Wednesday, 22 April 2015

KUWA WAKILI MWAMINIFU WA MALI ZA MUNGU

Na. Mch. Ruth Kyando.
Mch. Ruth Kyando akihudumu katika madhabahu ya ICC wakati wa Ibada ya Pili (Ibada ya Kiswahili).

Kabla ya Mahubiri, kwa kawaida ICC hutangulia Ibada ya Nguvu ya Kusifu na Kuabudu ambayo huongozwa na Timu ya Kusifu na Kuabudu ya ICC. Ibada ya Kusifu na kuabudu ilikuwa njema sana iliyojaa uwepo wa Nguvu za Mungu. Zifuatazo ni baadhi ya picha wakati wa Ibada hii.
Timu ya Ufundi na mbiundo mbinu wakihakikisha mambo yanakwenda sawa.

Waamini wa ICC wakibubujika wakati wa Ibada ya Kusifu na Kuabudu, Ibada ya Pili.

Baada ya Kusifu na kuabudu, ukafuatia wasaa wa kusikiliza Neno la Mungu.
Mch. Ruth Kyando akihudumu Ibada ya Pili ICC

SOMO: KUWA WAKILI MWAMINIFU WA MALI ZA MUNGU:
YALIYOMO:
I. MAANA NA AINA ZA MATOLEO.
II. MATOLEO KATIKA KUMCHA MUNGU.
III. MATOLEO YANAGUSAJE MAISHA YA MWAMINI?

UTANGULIZI:
  • Kiini cha somo ni jinsi gani matoleo yanavyoleta mahusiano kati ya Mwamini na Mungu.
  • Jambo hili la uhusiano na Mungu kupitia matoleo ni la muhimu sana kulijua.
  • Mara zote Mungu akitaka kuupima upendo na kujitoa kwa mtu anampima katika suala la matoleo. Kwa mfano: Abrahamu alipimwa katika kumtoa mwanae wa pekee Isaka, kipenzi cha moyo wake na tegemeo lake lote. Mwz 22:1 - 2. Kwa utii wa Abrahamu katika utoaji Bwana alimpa Baraka ya Kristo kuzaliwa katika ukoo wake. Math 1:1 - 17.
  • Utoaji unafungua milango ya baraka za Mungu. Mwz 22:15 - 16.
  • Jinsi matoleo yanavyohusiana na maisha ya rohoni. Mdo 10:1 - 4. Tunamuona Kornelio na familia yake.
MAANA YA UWAKILI/BALOZI:
  • Wakili ni mtu aliyepewa dhamana ya usimamizi wa jambo fulani na mtu mwingine, kwa lengo la kusimamia kwa weledi kwa kadri ya thamani ya kile kitu alichopewa.
I. MAANA NA AINA ZA MATOLEO.
  •  Matoleo ni kitu kinachotolewa kwa hiari, lakini pia ni sehemu ya ibada.
i) Dhabihu za kuteketeza.
> Kutoa kitu cha thamani.
> Hizi zilikuwa sadaka za wanyama ambao waliuwawa na kutoa maisha yao (damu zao - uhai wao).
> Dhabihu iliteketezwa kwa moto (Lawi 6:8 - 13) na  damu ya mnyama iliifunika dhambi ya mtoa dhabihu ili awe na uhusiano na Mungu na kuruhusiwa amwabudu.
> Kuteketezwa kwa moto mwili wote wa mnyama ilikuwa ni ishara ya mtoa sadaka kutoa maisha yake yote kikamilifu kwa Mungu katika utakatifu na kutengwa na dhambi.

ii) Dhabihu ya dhambi.
> Dhambi zilizotendwa sio kwa kusudi ila katika ujinga zilihitaji matoleo ya dhabihu ya dhambi. Lawi 4:1 - 35; 6:24 - 30.

