Shalom!
Karibu tena katika Wasaa wa kujifunza Maneno ya Mungu. Siku ya leo upo na Mtumishi wa Mungu kutoka ICC, Mr. Peter Brian Genya. Akifundisha Ujumbe unaosema "Mlima Wako, Baraka Yako" Milima Kama Chanzo Cha Baraka.
Mr. Peter Brian Genya akifundisha na kuhubiri katika Madhabahu ya ICC Lugalo
Katika Somo hili Mtumishi wa Bwana alitumia Milima kama kiwakilishi cha Vizuizi, Vikwazo, Majaribu, Matatizo au Upinzani unaokabiliana nao. Lakini jambo unalopaswa kufahamu ni kuwa Milima hiyo ndiyo Chanzo cha Baraka zako. Hupaswi kuukimbia au kuukwepa mlima, bali unapaswa kumuomba Roho Mtakatifu ili akusaidie kutambua aina ya mlima unaokabiliana nao ili akupe namna ya kuweza kushinda.
Alifundisha kuwa, katika Ulimwengu wa Kiroho unaweza kukabiliana na Milima kwa Namna tatu:
1. Milima ya Kusawazisha.
> Milima ya namna hii unahitaji kutumia buldozer linaloitwa Imani ili kukabiliana nayo, ni vita inayohitaji kupiganwa. Mlima wa kusawazisha ni kikwazo kinachozuia Baraka zilizo mbele yako, hivyo ni lazima uisawazishe/uiondoe ili ufike kwenye Baraka yako. Marko 11:22-23.
2. Milima ya Kupanda
> Milima ya namna hii haihotaji kusawazishwa, unahitaji kupanda hadi kileleni ili uifikie Baraka yako. Kwani Baraka yako ipo juu ya Mlima, hivyo unahitaji kuwa na Nguvu ya kufika juu y kilele cha mlima na kama ni vita basi ni ya kuvumilia. Isaya 40:28-31; Hesabu 14:44; Kumb 1:41,43.
3. Milima ya Kuzunguka.
> Aina hii ya milima haihitaji kusawazisha wala kupanda, bali inahitaji kuizunguka. Hii ni vita ambayo wewe huitaji kujipigania bali Bwana wa Majeshi husimama kupigana vita hivi. Milima hii inahitaji Kumtumaini Bwana tu, na unamwachia Bwana ajitetee mwenyewe. Zaburi 131; Kum 1:2,6,19. mifano ipo mingi katika Biblia. Shimei/Daudi 2Sam 16:5-13; Waisrael/Bahari/Majeshi ya Misri Kutoka 14:13-31; Vita 2 Falme 19:35.
Mpendwa katika Bwana hiyo ni kwa ufupi tu. Fatilia mafundisho haya ili upate kujua Mlima unaokabiliana nao ni wa Namna gani, Vipi ukabiliane nao, na makusudi ya Milima hiyo.
Mungu Akubariki.
Mtumishi wa Bwana Peter Brian Genya, akiitendea Haki Madhabahu ya ICC Lugalo.
Mafundisho mazuri, Ubarikiwe na Bwana Yesu
ReplyDelete