Kaambi ya Vijana (CA's) iliyoandaliwa na T.A.G Sehemu ya Iringa imefunguliwa rasmi leo hii na Mwangalizi wa T.A.G Sehemu ya Iringa Mch. Mlumbe. Kambi hii inafanyikia katika Kanisa la T.A.G Cornerstone kwa Mch. Matipa.
Mwangalizi wa Sehemu ya Iringa Mch. Mlumbe (Aliyevaa Suti) akiwa na Kiongozi wa CA's Sehemu ya Iringa Mr. Ezekiel Fungo, pamoja na Vijana kutoka Sehemu mbalimbali za Iringa.
Baada ya ufunguzi wa Kambi hili, Mch. Mlumbe alimkaribisha mwalimu wa kwanza ambaye ni Mch. Raphael Kitine, kabla ya kumkaribisha aliuliza kama Vijana wamekuja na dhana zao za kazi zikiwemo Biblia, Daftari na Kalamu. Vijana kiukweli wamejipanga vyema kwani wote walionesha dhana zao za kazi.
Baada ya hapo akamkaribisha Mch. Kitine aendelee na mafundisho.
Mch. Raphael Kitine akiweka mambo sawa kabala hajaanza kufundisha. Alifundisha somo lenye kichwa cha habari Semina ya Vijana kuhusu Uchumba.
Alianza kwa kutoa utangulizi kuwa somo hili sio maalumu tu kwa Vijana ambao hawajaoa na kuolewa bali watu wote. Kwani wale ambao wameshaoa au kuolewa wanapata ujuzi ambao watautumia kwenda kufundisha Vijana wengine huko wanapotoka. Pia litawasaidia kuongeza ufahamu na kujiweka katika nafasi nzuri ya kuwasaidia Vijana Makanisani.
Wadau wakifatilia somo kwa umakini mkubwa, mikononi wakiwa na dhana za kazi. Somo kamili litawajia hapahapa, usitoke usiondoke stay tuned.
Baada ya kupata dozi ya ukweli, Vijana walipata muda wa mapumziko ambao waliutumia kwa kusifu na kuabudu.
No comments:
Post a Comment