Wednesday, 9 December 2015

MKUTANO WA INJILI KIHESA SOKONI

Shalom!

Wapendwa katika Bwana, napenda kutumia fursa hii kuwaalika wakazi wa Iringa katika Mkutano wa Injili unaofanyika Kihesa Sokoni. Mkutano huu umeandaliwa na kuendeshwa kwa ushirikiano wa Kanisa la T.A.G ICC Lugalo na Umoja wa Wa Wanafunzi wa Kikristo wa Chuo Kikuu cha Ndejje kutoka Uganda (Ndejje University Christian Union). Wanafunzi hawa wa Chuo wamekuja kushirikiana nasi ili kuhubiri Injili katika mji wetu wa Iringa. Kwa nyakati za asubuhi watakuwa wakizunguka maeneo mbali mbali kuhubiri, hivyo wenyeji tunaombwa kufika Kanisani kuanzia saa mbili asubuhi ili tuweze kuungana nao.

Mkutano umeanza leo utaendelea hadi mwisho wa Wiki. Tafadhali upatapo ujumbe huu mjulishe na mwenzako.

Mungu Akubariki.

Basi walilotumia Wanachuo toka Uganda hadi Iringa

Zifuatazo ni baadhi ya picha za matukio katika Mkutano siku ya leo.
Hizi ni baadhi tu ya Picha za Matukio katika Mkutano wa Leo. Tafadhali, usikose kila siku jioni saa kuanzia kumi kamili.

Monday, 7 December 2015

ICC SINGLE's DAY 2015 WAS AMAZING

Shalom!

Hakika Mungu ni mwema, hakuna namna ambayo naweza kuelezea kuhusu Siku Maalumu ya Vijana ambao bado hawajaoa au hawajaolewa. Siku hii maalumu (Single's Day) huandaliwa na Kanisa la T.A.G - ICC Lugalo, ambapo Vijana Singles hukutana kwa ajili ya kujadili changamoto mbalimbali za maisha, kimwili, kiroho na kiuchumi.

Mwaka huu Siku hii tulifanyia eneo la Rivervalley Campsite, siku ya Jumamosi Tarehe 05/12/2015.
 Baadhi ya Vijana wakipata picha ya kumbukumbu njiapanda kuelekea Campsite

Pamoja na kujadiliana kama Vijana, pia huwa kuna mwezeshaji kwaajili ya kujibu baadhi ya hoja toka kwa vijana. Mwaka huu tulikuwa na Mchungaji Kiongozi wa ICC Lugalo, Mch. Raphael Kitine. Ninaamini, hakuna kijana aliyeshiriki ambaye anajutia kushiriki siku hiyo. Hakika ilikuwa ya kupendeza, tulifaidika kimwili na kiroho kwa kweli; tulikula, tulikunywa tulifurahia aisee.

Nawaalika tena kwa wale wataokuwa Single mwakani basi msikose kushiriki siku hii ya kipekee. Mungu Awabariki.

Zifuatazo ni baadhi tu ya picha za mambo yalivyokuwa.
                                                          Safari ilianzia hapa.. ICC Lugalo

    Tukafika hapaa.. njiapanda ya Campsite, tukaweka pouz kwa ajili ya kupata kumbukumbu

Baada ya hapo tukaelekea eneo la tukio kuendelea na safari, tulipowasiliana, tukafungua kwa maombi kisha michakato ikaendelea...
Mchungaji Kiongozi wa ICC Lugalo, MCh. Raphael Kitine, akitoa muongozo wa Single's Day 2015

Baada ya kupata muongozo, tukaunda makundi matatu na kuanza majadiliano rasmi.
                                                   Kundi la kwanza, wakiwa katika majadiliano

                                                     Kundi la pili nalo likiendelea kujadili mada motomoto

                                                Kundi la tatu nalo halikuwa nyuma kujadili

Baada ya majadiliano kwa makundi yote matatu, tukapata muda wa mapumziko kisha tukapata mthothii
                                               Mazingira ya kukandamiza menu yakiwekwa sawa

Baada yapo tumbo likapata haki yake
   Wadau wa Single's Day 2016 wakipata chakula cha mwili, vyuku, vyoda, pilau n.k vilihusika sana

Baada ya mthoth uwasilishaji wa mada ukaanza kwa kila kundi kuteua mwakilishi wa kuwasilisha kwa niaba ya kundi.
Vijana wakiwasilisha mada pamoja na kuuliza maswali, Mch. Raphael Kitine alikuwepo kuweka mambo sawa hasa kwa changamoto tata zilizoonekana kutatiza vijana.

Baada ya kipindi Vijana ikawa mwisho wa siku, zikafuata selfie za ukweli..
Mungu Awabariki sana Vijana wote mlioshiriki ICC Single's Day 2015, kwa ambao hamkufanikiwa mwaka huu tafadhali msikose mwakani, kwakuwa kukamilika kwa hii ndio mwanzo wa ICC Single's Day 2016.