Shalom!
Mungu ni mwema wakati wote. Roho wa Bwana ameendelea kuhudumia watu wake katika Ibada zote mbili za ICC siku ya leo.
Ibada ya kwanza inayoendeshwa kwa lugha ya Kiingereza alihudumu mpakwa mafuta wa Bwana Mch. Omega Kipemba, ambaye kwa sasa yupo likizo anasoma Chuo cha Theolojia kilichopo Nairobi Kenya. Alifundisha Ujumbe wenye kichwa cha habari "PNEUMATOLOGY". He defined Pneumatology as the study of the person and the work of the Holy Spirit. The leading scriptures were from the book of John 14:15-18. He also defined Pneumatology as the theological discipline that focuses only on the Holy Spirit. This discipline is covered all over the Bible from the book of Genesis to the book of Revelation. Other sciptures Mathew 19:28; Titus 3:5; John 3:3; Eph 2:6, more deatails about this subject will be available here later. Stay tuned, Usitoke usiondoke.
Mch. Omega Kipemba akiwa na Mtafsiri wake Mr. Edson Ishengoma wakichimbua madini ya ukweli toka kwenye mgodi wa Roho Mtakatifu.
Ibada ya pili inayoendeshwa kwa lugha ya Taifa alihudumu Mtumishi wa Bwana Mch. Ruth Kyando ambaye naye yupo likizo, anasoma Chuo Cha Biblia Dodoma. Yeye alifundisha Ujumbe wenye kichwa cha habari "ROHO MTAKATIFU", Maandiko: Mwanzo 1:2; Mk 1:10-11; Mt 28:19; Yohana 14:16, 26-27; 16:8-13. Somo kamili utalipata hapahapa. Ndio maana nikasema ni Ibada ya Udhihirisho wa Roho Mtakatifu, kwani Ibada zote mbili Watumishi wa Bwana wamefundisha Jumbe zenye maudhui yanayofana ingawa kila mmoja lifundisha kadri Roho wa Bwana alivyomuwezesha.
Mch. Ruth Kyando akiwa madhabahuni ICC, kidigitali zaidi lakini Roho Mtakatifu anajidhihirisha.
Kama ilivyo kawaida, Ibada ya Sifa hutangulia kabla ya mahubiri. Katika Ibada zote mbili Timu ya Kusifu na Kuabudu ilifanya vyema katika kuliongoza Kanisa kwenye Sifa na Kuabudu.
Timu ya Kusifu na Kuabudu ya ICC ikiwajibika ipasavyo Madhabahuni.
Kwaya ya Kanisa PATMO nao walihudumu katika Madhabahu ya ICC.
Patmo Christian Singers (PCS) ya ICC wakifanya yao Madhabahuni.
Kanisa zima kwa ujumla lilishiriki vyema katika kumsifu na kumuabudu Mungu katika Roho na kweli.
Baada ya Ibada ya Kusifu na Kuabudu, ilifanyika Ibada ya Maombezi iliyoongozwa na Mchungaji Kiongozi wa ICC Mch. Raphael Kitine kwa kushirikiana na Wachungaji waliohudumu Ibada zote za leo na Wazee wa Kanisa.
Upande wa muziki, Mwl. Alpha aliwaongoza vyema vijana wake Amani na James.
Matukio yalichukuliwa na Mr. Gerlad, dawati la IT kama kawaida Mr. Mkea na Sir ECHA waliwajibika ipasavyo
Kumbuka kuanzia Jumatatu (21/07/2014) hadi Jumamosi (26/07/2014) ni Wiki ya Maombi ya Kufunga kwa Kanisa zima. Tutakuwa tunakutana Kanisani kila siku kuanzia saa kumi na nusu jioni.
Karibu sana ICC, Mungu akubariki.
Random Posts
Sunday, 20 July 2014
Sunday, 13 July 2014
KUTOKA MADHABAHUNI ICC: NJIA KUU ZA MAISHA
Mhubiri: Mrs. S. Kipemba
Maandiko:
Mathayo 7:13-14, 16; 3:1-3, 8-10; 2Timotheo 2:15-19; Mathayo 6:33; 22:37-39; Zaburi 122:1-2, 42:1-4
Muhubiri wa Ibada ya leo Mrs. S. Kipemba akihubiri Ujumbe kama unavyo onekana katika screen.
