Tuesday, 24 June 2014

KUTOKA MADHABAHUNI ICC: MATOKEO YA KUFANYA MAAMUZI MAGUMU

Shalom Shalom!
Mungu ni mwema siku zote katika maisha yetu na anatuwazia yaliyo mema. Jumapili ya Tarehe 22/06/2014 Mungu ameendelea kusema na Watu wake kupitia kwa mpakwa mafuta wa Bwana, na Mchungaji Kiongozi wa ICC Mch. Raphael Kitine. Katika Ibada ya pili ICC inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, Mtumishi wa Mungu Mch. Kitine alihubiri katika uwepo wa Mungu wa hali ya juu sana Somo aliloliita " Matokeo ya kufanya Maamuzi Magumu". Ulikuwa ni Ujumbe wenye Nguvu za Mungu ambao ulimgusa kila mtu.

Kama kawaida, kabla ya Neno ilitangulia Ibada ya Sifa na Kuabudu ambayo nayo ilijawa na uwepo wa Roho Mtakatifu isivyo kawaida. Roho wa Bwana alitamalaki kiukweli katika Ibada hii.
Mch. Kitine (wa kwanza kushoto) akienda sambamba na Timu ya Kusifu na Kuabudu katika Ibada ya kwanza. Anayefata ni Mrs. Adder Mkea, Ms. Agreth Makombe, Ms. Glory Chanai na Mr. Petro Ng'ondya.

Sifa na kuabudu Ibada ya pili ilisimamiwa na Timu ya Kusifu na kuabudu ikiongozwa na Mrs. Mahinya, aliyeshirikiana vyema na Timu nzima.

Kanisa zima nalo lilishiriki kikamilifu katika Ibada hii ya Kusifu na Kuabudu;

Upande wa mziki alisimama vilivyo Rabi Nuhu katika Keyboard, upande wa gitaa alishirikiana Mr. Nicas pamoja na Bwana mdogo anayechipukia kwa spidi ya hatari katika upigaji wa base Ndg. James. Katika benchi la IT alisimama sawia Mr. Mkea kuhakikisha mambo yanakwenda vile inavyotakiwa.

Baada ya Ibada ya kusifu na kuabudu ndipo akasimama Mch. Raphael Kitine kuleta Neno la Bwana.Ujumbe ni "Matokeo ya Kufanya Maamuzi Magumu" kama unavyoonekana katika Screen.
MAANDIKO YA SOMO: 2 Wafalme 7:3-9; Mt 16:24-25.

Wakati wote wa Mahubiri Kanisa lilikuwa na utulivu wa kutosha.

I. UTANGULIZI:

1. MAANA YA NENO MAAMUZI MAGUMU:
>  Ni tendo la mtu kukata shauri kufanya jambo tata lisilowezekana katika hali ya kawaida.
2. WENYE UKOMA: 2Fal 7:3
> Katika Taifa la Israel ukoma ulifananishwa na dhambi na laana.
> Wagonjwa  wa Ukoma walitengwa na Jamii ili wasiweze kuambukiza Watu wengine.
> Wagonjwa wanne wenye Ukoma walitengwa na Jamii na kuishi nje ya Mji.
3. MAAMUZI MAGUMU: 2Fal 7:4-5
> Njaa ilikuwa kali sana katika Mji wa Samaria ambapo Wakoma walilazimika kufanya maamuzi magumu, yaliyohatarisha maisha yao.
> Maamuzi magumu katika kuacha kufanya jambo linaloonekana kuwa faida kwake lakini linahatarisha usalama wa maisha yake ya kiroho. Mfano: Yusufu, Mwanzo 39:5-12; Musa, Kutoka 2:11-15.
> Maamuzi magumu katika kutetea haki hata kama inahatarisha usalama wa maisha yako. Mfano: Daniel, Daniel 6:10-16; Stefano, Matendo 7:57-60.
> Kufanya maamuzi magumu wakati unapokutana na mapingamizi ya kifamilia kuhusu wokovu. Dan 3:17-18
> Kufanya maamuzi magumu unapojitokeza ugumu katika kumtolea Mungu. Mwanzo 22:2-3

II. SOMO LENYEWE: MATOKEO YA MAAMUZI MAGUMU 2Fal 7:6-8
1. Kukuzwa kwa vishindo vya miguu yao kufikia sawa na magari ya kivita na kusababisha kuwa tishio kwa maadui Washami. (Mstari 6).
> Waamini walioamua kuchukua hatua katika yale wanayofanya, yanakuzwa maradufu katika ulimwengu wa Roho. Mt 18:18;
> Kinywa cha Mtu mwenye maamuzi magumu ni pigo kubwa mbele ya shetani katika ulimwengu wa Roho. Luka 10:18-19;
> Ukifanya maamuzi magumu katika majaribu unayoyapitia, utapita pamoja na Mungu na kumtia hofu kubwa shetani. Yer 1:8-10.
2. Maadui waliojipanga kwa vita hukimbia kwa hofu kubwa na kuacha kila kitu kwa ajili ya kujiponya nafsi zao. (Mstari 7).
> Kwa kufanya maamuzi magumu maadui waliojipanga dhidi yako hukimbia. Kumb 28:7;
> Kwa kufanya maamuzi magumu, jaribu ulilonalo hutafuta mlango wa kutokea na kutoweka kabisa. Matendo 16:22-26.
3. Wenye Ukoma waliodharauliwa sasa kuwa matajiri na watetezi wa Jamii iliyochoka kwa njaa na umasikini. (Mstari 8)
> Kwa kufanya maamuzi magumu mahali ulipodharauliwa utainuliwa. Mwanzo 41:38-41;
> Maamuzi magumu hukutoa katika jaribu zito kuelekea katika mafanikio ya ajabu. Ayubu 42:10

III. HITIMISHO: WENYE UKOMA KUTANGAZA HABARI NJEMA KWA JAMII ILIYOWADHARAU.
> Furaha ya kufunguliwa humfanya mwenye haki kutojizuia kutangaza habari njema. Yn 4:28-29.

Baada ya Mahubiri, Mch. Kitine alifanya maombezi kwa waamini wote.

No comments:

Post a Comment