Maadhimisho ya miaka 75 ya Kanisa la T.A.G yalifanyika Siku ya Jumapili (8/06/2014) katika Kanisa la I.C.C. Ibada ilianza kama kawaida, ambapo Ibada ya kusifu na Kuabudu ilisimamiwa na Timu ya kusifu na kuabudu ya Kanisa.
Keyboard ilisimamiwa na Mtumishi wa Bwana, Mr. Andrew Magelanga; Gitaa la base alikamata Mwl. Nuhu, upande wa IT alikuwepo Bwana Mdogo James akiratibu michakato yote kuhakikisha mambo yanakwenda sawa.
Timu ya kusifu na kuabudu ilitimiza wajibu wake ipasavyo katika kuliongoza Kanisa zima kwenye kusifu na kuabudu;
Baada ya kukamilisha taratibu za awali za Ibada, Waamini wote tulitoka nje kwa ajili ya maandamano yaliyoongozwa na Mchungaji Kiongozi wa ICC Mch. Raphael Kitine.
Maandamano hayo yalipokewa na Mgeni Rasmi wa Siku hiyo Mch. Chavala ambaye ni Katibu wa Sehemu ya Iringa.
Baada ya kupokelewa na Mgeni Rasmi, moja kwa moja tukaingia Kanisani kwaajili ya kuanza Ibada ya Maalum ya Maadhimisho ya Jubilee ya miaka 75 ya Kanisa la T.A.G, pia maadhimisho ya miaka 13 ya Kanisa la ICC. Mchungaji Kiongozi wa ICC alizungumza maneno ya utangulizi wa shughuli hii.
Shamra shamra zilikuwepo za kutosha, ambapo Kwaya ya PATMO waliimba wimbo mkali sana wa Jubilee;
Wimbo wa PATMO wa Jubilee uliibua shangwe kubwa ambapo Kanisa lote likiongozwa na Mchungaji Kitine na Mama Mchungaji Kitine walijumuika kucheza na Kwaya ya PATMO;
Tukio la kuvutia lilikuwa ni la keki, ambapo Mchungaji Kiongozi Mch. Raphael Kitine, Mgeni Rasmi Mch. Chavala pamoja na Mama Mchungaji Mrs. Roswita Kitine waliongoza katika zoezi la kukata keki.
Alianza Mch. Raphael Kitine kumlisha keki Mama Mchungaji, Mrs Roswita Kitine; kisha akamlisha mgeni Rasmi Mch. Chavala. Baada ya hapo Mgeni Rasmi Mch. Chavala akaanza kuwalisha Viongozi mbalimbali wa Kanisa kwa niaba ya Waumini wote wa T.A.G ICC
Mch. Raphael Kitine akimlisha keki Mama Mchungaji Mrs. Roswita Kitine
Mch. Kitine akimlisha keki Mgeni Rasmi Mch. Chavala
Mgeni Rami Mch. Chavala akimlisha keki Mch. Kitine
Mgeni Rami Mch. Chavala akimlisha keki Mzee Kiongozi wa ICC Mh. Mwl. Given Lemway.
Mgeni Rami Mch. Chavala akimlisha keki Katibu wa Kanisa Mwinjilisti Oscar Mwanjala
Mgeni Rami Mch. Chavala akimlisha keki Mzee wa Kanisa Mama Eva Makombe
Mgeni Rami Mch. Chavala akimlisha keki Mzee wa Kanisa Mwl. Ezekiel Fungo
Mzee wa Kanisa Mama Mgeni akisikilizia utamu wa keki
Mc Maarufu Irina na Mtangazaji wa Kituo cha Redio Nuru FM Mr. Gerald Enock Malekela naye alipata utamu wa keki
No comments:
Post a Comment