Sunday, 20 July 2014

Udhihirisho wa Nguvu za Roho Mtakatifu Ibadani ICC

Shalom!
Mungu ni mwema wakati wote. Roho wa Bwana ameendelea kuhudumia watu wake katika Ibada zote mbili za ICC siku ya leo.

Ibada ya kwanza inayoendeshwa kwa lugha ya Kiingereza alihudumu mpakwa mafuta wa Bwana Mch. Omega Kipemba, ambaye kwa sasa yupo likizo anasoma Chuo cha Theolojia kilichopo Nairobi Kenya. Alifundisha Ujumbe wenye kichwa cha habari "PNEUMATOLOGY".  He defined Pneumatology as the study of the person and the work of the Holy Spirit. The leading scriptures were from the book of John 14:15-18. He also defined Pneumatology as the theological discipline that focuses only on the Holy Spirit. This discipline is covered all over the Bible from the book of Genesis to the book of Revelation. Other sciptures Mathew 19:28; Titus 3:5; John 3:3; Eph 2:6, more deatails about this subject will be available here later. Stay tuned, Usitoke usiondoke.
Mch. Omega Kipemba akiwa na Mtafsiri wake Mr. Edson Ishengoma wakichimbua madini ya ukweli toka kwenye mgodi wa Roho Mtakatifu.

Ibada ya pili inayoendeshwa kwa lugha ya Taifa alihudumu Mtumishi wa Bwana Mch. Ruth Kyando ambaye naye yupo likizo, anasoma Chuo Cha Biblia Dodoma.  Yeye alifundisha Ujumbe wenye kichwa cha habari "ROHO MTAKATIFU",  Maandiko: Mwanzo 1:2; Mk 1:10-11; Mt 28:19; Yohana 14:16, 26-27; 16:8-13. Somo kamili utalipata hapahapa. Ndio maana nikasema ni Ibada ya Udhihirisho wa Roho Mtakatifu, kwani Ibada zote mbili Watumishi wa Bwana wamefundisha Jumbe zenye maudhui yanayofana ingawa kila mmoja lifundisha kadri Roho wa Bwana alivyomuwezesha.
Mch. Ruth Kyando akiwa madhabahuni ICC, kidigitali zaidi lakini Roho Mtakatifu anajidhihirisha.

Kama ilivyo kawaida, Ibada ya Sifa hutangulia kabla ya mahubiri. Katika Ibada zote mbili Timu ya Kusifu na Kuabudu ilifanya vyema katika kuliongoza Kanisa kwenye Sifa na Kuabudu.
Timu ya Kusifu na Kuabudu ya ICC ikiwajibika ipasavyo Madhabahuni.

Kwaya ya Kanisa PATMO nao walihudumu katika Madhabahu ya ICC.
Patmo Christian Singers (PCS) ya ICC wakifanya yao Madhabahuni.

Kanisa zima kwa ujumla lilishiriki vyema katika kumsifu na kumuabudu Mungu katika Roho na kweli.

Baada ya Ibada ya Kusifu na Kuabudu, ilifanyika Ibada ya Maombezi iliyoongozwa na Mchungaji Kiongozi wa ICC Mch. Raphael Kitine kwa kushirikiana na Wachungaji waliohudumu Ibada zote za leo na Wazee wa Kanisa.

Upande wa muziki, Mwl. Alpha aliwaongoza vyema vijana wake Amani na James.

Matukio yalichukuliwa na Mr. Gerlad, dawati la IT kama kawaida Mr. Mkea na Sir ECHA waliwajibika ipasavyo

Kumbuka kuanzia Jumatatu (21/07/2014) hadi Jumamosi (26/07/2014) ni Wiki ya Maombi ya Kufunga kwa Kanisa zima. Tutakuwa tunakutana Kanisani kila siku kuanzia saa kumi na nusu jioni.

Karibu sana ICC, Mungu akubariki.

No comments:

Post a Comment