Jumapili ya Tarehe 31/05/2015 imeingia katika historia ya Kanisa la Tanzania Assemblies of God - Iringa Central Church kuabudia katika Jengo la Sabasaba Iringa Mjini. Kanisa hili linaongozwa na Mch. Raphael Kitine, ambaye ndiye mwanzilishi wa Kanisa hili la Iringa Central Church (ICC). Historia ya kuabudu katika Jengo hili ilianza Tarehe 3/06/2001, tangu wakati huo tukatumia Jina la ICC-Sabasaba kama utambulisho wa Kanisa letu. Jumapili hii imekuwa ya Mwishooo mwisho kabisaaa kuabudu katika Jengo hili na kutumia Jina la ICC Sabasaba, kwasasa tutafahamika kama ICC Lugalo.
Hili ndilo Jengo la Sabasaba ambalo Wana-ICC tumelitumia kufanyia Ibada kwa takribani miaka 14, hatimaye imefika mwishooo.. mwisho kabisa wa kuabudu katika jengo hili.Baadhi ya Magari ya Waamini wa ICC yakiwa yameegeshwa nje ya Jengo la Sabasaba Iringa Mjini katika siku ya mwishoo.. mwishoo kabisa kuabudu katika Jengo hili la Sabasaba
Huu ndio mlango mkuu uliotumika kwa kipindi chote cha miaka 14, kuingia na kutoka katika Ukumbi wa kuabudia, ICC-Sabasaba. hatimaye imefika mwishoo, mwishoo kabisaaa wa kutumia mlango huu.
Timu ya Kusifu na Kuabudu ikihudumu katika madhabahu ya ICC Sabasaba kwa mara ya mwisho, mwishoooo kabisa.
Wanamuziki wa ICC wakitimiza wajibu wao katika Ukumbi wa Sabasaba katika Ibada ya mwisho, mwishoo kabisaa katika Ukumbi huu.
Mzee Kiongozi wa ICC, Mh. Mwl. Given Lemway, sambamba na Wazeee wa Kanisa Mama Eva Makombe, Mama Imelda Makombe na Mzee Silus Msola; wakiwa katika Ibada ya mwishoo, mwishoo kabisa, Ibada ya Kusifu na kuabudu katika Ukumbi wa Sabasaba.
Waamini wa ICC wakiwa katika Ibada ya mwisho, mwisho kabisaa; Ibada ya Kusifu na kuabudu katika Ukumbi wa Sabasaba.
Mchungaji Kiongozi wa ICC, Mch. Raphael Kitine akitoa Nasaha zake kwa mara ya mwisho, mwisho kabisaaa katika Madhabahu ya ICC Sabasaba. Baada ya hapo akaongoza msafara kuelekea makao mapya.. ICC Lugalo
Waamini wa ICC wakiongozwa na Mch. Raphael Kitine, mdogo mdogo toka Sabasaba hadi Lugalo...
Sifa na Utukufu kwa Mungu aliyewezesha mchakato woote kukamilika.
Hatimaye ni mwishoo, mwisho kabisaaaa kuabudia Sabasaba..
No comments:
Post a Comment