Na. Mch. Raphael Kitine (Mchungaji Kiongozi ICC).
Andiko Kuu: Matendo 1:8
Mch. Raphael Kitine (Mchungaji Kiongozi ICC) akiwa Madhabahuni ICC
I. UTANGULIZI:
i. Maana ya Neno Nguvu.
> Ni uwezo wa kufanya kitu;
> Uwezo, nguvu ya kufanya kitu.
ii. Nguvu ya Roho Mtakatifu.
> Nguvu ya Roho Mtakatifu ni Nguvu ya Mungu.
> Ni Udhihirisho wa Roho Mtakatifu katika maisha ya Mwamini kuwa na uwezo wa kufanya yale yasiyotarajiwa.
II. UDHIHIRISHO WA NGUVU YA ROHO MTAKATIFU.
> Katika Agano la Kale Roho Mtakatifu hakuweka makazi ya kudumu kwa Watu wa Mungu, japokuwa alitembea katikati yao na aliwapa Nguvu za kuweza kupata vitu vile walivyoshindwa kuvipata kwa juhudi zao binafsi.
> Nguvu yake ilionekana katika Uumbaji, kwa Nguvu zake Ulimwengu uliumbwa. Mwanzo 1:1-2; Ayubu 26:13.
> Roho Mtakatifu pia aliwapa Nguvu Watu katika Agano la Kale ili waweze kutenda kusudi na mapenzi ya Mungu. 1 Samweli 16:13; Kutoka 31:2-5; Hesabu 27:18.
> Uweza wa Nguvu za Samsoni ulimjia moja kwa moja toka kwa Roho Mtakatifu aliyekuwa juu yake. Waamuzi 14:6, 19; 15:14.
Waamini wa ICC wakifuatilia mafundisho kwa umakini.
III. UMUHIMU WA KUPOKEA NGUVU ZA ROHO MTAKATIFU.
i. Nguvu ya kufanyika Wana wa Mungu. Warumi 8:14.
> Pasipo Nguvu ya Mungu ndani yetu, kamwe hatutokuwa Wana (Watoto) Wake.
> Mwanadamu alishapoteza kusudi la njia yake na hamtambui Baba wa Kweli, Roho Mtakatifu huamsha mahitaji yetu ya kiroho na kutuelekeza kwa Yesu.
ii. Nguvu ya kuishi maisha ya Imani. Waebrania 11:6.
> Tunazo Nguvu za Roho Mtakatifu kwenye maisha yetu ya siku zote. Efeso 3:16-17.
> Mungu anatutaka tupokee Nguvu zake na tuendelee kuishi maisha ya imani na tuwe mfano kwa wengine.
iii. Nguvu za kuushinda uovu.
> Kila Mwamini yupo kwenye ukanda wa mapambano.
> Nguvu za Mungu zapatikana ndani yetu ili tuweze kumtambua na kumpiga shetani. 1 Yohana 4:4.
iv. Nguvu ya kushirikisha Neno la Mungu.
> Nguvu za Roho Mtakatifu zatuwezesha kujiamini na kuwashuhudia wengine juu ya habari za Yesu Kristo. Mdo 4:13.
> Pasipo Nguvu za Roho Mtakatifu mtu huwa mwoga kushuhudia habari za Yesu. Mathayo 26:69-70.
IV. NAMNA YA KUPOKEA NGUVU ZA ROHO MTAKATIFU.
> Tunapokea Nguvu za Roho Mtakatifu kwa njia ya Ubatizo wa Roho Mtakatifu.
i. Vigezo vya kubatizwa na Roho Mtakatifu.
> Lazima uwe umeokoka. Yohana 5:32.
> Lazima uwe na shauku ya kujazwa na Roho Mtakatifu. Mathayo 5:6; Warumi 15:16; 1 Wakorintho 6:11; 7:37.
> Lazima kujitoa kikamilifu kwa Mungu. Matendo 5:32.
ii. Hatua za Ubatizo wa Roho Mtakatifu.
> Kikaribie kiti cha Neema kwa Ujasiri. Waebrania 4:16.
> Mwombe Mungu akujaze Roho wake. Luka 11:10-13.
