafasi ya Mungu

III.              JINSI YA KUZITAMBUA IMANI POTOFU
i.         Kuujenga mwili kuliko roho Mt 6:31-33; Flp 3:17-20
Ø  Maombezi ya kimwili huchukua sehemu kubwa kuliko ya Kiroho

Ø  Mafundisho ya uponyaji wa kimwili huchukua nafasi kubwa zaidi kuliko ya kiroho
Ø Mafundisho ya mafanikio ya kimwili huchukua nafasi zaidi kuliko utakatifu
ii.        Nguvu inayotumiwa siyo ya Mungu Mt 7:22-23
Ø  Nguvu inayotumiwa inafanana kama ya Mungu lakini si Mungu

Ø  Nguvu ya kishirikina inatumiwa kufanya miujiza mbalimbali

Ø  Dalili ni matumizi haba ya jina la Yesu katika huduma
iii.       Kuona dhambi si kitu (Minimize Sin) 1Kor 5:1-2
Ø  Dhambi haipewi nafasi ya kukemewa

Ø  Watu wanaachwa kufanya wapendavyo

Ø  Hakuna hatua zinazochukuliwa kwa watenda dhambi
iv.       Hupiga vita imani sahihi 1Kor 14:32-33
Ø  Huzidhohofisha imani sahihi kwakuzipiga vita

Ø  Hutumia lugha za matusi na kejeli juu watumishi wa imani sahihi
v.        Humfanya Mungu kama mwanadamu (Humanize God)          Rm 1:21-25
Ø  Kuishusha hadhi ya Mungu

Ø  Huduma hazimpi Mungu utukufu
vi.       Kuwa kinyume na maandiko (Ostracize The Scriptures)           Gal 3:10; 2Tim 3:5-7
Ø  Hufundisha mambo yanayopingana na maandiko

Ø  Hupotosha tafsiri sahihi ya neno la Mungu
vii.      Watumishi kuchukua nafasi ya Mungu (Deify Man )             2Thes 2:3-4; 2Timotheo 3:1-4
Ø  Badala ya huduma kumtukuza Mungu huwatukuza watumishi binafsi

Ø  Majina ya watumishi kuchukua nafasi ya jina la Mungu
viii.     Kutoamini wokovu/au kuamini kwa njia isiyo sahihi 2Kor 6:14; Gal 1:6-9
Ø  Mafundisho na mahubiri yao hayatoi msisitizo wa wokovu kwa wanadamu

Ø  Mafundisho na mahubiri yao hayatoi msisitizo wa mtu kuisha maisha matakatifu

Ø  Msisitizo wa mafundisho ni utowaji sadaka kuliko utakatifu