Na. Mch. Paul Mulumbe (Semtema T.A.G)
Mtumishi wa Bwana Mch. Paul Mulumbe akihubiri katika Madhabahu ya ICC
Shalom!
Jumapili hii ICC tulipata Neema ya kutembelewa na Mtumishi wa Bwana Mch. Paul Mulumbe kutoka Kanisa la T.A.G Semtema. Alihudumu Ujumbe unaosema "Yesu Kristo Ni Kiini Cha Furaha Ya Mwamini".
Maandiko: Wafilipi 4:4-9; Waebrania 11:4.
Katika somo hili alisisitiza kuwa mali na fedha sio chanzo cha kumfanya Mtu awe na furaha. Kwani wapo matajiri wengi wenye pesa na mali za kutosha lakini hawana amani. Hivyo mpendwa katika Bwana Kiini cha Furaha ya kweli ni kuwa na Yesu Kristo. Haijalishi unapita katika mgumu namna gani, kwenye dhiki, shida na taabu, tunapaswa kumtumainia Yesu Kristo.
Ubarikiwe.
Waamini wa ICC wakifuatilia mahubiri kwa umakini mkubwa.
Zifuatazo ni picha mbalimbali wakati wa Ibada
No comments:
Post a Comment