Saturday, 21 June 2014

Askofu Mkuu Dr. Barnabasi Mtokambali ashiriki Maadhimisho ya Jubilee ya Miaka 75 ya T.A.G Jimbo la Iringa

Hatimaye Jimbo la Iringa laadhimisha miaka 75 tangu kuanzishwa kwa Kanisa la T.A.G, katika  maadhimisho haya Askofu Mkuu wa T.A.G Dr. Barnabas Mtokambali alishiriki kikamilifu katika matukio yoote.

Shughuli ilianza majira ya asubuhi kwa Wadau mbalimbali kukutana katika Centre ya Tanangozi kabla ya kufanya maandamano ya pamoja kulekea mahali ambapo kinajengwa Chuo Cha Ualimu Jimbo la Iringa.

Baada ya muda Askofu wa Jimbo la Iringa. Mch. Mkane aliwasili, akafanya maombi rasmi kwaajili ya kuanza maandamano kuelekea eneo la tukio.

Maandamano yalianza rami hadi eneo la tukio, baada ya kuwasili ilifanyika Ibada ya sifa ya ukweli si mchezo;

Kwaya mbalimbali zilikuwepo kuhudumu;


MC wa shughuli nzima alikuwa ni Mchungaji Raphael Kitine ambaye ni Mchungaji Kiongozi wa Iringa Central Church (ICC) na pia ni Katibu wa Jimbo la Iringa.

Baada ya hekaheka za hapa na pale hatimaye ule muda wa kuweka rasmi jiwe la msingi ukawadia, Askofu Mkuu, Dr. Barnabasi Mtokambali akaongoza jopo la Wachungaji kufanya maombi maalum na kuweka rasmi jiwe la msingi.

No comments:

Post a Comment