Shalom!
Siku ya Jana (07/06/2015) katika Ukumbi wa Lugalo, Kwaya ya kuu ya Kanisa ICC imezindua Albamu yake ya kwanza ya Audio iliyobeba Jina la "NYAMAZA". Mungu ni mwema, uzinduzi ulikwenda vzr, Sifa na Utukufu kwa Mungu juu mbinguni. Ameen.
Zifuatazo ni picha mbalimbali za tukio zima la uzinduzi.
Ukumbi wa Sekondari Lugalo ulipofanyika uzinduzi kabla ya kuanza shughuli.
Wanakwaya wa Patmo wakiwa katika pouz kabla ya kuingia Ukumbini kwaajili ya Uzinduzi
Wanakwaya ya Patmo wakielekea Ukumbini
Katibu wa Kwaya ya Patmo Mr. Nico William, akisoma Risala mbele ya Mgeni Rasmi wakati wa Uzinduzi. Aliyemshikia kipaza sauti ni Mwalimu wa Kwaya Mr. Alpha.
Kabla ya Uzinduzi, Mchungaji Kiongozi alikabidhiwa Box lenye CD hizo, kisha ikafanyiwa maombi kama Ishara ya kuwekwa Wakfu tayari kwa uzinduzi
Mgeni Rasmi akipokea CD ya Albamu ya NYAMAZA na kukata utepe kama Ishara ya Uzinduzi
Wanakwaya ya Patmo wakiwa tayari kuimba baada ya kukatwa utepe, MC wa Shughuli hii alikuwa ni Mr. Timiza Lwisa anayeonekana mbele ya Kwaya ya Patmo.
Hapo sasa kazi imeanza, ngoma inogile...
Meza kuu ikifuatilia Kwa umakini tukio zima la uzinduzi, katikani ni Mwakilishi wa Mgeni Rasmi kulia kwake ni Mch. R. Kitine (Mchungaji Kiongozi wa ICC na Mlezi wa Kwaya ya Patmo), kushoto ni Mr. O. Mwanjala (Katibu wa Kanisa ICC)
Kwaya, Vikundi na Waimbaji binafsi pia walialikwa katika Uzinduzi huu, na wote walipewa nafasi ya kuhudumu kabla ya Kwaya ya Patmo hawajapandaa Jukwaani. Ki ukweli palinoga sana...
Wanakwaya ya Patmo wakiwa wenye furaha baada ya Uzinduzi wa Albamu ya NYAMAZA.
Mungu Awabariki woooote waliowezesha mafanikio ya Uzinduzi wa Albamu hii.
No comments:
Post a Comment