Ibada ya Pili ya leo tumehudumiwa na Mch. MED VAHAYE wa T.A.G Kigonzile, amefundisha ujumbe unaosomeka "Ushindi wa Halali upo katika Neno la Mungu". Picha ya kwanza Mch. Med Vahaya akisalimia Kanisa katika Ibada ya kwanza, pembeni yake ni Mch. R. Kitine na mtafsiri wa matangazo Ms. Agreth Makombe. Picha inayofuata ni Ibada ya pili Mch. Vahaye akihudumu katika Madhabahu ya ICC.
Kama ilivyo ada ilianza Ibada ya kusifu na kuabudu;
Mr. Petro Ng'ondya akiongoza Jahazi la Timu ya Kusifu na kuabudu katika Ibada ya leo.
Mrs. Adder Mkea akiwakilisha kwa-stage
Katibu wa Kanisa Mwinjilisti Oscar Mwanjala naye siku ya leo alikwenda sambamba na Timu ya Kusifu na kuabudu.
Mtumishi wa Bwana Mr. Msigwa akiwa katika kusifu na kuabudu
Mch. Raphael Kitine naye akishiriki vyema Ibada ya kusifu na kuabudu.
Rabi Nuhu akipiga Keyboard huku akiwa katika uwepo wa Nguvu za Roho Mtakatifu.
Mwl. Alfa alikuwepo kuhakikisha gitaa la besi linaunguruma ipasavyo.
Dawati la IT lilisimamiwa vyema na Mr. Samwel Mkea.
Kila mtu yuko bize akiwajibika kwa nafasi yake kuhakikisha mabo yanakwenda sawia.
Kanisa lote kwa ujumla lilishiriki vyema Ibada hii.
Baada ya kusifu na kuabudu, Mch. Kitine alipanda Madhabahuni na kuhitimisha Ibada hiyo kwa kufanya Huduma ya Maombezi.
Baada ya kufanya maombezi, Madhabahu alikabidhiwa Mch. Vahaye akafanya vitu vyake kama alivyoongozwa na Roho wa Bwana.
Katika utangulizi wake alisoma Maandiko yafuatayo: 2 Tim 2:3 - 5; Mat 4:3 - 11, 16:18 - 19.
> Alianza kwa kufafanua kuwa Mwamini yeyote akilitumia Neno la Mungu ipasavyo, atamshinda shetani.
> Pia alisisitiza kuwa tulipe nafasi Neno la Mungu katika mioyo yetu; maana hata Yesu alimshinda Ibilisi kwa kuwa alikuwa amejawa na Neno.
> Akaendelea kufundisha kuwa Yesu alidhihirishwa ili azivunje kazi za ibilisi. 1 Yon3:8;
> Akiwa na upako wa hali ya juu akahimiza kwamba tunatakiwa kusimamia kanuni ambazo ni Neno la Mungu, wala tusiangalie ukubwa au udogo wa jaribu tunalokabiliana nalo. Isa 54:17
> Mwisho akahitimisha kwa kusema, tunalindwa na Nguvu za Mungu kwa njia ya Imani, hivyo tusimpe ibilisi nafasi katika mioyo yetu. 1 Petro 1:5; Ef 6:16, 4:27; 2 Yon 1:8.
Waamini wa ICC wakiwa wametulia kwa umakini mkubwa chini ya uwepo wa Roho wa Bwana wakifuatilia mahubiri.
Wahudumu a.k.a mashemasi katika Ibada ya leo wakitokelezea na tabasamu za ukweli
Mungu akubariki, karibu sana ICC.
No comments:
Post a Comment