iii) Dhabihu ya hatia.
> Lawi 5:14 - 19; 6:7. Dhambi za kushindwa kumuheshimu Mungu katika matoleo au mambo matakatifu aliyo agiza Bwana.
> Dhabihu hizi zilikoma baada ya Yesu kuja (Ebr 9:1 - 12); njia ya kuingia patakatifu ilikuwa bado haijadhihirishwa kama ilivyo sasa.
> Yeye alifanywa upatanisho badala ya wanyama. Rum 3:23 - 25.
> Sadaka nyingine ilikoma ni ya mzaliwa wa kwanza. Kut 13:2.
> Baadae aliwatoa Walawi wafanye ukuhani badala ya wazaliwa wa kwanza. Hes 3:11 - 13, 44 - 51.
> Yesu alipelekwa hekaluni kuwekwa wakfu mbele za Mungu. Lk 2:22 - 24; lakini Wazazi wake hawakutoa sadaka kumkomboa mzaliwa wa kwanza.
> Luka alitaja sadaka ya kutakasikakutoka unajisi wa uzazi kwa sheria ya agano la kale sheria ya Musa. Lawi 12:1 - 8.
> Yesu ni mzaliwa wa kwanza na wote aliowanunua. Uf 5:9 - 10.
> Ebr 12:23, Mkutano mkuu na Kanisa la wazaliwa wa kwanza walioandikwa mbinguni.

II. MATOLEO KATIKA KUMCHA MUNGU
a) Kutoa ni ibada. Zab 50:23.
b) Kutoa ni kumcha Mungu. Ay 1:5.
c) Kutoa ni kutambua kuwa vitu vyote ni mali ya Mungu. Zab 24:1.

iv) Dhabihu ya amani na ushirika.
> Hii ilikuwa sadaka ya hiari, na zinandelea hata sasa. 1 Kor 9:13 - 14.
> Lengo kuu ilikuwa ni dhabihu ya chakula. Lawi 3:1 - 17; 22:21 - 25.

> Kulikuwa na aina tatu za dhabihu ya amani.
  1. Dhabihu ya shukrani au ya sifa na kuabudu: Hii ilitolewa ili kumshukuru Mungu kwa Baraka mtu alizobarikiwa na Mungu au Neema mtu aliyoipata kwa Mungu.
  2. Dhabihu ya upendo kwa Mungu (Lawi 22:23): Iliruhusiwa kutoa kitu chochote kulingana na uwezo wa mtu na Mungu alivyomjalia.
  3. Dhabihu ya malipo ya nadhiri (Lawi 22:21): Hii ilitegemea mtu alikuwa ameweka nadhiri kitu cha namna gani kwa Bwana.
* Zaka ilijitegemea kwa kuwa ilikuwa ni sheria, zaka ni moja ya kumi (1/10) ya mapato ya mazao ya shamba, mifugo na mishahara ambayo inatolewa kwa Mungu. Malaki 3:10 - 12.
* Kutoa fungu la kumi sio tendo la hiari bali ni sheria na agizo la Mungu kibiblia. Kumb 14:22; Lawi 27:30.
* Yesu anasema, zaka na matoleo mengine yasiachwe. Math 23:23.
* Mungu haangalii wingi wa sadaka bali anaangalia moyo ulioridhia na kukubali. Mwz 4:3 - 7.
* Tunatofautiana vipato, kila mtu anainuliwa hatua kwa hatua kulingana na viwango vya mapato yake. Na kila mtu anamtukuza Mungu.
* Mali ulizonazo ni za Mungu, sisi ni mawakili tu tunasimamia badala yake. Zab 24:1.
* Hatuna kitu tulichokuja nacho duniani wala hatutaondoka na kitu. Ay 1:21. 

SPIRITUAL MOMENTUM (Vol 2)

By. Rev. Omega Kipemba
Rev. Omega Kipemba and his Wife (interpreter) Mrs. Sophia Kipemba Preaching the Gospel during the first Service (English Service) at ICC

SALUTATION
Praise the Lord!
Ladies and Gentlemen, brothers and sisters, my friends.

It is once again my pleasure to stand before you, children of the most high God. Congratulation for the wonderful celebration you did in previous Sunday services.

You indeed demonstrated that:
  • Unquestionably Unique;
  • Superbly Special;
  • Gloriously Gifted;
  • Outstandingly Amazing.

