Wednesday, 27 May 2015

USAFI - MAANDALIZI YA ENEO JIPYA LA KANICA (ICC)

Shalom! Shalom! Shalom!

Hatimaye Bwana Amefanya.
ICC tumefanikiwa kupata eneo letu rasmi la kuabudia, ni jirani kabisa na Shule ya Sekondari Lugalo, muda si mrefu tutahamia mahali hapo. Sifa na Utukufu ni kwa Mungu aliye juu Mbinguni. Mungu Awabariki watu wote walioshiriki kwa namna yeyote ile kufanikisha upatikanaji wa Eneo hili.

Wiki hii ni Wiki ya kufanya usafi wa mazingira, tangu Jumatatu Idara mbalimbali za Kanisa zimekuwa zikipokezana zamu ya kusafisha eneo hilo. Kuanzia leo Waamini wote, ndugu jamaa na marafiki tunatakiwa kufika kwa pamoja ili kuongeza kasi ya kukamilisha zoezi hili la usafi.

Kwa ambao hawapafahamu panda hiace zinazopita barabara ya Dodoma (Barabara ya Kihesa), shuka kituo cha Shule ya Sekondari Lugalo. Ukifika hapo nyoosha barabara kama unaingia Shuleni, ukifika kwenye Ukumbi wa Shule, basi upo jirani kabisa na eneo la Kanisa, nyoosha barabara ndogo iliyopo sambamba na Ukumbi utaona uzio wa senyenge na geti dogo, hapo utakuwa umefika.

Kama utakwama waweza kutumia namba zifuatazo za Viongozi wa Kanisa ili wakuelekeze, Mungu akubariki.
Mr. Ezekiel Fungo (Mzee wa Kanisa): 0755974279;
Mrs. Eva Makombe (Mzee wa Kanisa): 0755161802;
Mrs. Upendo Mahinya (Mwenyekiti WWK): 0752183022.

Kwa taarifa zaidi au jambo lolote kuhusu ICC waweza wasiliana na Viongozi wa Wakuu wa Kanisa.
Namba za Viongozi Wakuu wa Kanisa. 
Mch. Raphael Kitine: 0767354777 na 0784354777 (Mchungaji Kiongozi)
Mh. Mwl. Given Lemway:  0755536791 (Mzee Kiongozi wa Kanisa)
Mwj. Oscar Mwanjala: 0754615805 (Katibu Mkuu wa Kanisa)

Zifuatazo ni baadhi ya picha za Waamini wa ICC wakifanya Usafi katika Eneo hilo.


No comments:

Post a Comment