Wednesday, 9 December 2015

MKUTANO WA INJILI KIHESA SOKONI

Shalom!

Wapendwa katika Bwana, napenda kutumia fursa hii kuwaalika wakazi wa Iringa katika Mkutano wa Injili unaofanyika Kihesa Sokoni. Mkutano huu umeandaliwa na kuendeshwa kwa ushirikiano wa Kanisa la T.A.G ICC Lugalo na Umoja wa Wa Wanafunzi wa Kikristo wa Chuo Kikuu cha Ndejje kutoka Uganda (Ndejje University Christian Union). Wanafunzi hawa wa Chuo wamekuja kushirikiana nasi ili kuhubiri Injili katika mji wetu wa Iringa. Kwa nyakati za asubuhi watakuwa wakizunguka maeneo mbali mbali kuhubiri, hivyo wenyeji tunaombwa kufika Kanisani kuanzia saa mbili asubuhi ili tuweze kuungana nao.

Mkutano umeanza leo utaendelea hadi mwisho wa Wiki. Tafadhali upatapo ujumbe huu mjulishe na mwenzako.

Mungu Akubariki.

Basi walilotumia Wanachuo toka Uganda hadi Iringa

Zifuatazo ni baadhi ya picha za matukio katika Mkutano siku ya leo.
Hizi ni baadhi tu ya Picha za Matukio katika Mkutano wa Leo. Tafadhali, usikose kila siku jioni saa kuanzia kumi kamili.

No comments:

Post a Comment