SPIRITUAL MOMENTUM Vol 2:
SPIRITUAL DORMANCY

Pilot Verses: Deut 1:6 - 8.

1:6 "The LORD our God said to us at Horeb, "You have stayed long enough at this mountain.
1:7 Break camp and advance into the hill country of the Amorites; go to all the neighboring people in the Arabah, in the mountains,..
1:8 See, I have given you this land. Go in and take possession of the land that the LORD swore he would give to your fathers - to Abraham, Isaac and Jacob - and to their descendants after them."

INTRODUCTION
* MOMENTUM refers to the Quantity of motion of a moving object.
         Momentum = Mass x Velocity

* SPIRITUAL MOMENTUM is a force that increases the rate of spiritual development.

Brethren's, anything in the cosmos whether in motion or in its state of rest faces resistance. Any design either visible or invisible is subjected to resistance.

"The first law of motion states that; every body persists in its state of rest or uniform motion in a straight line unless it is compelled to change that state by force impressed on it"

SPIRITUAL DORMANCY
* The law explicates that, any matter maintain its state of rest unless it is compelled to change that state by forces acted on it. Such inactive state of rest in spiritual issues is called Spiritual Dormancy. In this state, there is neither experiential, movement, progress, increase, way out and nor direction.

"Meditate the Journey of Israelites"

Discus Deut 1: - 8.
Deut 1:6. God said that, "they have stayed long enough at this mountain".
  • Mountain refers to an obstacle, a hindrance, a challenge, a situation of impossibility, difficulties, or problems.
Deut 1:7. God tells them to break camp and advance..
  • They were in a state of stagnation.
  • Stagnation leads to frustration, just as stagnant water is a breeding ground for mosquitoes and germs.
  • It is not the will of God that we remain in the same place or condition all the time.
  • God brings us to the places so that we can learn the lessons of life and move the next level.
  • Nothing great was ever achieved without enthusiasm (passion, zeal).
* One's destiny is determined not by what he/she possesses, but by what possesses him.
* However, it is our responses and attitude which determines how long or how short we stay at a certain place/condition.
* The Israelites had overstayed at mount Horeb because of a wrong attitude (feelings) to the dealings (contact) of God. Deut 1:26 - 31.
 * They stayed at mount Horeb for one year, a place which was not their destination.
 *  The chosen of God, am telling you now, the problems you are facing right now are not a reflection of your destiny or future.
 * It is time to come out and make a progress.

Deut 1:8
"Behold, I have set {set: Heb. given} the land before you; go in and possess the land which the LORD swore unto your fathers, Abraham, Isaac, and Jacob, to give unto them and to their seed after them."

* ... Go and possess..
  • The word possess in Greek is "Yarash", (Yaw-rash) - meaning to occupy by driving out previous tenants, and possessing in their place.
CONCLUSION:
"Any stronghold that keeps you stagnated, is demolished, in Jesus Name!!!"
Rev. Omega Kipemba praying for the congregation at the end of the his preachings.

The following pictures were taken during the Praise and Worship Session.
 Praise & Worship Service, the session which normally takes place at ICC before Preachings.

The Technical Team during the service.

Wednesday, 15 April 2015

WASAA WA KUSIFU NA KUABUDU ICC

Shalom Shalom Shalom!!
 
Zaburi 150:1 - 6 
> Biblia inasema
"1. Haleluya. Msifuni Mungu katika patakatifu pake; Msifunikatika anga la uweza wake.
2. Msifuni kwa matendo yake makuu; Msifuni kwa kadri ya wingi wa ukuu wake.
3. Msifuni kwa mvumo wa baragumu; Msifuni kwa kinanda na kinubi;
4. Msifuni kwa matari na kucheza; msifuni kwa zeze na filimbi;
5. Msifuni kwa matoazi yaliayo; msifuni kwa matoazi yavumayo sana.
6. Kila mwenye pumzi anapaswa kumsifu Bwana."

Karibu sana ICC tumsifu Bwana katika Roho na Kweli.

Zifuatazo ni baadhi ya picha za Ibada ya Jumapili wakati wa Kusifu na Kuabudu.

Barikiwa.