Sunday, 28 September 2014

IDARA YA VIJANA (CA's) ICC YAZINDUA WIKI YA SIKUKUU YA CA's:

Hatimaye Idara ya Vijana CA's imefanikiwa kuzindua Wiki ya Sikukuu ya Idara (Vijana) ambayo kilele chake ni Jumapili ijayo ya tarehe 05/10/2014. Makanisa mengi ya TAG huwa na taratibu ya kuadhimisha Sikukuu za idara Jumapili iliyopangwa Kitaifa. Ila kwa ICC kuna utaratibu wa tofauti ambapo huwa kuna siku ya uzinduzi na siku ya hitimisho.

Kwaya ya Idara ya Vijana (CA's) ICC ikiwa madhabahuni tayari kwa uimbaji siku ya leo.

Pia katika wiki nzima Idara husika hufanya shughuli mbalimbali zinazoendana na malengo ya Idara husika. Kwa upande wa Idara ya Vijana ICC siku ya Jumatatu na Jumanne (29 & 30/10/2014) tutakutana Kanisani Vijana wote, Siku ya Jumatano (01/10/2014) Kanisa lote tutakuwa na Ibada ya Ijue Biblia kama kawaida pia tutakuwa na Mkutano wa Injili utakaofanyika Eneo la Kihesa kuanzia siku ya Alhamisi (02/10/2014) hadi Jumamosi (04/10/2014). Watu wote mnakaribishwa.

Aliyehubiri siku ya leo ni Mkurugenzi wa Idara ya Vijana (CA's) ICC Mwl. EZekiel Fungo, alifundisha somo linalosema IJUE CA's; kwani inaonekana Waamini wengi hawaijui vizuri CA's. .
Mwl. Ezekiel Fungo (Mkurugenzi wa Idara ya Vijana ICC) akifundisha siku ya leo katika uzinduzi wa Sikukuu.

Waamini wa ICC walitulia kwa umakini mkubwa wakimfuatilia Mwl. E. Fungo akifundisha somo hili la Ijue CA's. Somo kamili litawajia hapahapa. Mungu akubariki

No comments:

Post a Comment