Kama ilivyo ada ICC, kabla ya kipindi cha mahubiri huwa inatangulia Ibada ya kusifu na kuabudu inayosimamiwa na Timu ya kusifu na kuabudu ya ICC. Naipenda Timu hii kwani hakuna mwimbaji anayejiona kuwa ni superstar kuliko wengine. Wote kwa pamoja huimba kwa kushirikiana kadri Roho wa Bwana anavyo waongoza.
Ms. Glory Chanai akiongoza wana Timu wenzake katika kusifu na kuabudu.
Ms. Joyce Senje naye akifanya yake katika madhabahu ya ICC
Ms. Aggy Msigwa naye akiwajibika vyema madhabahuni.
Mr. Petro na Mr. Alpha nao walikuwepo katika Timu ya kusifu na kuabudu
Mchungaji Mwanafunzi (Chuo cha Biblia Nairobi), Mch. Omega Kipemba akiwa ameungana na Timu Madhabahuni.
Ki ukweli siku ya leo ilikuwa ya kipekee sana, upande wa muziki walisimama vyema vijana wadogo sana ambao sikuwafikiria kama wanaweza kuhudumu kwenye Ibada ya Jumapili wakiwa chini ya usimamizi wa Mwalimu wao Mr. Alfa. Waliokuwepo Ibadani leo walishuhudia mambo ya vijana hawa, Mungu awatie Nguvu wasonge mbele. Keyboard alipiga Bwana mdogo James na gitaa la base alipiga mwenzie Amani. Walivitendea haki ipasavyo vyombo hivyo.
Upande wa dawati la IT alikuwepo Sir. ECHA, huku Mr. Gerald akitendea haki Taaluma yake kwa kuchukua matukio ibadani.
Ibada ya kusifu na kuabudu si ya Timu peke yake, bali ni Kanisa zima.
Mtumishi wa Bwana Mr. Joseph Fungo akishiriki ipasavyo katika Ibada ya kusifu na kuabudu.
Baada ya Ibada ya kusifu na kuabudu, mahubiri yalifuatia.
Mrs. S. Kipemba akihubiri siku ya leo.
Katika somo hili alifundisha kuwa katika maisha ya kila mwanadamu, kuna njia kuu mbili ambazo hupita na kila njia ina hatima yake. Njia ya kwanza ni njia pana ambayo hatima yake inaelekea upotevuni, na njia ya pili ni nyembamba ambayo hatima yake inaelekea uzimani. Kila mwanadamu hupita kwenye mojawapo, haiwezekani ukapita katika njia zote mbili au ukawa katikati ya njia hizo.
Alianza kwa kuelezea njia pana kisha akahitimisha kwa kuelezea njia nyembamba. Injili za aina hii zimemisi sana katika Makanisa mengi ya kizazi cha leo, kwani kila unapopita utasikia njoo kwa Yesu upokee muujiza wako. Pokea magari, pokea nyumba, pokea mume au mke n.k. Je, watu wenye vitu hivyo hawatakiwi kuja kwa Yesu!! Tafakari chukua hatua.
Mrs. S. Kipemba akiwa anahubiri katika uwepo wa Roho Mtakatifu Ibadani leo.
Njia pana:
i. Ina nafasi kubwa na inaruhusu watu wengi kupita kwa pamoja na mizigo yao.
ii. Ina ushawishi mkubwa na haina masharti magumu.
iii. Njia hii wanapita wapagani, wenye dini mbalimbali, mataifa mbalimbali; hata baadhi ya waamini waliookoka pia hupiata njia hii.
> Alisisitiza kuwa walokole wanaopita njia hii ni wale waliopoteza mwelekeo wakidhani kuwa mtu anapo okoka ndio kamaliza kila kitu. La hasha! Kuokoka ni mwanzo tu wa safari ndefu san ya Mwamini, changamoto iliyopo ni kuishi maisha matakatifu ya ushindi siku zote.
> Msingi wa maisha yetu ya ulokole ni kuyafanya mapenzi ya Mungu na si vinginevyo. Watu wengi siku za leo wanasimamia zaidi masuala ya miujiza na uponyaji kuliko kuishi maisha ya utakatifu. Matokeo yake ni kuishi maisha ya mazoea na kuishia kupita njia pana inayoelekea upotevuni.
> Pia akasisitiza kuwa miujiza sio kigezo cha mtu kuwa amekubalika na Mungu, uhusiano na Mungu ndio jambo la msingi sana kuliko jambo lolote.
