Sunday, 15 June 2014

IBADA YA LEO ICC

Ibada ya leo ICC ilikuwa nzuri na ya kipekee sana. Timu ya kusifu na kuabudu ikiongozwa na Mrs. Adder Mkea. ilituongoza vyema katika kumsifu na kumwabudu Mungu katika Roho na Kweli.

Keyboard ilisimamiwa na Mwl. Nuhu, gitaa la base lilikamatwa na Bwana mdogo Amani.

Upande wa IT alisimama Sir ECHA, kwa kushirikiana na Bwana mdogo James;

Kwaya ya PATMO ilifanya mambo yake, ikiongozwa na Mrs. Kimbavala

 Kwa kila aliyefungua moyo wake alipokea jibu toka kwa Mungu;

Madhabahu ilisimamiwa na Borther Brian, aisee huyu Bwana ni moto wa kuotea mbali, waliokuwepo leo Ibadani walishuhudia wenyewe kwa macho na masikio yao!! Ujumbe kamili utawajia hapahapa usitoke usiondoke!

ICC YAADHIMISHA JUBILEE YA MIAKA 75 YA T.A.G, NA MIAKA 13 YA ICC

Maadhimisho ya miaka 75 ya Kanisa la T.A.G yalifanyika Siku ya Jumapili (8/06/2014) katika Kanisa la I.C.C. Ibada ilianza kama kawaida, ambapo Ibada ya kusifu na Kuabudu ilisimamiwa na Timu ya kusifu na kuabudu ya Kanisa.


Keyboard ilisimamiwa na Mtumishi wa Bwana, Mr. Andrew Magelanga; Gitaa la base alikamata Mwl. Nuhu, upande wa IT alikuwepo Bwana Mdogo James akiratibu michakato yote kuhakikisha mambo yanakwenda sawa.


 Timu ya kusifu na kuabudu ilitimiza wajibu wake ipasavyo katika kuliongoza Kanisa zima kwenye kusifu na kuabudu;


Baada ya kukamilisha taratibu za awali za Ibada, Waamini wote tulitoka nje kwa ajili ya maandamano yaliyoongozwa na Mchungaji Kiongozi wa ICC Mch. Raphael Kitine.

Maandamano hayo yalipokewa na Mgeni Rasmi wa Siku hiyo Mch. Chavala ambaye ni Katibu wa Sehemu ya Iringa.

Baada ya kupokelewa na Mgeni Rasmi, moja kwa moja tukaingia Kanisani kwaajili ya kuanza Ibada ya Maalum ya Maadhimisho ya Jubilee ya miaka 75 ya Kanisa la T.A.G, pia maadhimisho ya miaka 13 ya Kanisa la ICC. Mchungaji Kiongozi wa ICC alizungumza maneno ya utangulizi wa shughuli hii.

Shamra shamra zilikuwepo za kutosha, ambapo Kwaya ya PATMO waliimba wimbo mkali sana wa Jubilee;

Wimbo wa PATMO wa Jubilee uliibua shangwe kubwa ambapo Kanisa lote likiongozwa na Mchungaji Kitine na Mama Mchungaji Kitine walijumuika kucheza na Kwaya ya PATMO;


Tukio la kuvutia lilikuwa ni la keki, ambapo Mchungaji Kiongozi Mch. Raphael Kitine, Mgeni Rasmi Mch. Chavala pamoja na Mama Mchungaji Mrs. Roswita Kitine waliongoza  katika zoezi la kukata keki.

Alianza Mch. Raphael Kitine kumlisha keki Mama Mchungaji, Mrs Roswita Kitine; kisha akamlisha mgeni Rasmi Mch. Chavala. Baada ya hapo Mgeni Rasmi Mch. Chavala akaanza kuwalisha Viongozi mbalimbali wa Kanisa kwa niaba ya Waumini wote wa T.A.G ICC
 Mch. Raphael Kitine akimlisha keki Mama Mchungaji Mrs. Roswita Kitine

Mch. Kitine akimlisha keki Mgeni Rasmi Mch. Chavala

Mgeni Rami Mch. Chavala akimlisha keki Mch. Kitine

Mgeni Rami Mch. Chavala akimlisha keki Mzee Kiongozi wa ICC Mh. Mwl. Given Lemway.

Mgeni Rami Mch. Chavala akimlisha keki Katibu wa Kanisa Mwinjilisti Oscar Mwanjala

Mgeni Rami Mch. Chavala akimlisha keki Mzee wa Kanisa Mama Eva Makombe

Mgeni Rami Mch. Chavala akimlisha keki Mzee wa Kanisa Mwl. Ezekiel Fungo

Mzee wa Kanisa Mama Mgeni akisikilizia utamu wa keki

Mc Maarufu Irina na Mtangazaji wa Kituo cha Redio Nuru FM Mr. Gerald Enock Malekela naye alipata utamu wa keki

Sunday, 8 June 2014

MAADHIMISHO YA JUBILEE YA MIAKA 75 YA T.A.G HAPA ICC YAPENDEZA SANA

Kanisa la ICC leo limefanya hitimisho la maadhimisho ya Wiki ya Jubilee ya Miaka 75 ya T.A.G, pia miaka 13 tangu kuanzishwa kwa Kanisa hili. Maadhimisho haya yamefana kupita maelezo.

Ibada ilikuwa njema, angalia matukio katika picha, taarifa kamili itawajia hapahapa!









Stay tuned kwa taarifa kamili.