Hakika Mungu ni mwema, hakuna namna ambayo naweza kuelezea kuhusu Siku Maalumu ya Vijana ambao bado hawajaoa au hawajaolewa. Siku hii maalumu (Single's Day) huandaliwa na Kanisa la T.A.G - ICC Lugalo, ambapo Vijana Singles hukutana kwa ajili ya kujadili changamoto mbalimbali za maisha, kimwili, kiroho na kiuchumi.
Mwaka huu Siku hii tulifanyia eneo la Rivervalley Campsite, siku ya Jumamosi Tarehe 05/12/2015.
Baadhi ya Vijana wakipata picha ya kumbukumbu njiapanda kuelekea Campsite
Pamoja na kujadiliana kama Vijana, pia huwa kuna mwezeshaji kwaajili ya kujibu baadhi ya hoja toka kwa vijana. Mwaka huu tulikuwa na Mchungaji Kiongozi wa ICC Lugalo, Mch. Raphael Kitine. Ninaamini, hakuna kijana aliyeshiriki ambaye anajutia kushiriki siku hiyo. Hakika ilikuwa ya kupendeza, tulifaidika kimwili na kiroho kwa kweli; tulikula, tulikunywa tulifurahia aisee.
Nawaalika tena kwa wale wataokuwa Single mwakani basi msikose kushiriki siku hii ya kipekee. Mungu Awabariki.
Zifuatazo ni baadhi tu ya picha za mambo yalivyokuwa.
Safari ilianzia hapa.. ICC Lugalo
Tukafika hapaa.. njiapanda ya Campsite, tukaweka pouz kwa ajili ya kupata kumbukumbu
Baada ya hapo tukaelekea eneo la tukio kuendelea na safari, tulipowasiliana, tukafungua kwa maombi kisha michakato ikaendelea...
Mchungaji Kiongozi wa ICC Lugalo, MCh. Raphael Kitine, akitoa muongozo wa Single's Day 2015
Baada ya kupata muongozo, tukaunda makundi matatu na kuanza majadiliano rasmi.
Kundi la kwanza, wakiwa katika majadiliano
Kundi la pili nalo likiendelea kujadili mada motomoto
Kundi la tatu nalo halikuwa nyuma kujadili
Baada ya majadiliano kwa makundi yote matatu, tukapata muda wa mapumziko kisha tukapata mthothii
Mazingira ya kukandamiza menu yakiwekwa sawa
Baada yapo tumbo likapata haki yake
Wadau wa Single's Day 2016 wakipata chakula cha mwili, vyuku, vyoda, pilau n.k vilihusika sana
Baada ya mthoth uwasilishaji wa mada ukaanza kwa kila kundi kuteua mwakilishi wa kuwasilisha kwa niaba ya kundi.
Baada ya kipindi Vijana ikawa mwisho wa siku, zikafuata selfie za ukweli..
No comments:
Post a Comment