Wednesday, 1 October 2014

MKUTANO MKUBWA WA INJILI VIWANJA VYA SHULE YA KIHESA

Idara ya Vijana (CA's) ICC, imeandaa Mkutano mkubwa wa Injili utakaofanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Kihesa. Mkutano utaanza siku ya Alhamisi (02/10/2014) hadi Ijumamosi (04/10/2014) muda wa saa kumi kamili hadi saa kumi na mbili Jioni. Waleteni wagonjwa na watu wenye shida mbalimbali wataombewa kwa Jina Kuu kupita majina yote, Jina la Yesu Kristo. Watu wote mnakaribishwa.

Kutokana na Mkutano huu, hakutakuwa na Ibada Kanisani katika siku hizo, hivyo basi Waamini wote wa ICC tunatakiwa kufika kwenye Mkutano kuungana na Vijana kulitangaza Neno la Mungu. Upatapo taarifa hii mjulishe na mwenzako.
Mungu akubariki.

Tangazo la Mkutano wa Injili uliondaliwa na Idara ya Vijana (CA's) ICC.

 Vijana wa ICC (Sabasaba) wakiwa kwenye mazoezi ya uimbaji na maombi kujiandaa na Mkutano mkubwa wa Injili.

 Kauli Mbiu ya Vijana. ".....Tutavuna mpaka kieleweke..", Kwakuwa tu Wajumbe wa Kristo (2 Kor 5:20), Vijana tupo tayari kutimiza Agizo kuu la Bwana Yesu (Mathayo 28:18 - 20).

No comments:

Post a Comment