Mhubiri: Mrs. S. Kipemba
Maandiko:
Mathayo 7:13-14, 16; 3:1-3, 8-10; 2Timotheo 2:15-19; Mathayo 6:33; 22:37-39; Zaburi 122:1-2, 42:1-4
Muhubiri wa Ibada ya leo Mrs. S. Kipemba akihubiri Ujumbe kama unavyo onekana katika screen.
Kama ilivyo ada ICC, kabla ya kipindi cha mahubiri huwa inatangulia Ibada ya kusifu na kuabudu inayosimamiwa na Timu ya kusifu na kuabudu ya ICC. Naipenda Timu hii kwani hakuna mwimbaji anayejiona kuwa ni superstar kuliko wengine. Wote kwa pamoja huimba kwa kushirikiana kadri Roho wa Bwana anavyo waongoza.
Ms. Glory Chanai akiongoza wana Timu wenzake katika kusifu na kuabudu.
Ms. Joyce Senje naye akifanya yake katika madhabahu ya ICC
Ms. Aggy Msigwa naye akiwajibika vyema madhabahuni.
Mr. Petro na Mr. Alpha nao walikuwepo katika Timu ya kusifu na kuabudu
Mchungaji Mwanafunzi (Chuo cha Biblia Nairobi), Mch. Omega Kipemba akiwa ameungana na Timu Madhabahuni.
Ki ukweli siku ya leo ilikuwa ya kipekee sana, upande wa muziki walisimama vyema vijana wadogo sana ambao sikuwafikiria kama wanaweza kuhudumu kwenye Ibada ya Jumapili wakiwa chini ya usimamizi wa Mwalimu wao Mr. Alfa. Waliokuwepo Ibadani leo walishuhudia mambo ya vijana hawa, Mungu awatie Nguvu wasonge mbele. Keyboard alipiga Bwana mdogo James na gitaa la base alipiga mwenzie Amani. Walivitendea haki ipasavyo vyombo hivyo.
Upande wa dawati la IT alikuwepo Sir. ECHA, huku Mr. Gerald akitendea haki Taaluma yake kwa kuchukua matukio ibadani.
Ibada ya kusifu na kuabudu si ya Timu peke yake, bali ni Kanisa zima.
Mtumishi wa Bwana Mr. Joseph Fungo akishiriki ipasavyo katika Ibada ya kusifu na kuabudu.
Baada ya Ibada ya kusifu na kuabudu, mahubiri yalifuatia.
Mrs. S. Kipemba akihubiri siku ya leo.
Katika somo hili alifundisha kuwa katika maisha ya kila mwanadamu, kuna njia kuu mbili ambazo hupita na kila njia ina hatima yake. Njia ya kwanza ni njia pana ambayo hatima yake inaelekea upotevuni, na njia ya pili ni nyembamba ambayo hatima yake inaelekea uzimani. Kila mwanadamu hupita kwenye mojawapo, haiwezekani ukapita katika njia zote mbili au ukawa katikati ya njia hizo.
Alianza kwa kuelezea njia pana kisha akahitimisha kwa kuelezea njia nyembamba. Injili za aina hii zimemisi sana katika Makanisa mengi ya kizazi cha leo, kwani kila unapopita utasikia njoo kwa Yesu upokee muujiza wako. Pokea magari, pokea nyumba, pokea mume au mke n.k. Je, watu wenye vitu hivyo hawatakiwi kuja kwa Yesu!! Tafakari chukua hatua.
Mrs. S. Kipemba akiwa anahubiri katika uwepo wa Roho Mtakatifu Ibadani leo.
Njia pana:
i. Ina nafasi kubwa na inaruhusu watu wengi kupita kwa pamoja na mizigo yao.
ii. Ina ushawishi mkubwa na haina masharti magumu.
iii. Njia hii wanapita wapagani, wenye dini mbalimbali, mataifa mbalimbali; hata baadhi ya waamini waliookoka pia hupiata njia hii.
> Alisisitiza kuwa walokole wanaopita njia hii ni wale waliopoteza mwelekeo wakidhani kuwa mtu anapo okoka ndio kamaliza kila kitu. La hasha! Kuokoka ni mwanzo tu wa safari ndefu san ya Mwamini, changamoto iliyopo ni kuishi maisha matakatifu ya ushindi siku zote.
> Msingi wa maisha yetu ya ulokole ni kuyafanya mapenzi ya Mungu na si vinginevyo. Watu wengi siku za leo wanasimamia zaidi masuala ya miujiza na uponyaji kuliko kuishi maisha ya utakatifu. Matokeo yake ni kuishi maisha ya mazoea na kuishia kupita njia pana inayoelekea upotevuni.
> Pia akasisitiza kuwa miujiza sio kigezo cha mtu kuwa amekubalika na Mungu, uhusiano na Mungu ndio jambo la msingi sana kuliko jambo lolote.
Kuonesha msisitizo ili mlazimu kuacha madhabahu na kuwafuata washirka walipokaa
Njia nyembamba:
i. Njia hii imesonga sana, inaruhusu kupita mtu peke yake bila kuwa na mizigo ya aina yeyote ile.
ii. Ili kupita njia hii, mtu ni lazima afanye maamuzi mazito ya kuuvua utu wa kale.
iii. Njia hii inahitaji mtu kujikana.
> Wokovu ni kusonga mbele wala si kuangalia nyuma.
> Unapoamua kuokoka ni lazima uamue kukabiliana kwa dhati na changamoto mbalimbali unazokutana nazo njiani.
> Biblia inasema kuwa kila alitajaye Jina la Bwana na auache uovu.
iv. Unapoamua kupita Njia hii, ni lazima Yesu awe kipaumbele katika maisha yako.
> Siku za leo watu wengi wamekuwa na vipaumbele vingine badala ya Yesu.
> Kwa mfano msimu huu ni wa kombe la Dunia, watu wengi wameweka mashindano hayo kuwa kipaumbele kuliko Yesu. Imefika wakati watu wanashindwa kukesha makanisani lakini wapo tayari kukesha kuangalia kombe la Dunia.
Mwisho Ibada iliahirishwa kwa maombi yaliyoongozwa na Mtumishi wa Bwana Mch. Omega Kipemba.
Mch. Omega Kipemba (Kulia) akiwa na Katibu wa Kanisa Mwj. Oscar Mwanjala wakihitimisha Ibada kwa maombi.
NB: Vijana wote tunakaribishwa siku ya kesho kuanzia saa kumi kamili jioni kuendelea na Semina maalumu ya Vijana. Wewe Kijana unayesoma habari hii usikose, pia mualike na Kijana mwenzako.
No comments:
Post a Comment