Sunday, 21 September 2014

HITIMISHO LA SOMO LA IMANI POTOFU - JINSI MWAMINI ANAVYOWEZA KUJIKINGA NA MADHARA YA IMANI POTOFU

Shalom!
Katika Ibada ya leo ICC (Sabasaba) Mchungaji Kiongozi Mch. Raphael Kitine amehitimisha somo la Imani Potofu ambalo amefundisha mfululizo kwa wiki kadhaa.
Mch. Raphael Kitine akiwa katika Madhabahu ya ICC kuhitimisha Somo la Imani Potofu.

Kama ilivyo kawaida ya Mch. R. Kitine huanza kufundisha kwa kufanya marejeo ya Somo lililopita ili kupata muendelezo mzuri wa Somo la leo.

Baada ya marejeo ya somo lililopita alianza Somo la leo kuhusu Imani Potofu katika kipengele cha "Jinsi Mwamini anavyoweza kujikinga na madhara ya Imani potofu".

Mch. Raphael Kitine akiendelea kufundisha somo la Imani Potofu. Somo kamili sehemu ya leo ni kama ifuatavyo.

Maandiko ya Somo:
Mathayo  7:15 - 18; 1 Wafalme 18:21 - 40.

Somo: JINSI MWAMINI ANAVYOWEZA KUJIKINGA NA MADHARA YA IMANI POTOFU.
i. Jiepushe kusikiliza au kuangalia mafundisho ya mtumishi usiyemjua undani wake kiimani.
ii. Jiepushe mijadara au malumbano ya kiimani na watu usio wajua undani wao kiimani.
iii. Jiepushe kusoma vitabu vya masomo ya kiroho vya mwandishi usiyemjua undaani wa imani yake.
iv. uwe mwamini mwenye kuongozwa na roho wa Mungu.
v. Uwe mwamini mwenye kujitegemea kimaandiko.
vi. Kuwa makini na watu wakwambiao yale upendayo kusikia tu, kwamba kila kitu ni shwari.
> Watu huchukulia udhaifu wa binadamu ili kuteka nafsi yako.
vii. Pima mafundisho kwa vipimo sahihi vya kiroho.
> Neno la Mungu linasemaje kuhusu hilo fundisho?
> Je, mtumishi huyo anafundisha lile analolitendea kazi?

HITIMISHO:
> Imani potofu zipo kwa ajili ya kuithibitisha Imani sahihi, "Katika Bwana tunashinda na zaidi ya kushinda".
Mch. Raphael Kitine akihitimisha Somo la Imani potofu.

Wakati wote wa mahubri Waamini wa ICC walikuwa katika hali ya utulivu na umakini wa hali ya juu kufuatilia somo.






1 comment:

  1. DAAAH IMENIKUTA SANA, SIKUWAHI KUHISI KUWA HURU KIROHO HADI NILIPOJITENGA WAZIWAZI NA MAFUNDI WA MAANDIKO KUMBE KWENYE UTEKELEZAJI MAJUMBANI MWAO HAMNA KITU. BINAFSI NAAMINI KILA NENO LA MUNGU KWA KUJARIBU KULITENDA NA KUJIKUTA NAFUNGUKIWA NA NEEMA ZINGINE WAKATI WANADAMU HUSEMA ETI BINADAMU HAWEZI KUMCHA MUNGU!! WANANIKERA SANA. WALA MIMI SIACHI KUMTENDEA MUNGU DOGO NIWEZALO JAPO HAWAACHI KUNISIMANGA.

    ReplyDelete