CMF ni kifupisho cha maneno ya kiingereza Christian Men's Fellowship, kwa kiswahili ni Ushirika wa Wanaume wa Kikristo, Ushirika huu ni Idara ya Wanaume wa Kanisa la T.A.G kama zilivyo Idara zingine, mfano Wanawake (WWK) na Vijana (CA's).
Neno Kuu la Ushirika wa Wanaume (CMF) linatoka katika Kitabu cha Habakuki 3:2; na Dua ya Ushirika ni "..Ee Bwana Fufua kazi yako katikati ya miaka.."
Ushirika wa CMF ulianzishwa kwa nia ya kutimiza makusudi matano ya Kanisa la T.A.G ambayo ni:
1. Kuabudu;
2. Ushirika;
3. Kujengana;
4. Utumishi;
5. Uinjilisti.
CMF ICC haipo nyuma katika kutimiza makusudi hayo, ni mengi ambayo CMF ICC tumefanya. Jumamosi wiki hii 08/08/2015 Wana CMF ICC tuliamua kuwa na mtoko Maalumu wa kwenda kutafuna mbuzi na mengineyo. Tulkwenda sehemu tuliiivu mbali na Kanisa kwetu ICC Lugalo ili kwenda kudumisha Ushirika wetu. Tulitafuna nyama ya mbuzi na kunywa soda, juice na maji. Tukajadiliana mengi yanayotuhusu Wanaume, ya kiroho na ya kimwili pia. Naamini muda si mrefu, CMF ICC Lugalo, itakuwa mfano mzuri wa kuigwa, kwa Kanisa, Mkoa, na Taifa letu. It's just matter of time; God is with us, who can be against us!!???
Mungu Awabariki wote mlioshiriki na kufanikisha mtoko huu. Zifuatazo ni baadhi ya picha za mtoko huo.
No comments:
Post a Comment