Kuonesha msisitizo ili mlazimu kuacha madhabahu na kuwafuata washirka walipokaa
Njia nyembamba:
i. Njia hii imesonga sana, inaruhusu kupita mtu peke yake bila kuwa na mizigo ya aina yeyote ile.
ii. Ili kupita njia hii, mtu ni lazima afanye maamuzi mazito ya kuuvua utu wa kale.
iii. Njia hii inahitaji mtu kujikana.
> Wokovu ni kusonga mbele wala si kuangalia nyuma.
> Unapoamua kuokoka ni lazima uamue kukabiliana kwa dhati na changamoto mbalimbali unazokutana nazo njiani.
> Biblia inasema kuwa kila alitajaye Jina la Bwana na auache uovu.
iv. Unapoamua kupita Njia hii, ni lazima Yesu awe kipaumbele katika maisha yako.
> Siku za leo watu wengi wamekuwa na vipaumbele vingine badala ya Yesu.
> Kwa mfano msimu huu ni wa kombe la Dunia, watu wengi wameweka mashindano hayo kuwa kipaumbele kuliko Yesu. Imefika wakati watu wanashindwa kukesha makanisani lakini wapo tayari kukesha kuangalia kombe la Dunia.
Mwisho Ibada iliahirishwa kwa maombi yaliyoongozwa na Mtumishi wa Bwana Mch. Omega Kipemba.
Mch. Omega Kipemba (Kulia) akiwa na Katibu wa Kanisa Mwj. Oscar Mwanjala wakihitimisha Ibada kwa maombi.
NB: Vijana wote tunakaribishwa siku ya kesho kuanzia saa kumi kamili jioni kuendelea na Semina maalumu ya Vijana. Wewe Kijana unayesoma habari hii usikose, pia mualike na Kijana mwenzako.

Wednesday, 9 July 2014
ICC IBADA YA KUSIFU NA KUABUDU
Wakati umefika wa Kumuabudu Mungu katika Roho na Kweli.
Yohana 4:23 - 24.
Kwa maana saa ipo na sasa saa imefika, ambapo waabuduo halisi ,
watamwabudu Baba katika roho na kweli; Kwa maana Baba anawatafuta, watu kama hao, ili wamwabudu.
Kwa maana Mungu ni Roho, na wote wamwabuduo Yeye, imewapasa kumwabudu katika roho na kweli
Karibu sana ICC Sabasaba tumuabudu Mungu katika Roho na Kweli. Ubarikiwe.

Monday, 7 July 2014
SEMINA MAALUM YA VIJANA (CA's) ICC: KIZAZI CHA SASA NA UTUMISHI/HUDUMA
Siku ya leo Mzee Kiongozi wa ICC Mh. Mwl. Given Lemway a.k.a "Mzee wa Kweli kuu" amefanya Semina Maalum ya Vijana ili kuwanoa makali katika kumtumikia Mungu. Alifundisha somo "Kizazi cha sasa katika Utumishi/Huduma".
Mhubiri: Mh. Mwl. Given Lemway
Maandiko: Muhubiri 3:1 - 22; Matendo 1:8
Kweli Kuu: "Kwa kila Jambo na majira, nyakati na wakati wake chini ya mbingu ambalo Mungu amemwekea mwanadamu, kuzaliwa, kuishi na kufa kimwili na kiroho pia"
I. UTANGULIZI: Maana ya Maneno Muhimu
1. Kizazi:
> Ni kundi la watu waliozaliwa katika wakati unaofanana. Mfano 1940 - 1950; 1950 - 1960; 1970 - 1980 n.k
> Tangu Kanisa la T.A.G lianze miaka 75 iliyopita kuna kama vizazi vitatu vimepita hadi sasa. Kizazi cha kwanza ni cha miaka ya 1940 - 1950 miongoni mwao ni akina Askofu Lazaro ambao kimsingi walikabidhi kijiti kwa kizazi kilichofuata chja miaka ya 1950 - 1960 ambao ndio wanaomalizia kazi kwa sasa. Kizazi hicho cha pili kinatakiwa kukabidhi kwa kizazi cha miaka ya 1970 - 1980 ambacho ni Vijana wengi wenye nguvu kwa sasa. Swali, Je, kizazi hiki cha tatu kinatimiza wajibu wake ipasavyo katika kuhubiri Injili!!??
2. Wakati:
> Ni kiwango cha muda, nukta, saa hadi miaka. Daniel 7: 12 - 25.
> Kila mtu anapaswa kuutambua wakati wake.