> Msifu Mungu kwa Imani. Luka 24:53.
V. HITIMISHO - FUNGUO MUHIMU ZA UBATIZO WA ROHO MTAKATIFU.
i. Kiu.
ii. Imani. Waebrania 11:16; Marko 11:24.
iii. Sifa. Matendo 4:21.
iv. Unyenyekevu. Warumi 6:13; 12:1.
Waamini wa ICC wakiwa katika Ibada ya kusifu na kuabudu.
Random Posts
Wednesday, 22 October 2014
Monday, 13 October 2014
HOW TO FINISH THE YEAR SUCCESSFULLY
By Rev. Raphael Kitine (Senior Pastor ICC).
Pilot Verse: 2 Tim 4:7-8.Rev. Raphael Kitine (LHS) alongside his translator Mr. Edom Fungo (RHS).
A. INTRODUCTION. 1Kor 9:24-27
i) Why should we learn this?
> To help us conclude the year on high spiritually and physically.
> To help us lay out the foundation for the subsequent year’s goals.
ii) Truth about concluding the year successfully
> To succeed in the year 2015 will depend on the heights of achievements reached in the year 2014.
> Excellent conclusion of the year is a launching step for the subsequent year.
> The measure of a person achievement is determined at the end of the journey.
B. IMPORTANT THINGS TO HELP US CONCLUDE THE YEAR SUCCESSFULLY. Philippians 3:14.
> According to Apostle Paul, the life of faith for a believer is equivalent to a race tournament in which a competitor is aiming to finish on high position as the first at the end of the competition.
i) Focus on your game. Nehemiah 4:1-6.
> Don't compare yourself with others.
> Stay positive.
> Don't pay any attention to the critics.
ii) Consider the time left on the scoreboard. Ephessians 5:16-17.
> Don't waste your time.
> Pace yourself.
iii) Be a Team Player. Proverbs 27:17; 18:1.
> Know your strengths and weaknesses.
> We need each other.
iv) Listen to your Coach. Proverbs 3:5-6.
> Remember you are not the Coach, Your Coach is your God.
> Memorize His game plan through reading the Bible and prayers.
v) Practice amnesia often. Philippians 3:13.
> Don't live in the past.
> Forgive and forget.
vi) Don't be boastfull. Jeremiah 50:32.
> Don't think that you are better than others.
vii) Stay committed. Rev 3:11.
> Be determined, don't give up.
Sunday, 5 October 2014
VIJANA WA ICC TUMEFIKIA KILELE CHA SIKUKUU YETU
Hatimaye Vijana wa ICC tumehitimisha Wiki ya Sikukuu ya Vijana tuliyoizindua rasmi Jumapili ya Wiki iliyopita. Mungu awabariki wote mlioshiriki kuifanikisha Wiki hii ya Sikukuu. Mungu awatimizie haja ya mioyo yenu. Zaburi 20:1-9.
Barikiwa kwa picha za matukio mbalimbali ya leo. Taarifa kamili ya Sikukuu itawajia hapahapa.
Barikiwa kwa picha za matukio mbalimbali ya leo. Taarifa kamili ya Sikukuu itawajia hapahapa.
Friday, 3 October 2014
MKUTANO WA INJILI WAENDELEA
Mkutano wa Injili ulioandaliwa na Idara ya Vijana (CA's) unaendelea katika Viwanja vya Shule ya Msingi Kihesa, katika maadhimisho ya Wiki ya Sikukuu ya Vijana.
Wewe ambaye hujafika unakaribishwa sana, waleteni wagonjwa na wenye shida mbalimbali ili wapokee uponyaji kwa Jina la Yesu. Kesho ndio siku ya mwisho. Watu wote mnakaribishwa, muda ni kuanzia saa kumi kamili jioni.
Wewe ambaye hujafika unakaribishwa sana, waleteni wagonjwa na wenye shida mbalimbali ili wapokee uponyaji kwa Jina la Yesu. Kesho ndio siku ya mwisho. Watu wote mnakaribishwa, muda ni kuanzia saa kumi kamili jioni.
Subscribe to:
Posts (Atom)