Shalom!
Ushirika wa Wanaume wa Kikristo (CMF) ICC, baada ya kuwa na ziara kadhaa za kutembelea Wanaushirika (Wanaume) wa ICC; sasa imeandaa mtoko maalumu siku ya Jumamosi 08/08/2015.
Ziara ya Ushirika wa Wanaume wa Kikristo (CMF) ICC Lugalo, Nyumbani kwa Mzee Kiongozi wa Kanisa; Mh. Mwl. Given Lemway, ambaye alifiwa na Mama yake Mzazi.
Ziara ya Ushirika wa Wanaume wa Kikristo (CMF) ICC Lugalo, Nyumbani kwa Mchungaji Mwanafunzi; Mch. Omega Kipemba, ambaye alifiwa na Baba yake Mzazi.
Ziara ya Ushirika wa Wanaume wa Kikristo (CMF) ICC Lugalo, Nyumbani kwa Ndg. Eliud Tati ambaye amefunga ndoa hivi karibuni
Baada ya ziara hizo, Ushirika wa Wanaume wa kikristo ICC tumepanga kuwa na Tukio Maalumu kwa Wanaume wote. Tumepanga kuwa na muda mzuri wa kubadilishana mawazo, kuburudika with Nyamachoma na vinywaji.
Mwenyekiti na Katibu wa CMF ICC pamoja na mwana CMF walipotembelea eneo la tukio kabla ya siku ya Tukio
Mtoko huu utafanyika siku ya Jumamosi (08/08/2015) eneo la Igingilanyi kwa mchango mdogo tu wa Tsh. 10,000/-. Safari itaanzia Kanisani ICC Lugalo saa Sita kamili Mchana.
Matukio Makuu:
> Neno la Mungu
> Kuongea (Kubadilishana mawazo)
> Kula na Kunywa
> Mengineyo
Pamoja Tunaweza: Thibitisha ushiriki wako kwa namba zifuatazo
0755930595/0788992963/0767362042. Tafadhali usipange kukosa, Mjulishe na mwenzako.
Mungu Akubariki.
Zifuatazo ni picha za Wajumbe waliotembelea eneo litapofanyika tukio au mtoko huu.
USIPANGE KUKOSAA!!
No comments:
Post a Comment