3. Nyakati:
> Ni vipindi vya hesabu za kibiblia vinavyo onesha miaka na vizazi na utendaji wake.
> Mfano: katika kukua mwanadamu hupitia nyakati mbalimbali. Mfano Utoto, Ujana, Uzee.
4. Majira:
> Ni vipindi vya misimu vinavyo onesha matukio mbalimbali yaliyopita au yaliyotokea katika vizazi vilivyo pita.
> Mfano: Majira ya Sikukuu za idara kanisani kama CA's, WWK, CMF n.k kilka Idara inakuwa na majira yake kila mwaka.
> Kila kizazi kinapaswa kujitambua katika wakati, nyakati na majira mbalimbali.
> Kizazi hiki cha sasa (kizazi cha tatu) kinapaswa kujitambua kinafanya nini katika kumtumikia Mungu. Kizazi cha sasa kimekuwa bize sana katika facebook na blogs kuliko kumtumikia Mungu, Je ndilo agizo tulilopewa. Hivyo basi kizazi hiki kinapaswa kutumia teknolojia ya kisasa katika kuhubiri injili. Pia kutumia uwezo wa akili ambao Mungu kajaalia katika kuwaleta mataifa kwa Yesu.
> Imefika hatua sasa, Kanisa linaongezeka kibailojia na si kuhubiri watu injili na kuokoka. Kukua kibailojia maana yake kama Baba kaokoka, basi watoto wake nao wamezaliwa katika dini hiyo na kuendelea kuwa wafuasi wa dini kwa kuwa wamezaliwa humo. Hivyo kazi ya ziada inabidi ifanyike ili Kanisa lisiongezeke kibailojia tu bali kwa kuhubiri injili na kuwageuza mataifa waikubali kweli kuu.
> Kizazi cha sasa kimekuwa ni cha kutumwa zaidi kuliko kutumika. Lengo sio kutumwa bali kutumika nyumbani mwa Bwana. Hivyo basi kila Kijana anapaswa kuwa na ndoto ili amtumikie Mungu kutokana na ndoto yako, badala ya kuwa mtumwa. Leo utatumwa kafunge projector screen, kesho kafagie kanisa n.k badala ya kumtumikia Mungu.
II. MAKUNDI YA WATU WALIOTUMIA WAKATI WAO VIBAYA KATIKA BIBLIA:
i. Mfalme Sauli: 1 Samweli 15: 1 - 35
> Katika kipindi hiki Taifa la Israel liliongozwa na Mungu kupitia kwa Nabii wake Samweli. Samweli ndio alikuwa Kuhani Mkuu , hivyo Taifa lilipokea maagizo yote kutoka kwa Mungu kupitia kwake.
> Baada ya Samweli kuzeeka, watoto wake walianza kuhudumu katika madhabahu ya Bwana, lakini watoto hao walijawa na rushwa na kufanya mambo kinyume na Mungu.
> Taifa la Israel likadai kupatiwa Mfalme, ndio wakapewa Sauli awaongoze.
> Sauli hakuwa na roho ya utii, hakuonekana kukubaliana na maelekezo aliyokuwa akipewa na Samweli.
> Sauli aliutumia wakati wake mwingi kulipiza kisasi dhidi ya Daudi. Kwa kutoutambua wakati wake vyema Mungu alimkataa asiwe Mfalme.
> Sauli alipoteza uhusiano wake na Mungu kwa kuwa hakufuata maelekezo ya Mungu, Mungu akamkataa. Ikafika hatua Sauli alienda kwa waganga wa kienyeji (wapunga pepo) kuulizia mustakabali wake.
> Mwishowe Sauli alijiua mwenyewe kwa kuangukia upanga wake.
Mh. Mwl. Given Lemway akiendelea kushusha dozi ya ukweli kwa Vijana, yaani leo yalikuwa ni makavu live.
> Kutoka kwa Mfalme Sauli kuna mambo mengi ya kujifunza;
* Kizazi cha sasa tunapaswa kuutumia muda (Nyakati, wakati na majira) vizuri ili kutimiza agizo kuu la Bwana Yesu.
* Kizazi cha sasa tunapaswa kuwa watii wa maneno/maagizo ya Mungu.
* Tusipofuata maelekezo ya Mungu, Mungu atatukataa.
* Kizazi cha sasa tusipotambua nafasi zetu katika kumtumikia Mungu tutapoteza uhusiano wetu na Mungu.
