Na. Mch. Raphael Kitine (Mchungaji Kiongozi ICC).
Andiko Kuu: Matendo 1:8
Mch. Raphael Kitine (Mchungaji Kiongozi ICC) akiwa Madhabahuni ICC
I. UTANGULIZI:
i. Maana ya Neno Nguvu.
> Ni uwezo wa kufanya kitu;
> Uwezo, nguvu ya kufanya kitu.
ii. Nguvu ya Roho Mtakatifu.
> Nguvu ya Roho Mtakatifu ni Nguvu ya Mungu.
> Ni Udhihirisho wa Roho Mtakatifu katika maisha ya Mwamini kuwa na uwezo wa kufanya yale yasiyotarajiwa.
II. UDHIHIRISHO WA NGUVU YA ROHO MTAKATIFU.
> Katika Agano la Kale Roho Mtakatifu hakuweka makazi ya kudumu kwa Watu wa Mungu, japokuwa alitembea katikati yao na aliwapa Nguvu za kuweza kupata vitu vile walivyoshindwa kuvipata kwa juhudi zao binafsi.
> Nguvu yake ilionekana katika Uumbaji, kwa Nguvu zake Ulimwengu uliumbwa. Mwanzo 1:1-2; Ayubu 26:13.
> Roho Mtakatifu pia aliwapa Nguvu Watu katika Agano la Kale ili waweze kutenda kusudi na mapenzi ya Mungu. 1 Samweli 16:13; Kutoka 31:2-5; Hesabu 27:18.
> Uweza wa Nguvu za Samsoni ulimjia moja kwa moja toka kwa Roho Mtakatifu aliyekuwa juu yake. Waamuzi 14:6, 19; 15:14.
Waamini wa ICC wakifuatilia mafundisho kwa umakini.
III. UMUHIMU WA KUPOKEA NGUVU ZA ROHO MTAKATIFU.
i. Nguvu ya kufanyika Wana wa Mungu. Warumi 8:14.
> Pasipo Nguvu ya Mungu ndani yetu, kamwe hatutokuwa Wana (Watoto) Wake.
> Mwanadamu alishapoteza kusudi la njia yake na hamtambui Baba wa Kweli, Roho Mtakatifu huamsha mahitaji yetu ya kiroho na kutuelekeza kwa Yesu.
ii. Nguvu ya kuishi maisha ya Imani. Waebrania 11:6.
> Tunazo Nguvu za Roho Mtakatifu kwenye maisha yetu ya siku zote. Efeso 3:16-17.
> Mungu anatutaka tupokee Nguvu zake na tuendelee kuishi maisha ya imani na tuwe mfano kwa wengine.
iii. Nguvu za kuushinda uovu.
> Kila Mwamini yupo kwenye ukanda wa mapambano.
> Nguvu za Mungu zapatikana ndani yetu ili tuweze kumtambua na kumpiga shetani. 1 Yohana 4:4.
iv. Nguvu ya kushirikisha Neno la Mungu.
> Nguvu za Roho Mtakatifu zatuwezesha kujiamini na kuwashuhudia wengine juu ya habari za Yesu Kristo. Mdo 4:13.
> Pasipo Nguvu za Roho Mtakatifu mtu huwa mwoga kushuhudia habari za Yesu. Mathayo 26:69-70.
IV. NAMNA YA KUPOKEA NGUVU ZA ROHO MTAKATIFU.
> Tunapokea Nguvu za Roho Mtakatifu kwa njia ya Ubatizo wa Roho Mtakatifu.
i. Vigezo vya kubatizwa na Roho Mtakatifu.
> Lazima uwe umeokoka. Yohana 5:32.
> Lazima uwe na shauku ya kujazwa na Roho Mtakatifu. Mathayo 5:6; Warumi 15:16; 1 Wakorintho 6:11; 7:37.
> Lazima kujitoa kikamilifu kwa Mungu. Matendo 5:32.
ii. Hatua za Ubatizo wa Roho Mtakatifu.
> Kikaribie kiti cha Neema kwa Ujasiri. Waebrania 4:16.
> Mwombe Mungu akujaze Roho wake. Luka 11:10-13.
> Msifu Mungu kwa Imani. Luka 24:53.
V. HITIMISHO - FUNGUO MUHIMU ZA UBATIZO WA ROHO MTAKATIFU.
i. Kiu.
ii. Imani. Waebrania 11:16; Marko 11:24.
iii. Sifa. Matendo 4:21.
iv. Unyenyekevu. Warumi 6:13; 12:1.
Waamini wa ICC wakiwa katika Ibada ya kusifu na kuabudu.
No comments:
Post a Comment