SHALOOM!
[ZABURI 33:1-3; 35:18; 86:12; 147:1; 150:1-6]
ZABURI 147:1
Haleluya. Msifuni Bwana; Maana ni vema kumwimbia Mungu wetu, Maana kwapendeza, kusifu ni kuzuri.
ZABURI 86:12
Nitakusifu Wewe, Bwana, Mungu wangu, Kwa moyo wangu wote, Nitalitukuza jina lako milele.
ZABURI 33:1
1 Mpigieni Bwana vigelegele, enyi wenye haki, Kusifu kunawapasa wanyofu wa moyo.
Uongozi wa Timu ya Kusifu na Kuabudu ICC, kwa niaba ya Uongozi wa Kanisa ICC Lugalo, unakualika ndugu, jamaa na marafiki katika Ibada Maalumu ya Kusifu na Kuabudu katika mwezi huu wa mwisho wa mwaka 2015. Itakuwa ni Ibada ya Kipekee sana na ya Kitofauti sana. Hakika, Hutajutia kushiriki katika Ibada hii. Ibada hii itafanyika itafanyika Siku ya Jumapili 13/12/2015 katika Ibada zote za ICC.
Karibu sana mpendwa, Tafadhali mjulishe na mwenzako.
Mpendwa, kuna siri kubwa sana katika kusifu:
2Nyakati 20:22; Yoshua 6:15-21.
TARATIBU ZA IBADA ZA JUMAPILI ICC LUGALO:
01:00 - 01:30 Asubuhi Maombi na Maombezi;
01:30 - 03:30 Asubuhi Ibada ya Kwanza (English);
03:30 - 04:30 Asubuhi Shule ya Jumapili naUanafunzi;
04:30 - 07:00 Mchana Ibada ya Pili (Kiswahili);
09:30 - 11:00 Jioni Ibada ya Watoto.
11: 00 - 12: 00 Jioni Ibada ya Wanaume (CMF)
Zifuatazo ni baadhi ya picha za Ibada ya Kusifu na Kuabudu ICC Lugalo
No comments:
Post a Comment