* Endapo tutapoteza uhusiano na Mungu, tutakufa kiroho.
TAFAKARI, CHUKUA HATUA.
* Semina hii itaendelea tena Jumatatu wiki Ijayo Tarehe 14/07/2014. Karibuni wote.
Vijana wakisikiliza kwa umakini mkubwa, Ya leo ngumu kumeza haina kuremba mwandiko, yaani ni chungu lakini dawa.
Mkurugezi wa Idara ya Vijana (CA's) ICC Mr. Ezekiel Fungo akisisitiza jambo baada ya mafundisho ya leo.
Mh. Mwl. Given Lemway akiwa amepoz na Vijana baada ya somo.

Sunday, 6 July 2014
KUTOKA MADHABAHU YA ICC: USHINDI WA HALALI UPO KATIKA NENO LA MUNGU
Ibada ya Pili ya leo tumehudumiwa na Mch. MED VAHAYE wa T.A.G Kigonzile, amefundisha ujumbe unaosomeka "Ushindi wa Halali upo katika Neno la Mungu". Picha ya kwanza Mch. Med Vahaya akisalimia Kanisa katika Ibada ya kwanza, pembeni yake ni Mch. R. Kitine na mtafsiri wa matangazo Ms. Agreth Makombe. Picha inayofuata ni Ibada ya pili Mch. Vahaye akihudumu katika Madhabahu ya ICC.
Kama ilivyo ada ilianza Ibada ya kusifu na kuabudu;
Mr. Petro Ng'ondya akiongoza Jahazi la Timu ya Kusifu na kuabudu katika Ibada ya leo.
Mrs. Adder Mkea akiwakilisha kwa-stage
Katibu wa Kanisa Mwinjilisti Oscar Mwanjala naye siku ya leo alikwenda sambamba na Timu ya Kusifu na kuabudu.
Mtumishi wa Bwana Mr. Msigwa akiwa katika kusifu na kuabudu
Mch. Raphael Kitine naye akishiriki vyema Ibada ya kusifu na kuabudu.
Rabi Nuhu akipiga Keyboard huku akiwa katika uwepo wa Nguvu za Roho Mtakatifu.
Mwl. Alfa alikuwepo kuhakikisha gitaa la besi linaunguruma ipasavyo.
Dawati la IT lilisimamiwa vyema na Mr. Samwel Mkea.
Kila mtu yuko bize akiwajibika kwa nafasi yake kuhakikisha mabo yanakwenda sawia.
Kanisa lote kwa ujumla lilishiriki vyema Ibada hii.
Baada ya kusifu na kuabudu, Mch. Kitine alipanda Madhabahuni na kuhitimisha Ibada hiyo kwa kufanya Huduma ya Maombezi.
Baada ya kufanya maombezi, Madhabahu alikabidhiwa Mch. Vahaye akafanya vitu vyake kama alivyoongozwa na Roho wa Bwana.
Katika utangulizi wake alisoma Maandiko yafuatayo: 2 Tim 2:3 - 5; Mat 4:3 - 11, 16:18 - 19.
> Alianza kwa kufafanua kuwa Mwamini yeyote akilitumia Neno la Mungu ipasavyo, atamshinda shetani.
> Pia alisisitiza kuwa tulipe nafasi Neno la Mungu katika mioyo yetu; maana hata Yesu alimshinda Ibilisi kwa kuwa alikuwa amejawa na Neno.
> Akaendelea kufundisha kuwa Yesu alidhihirishwa ili azivunje kazi za ibilisi. 1 Yon3:8;
> Akiwa na upako wa hali ya juu akahimiza kwamba tunatakiwa kusimamia kanuni ambazo ni Neno la Mungu, wala tusiangalie ukubwa au udogo wa jaribu tunalokabiliana nalo. Isa 54:17
> Mwisho akahitimisha kwa kusema, tunalindwa na Nguvu za Mungu kwa njia ya Imani, hivyo tusimpe ibilisi nafasi katika mioyo yetu. 1 Petro 1:5; Ef 6:16, 4:27; 2 Yon 1:8.
Waamini wa ICC wakiwa wametulia kwa umakini mkubwa chini ya uwepo wa Roho wa Bwana wakifuatilia mahubiri.
Wahudumu a.k.a mashemasi katika Ibada ya leo wakitokelezea na tabasamu za ukweli
Mungu akubariki, karibu sana ICC.

Subscribe to:
Posts (Atom)