Thursday, 4 June 2015

UZINDUZI UZINDUZI UZINDUZI

Shalom!

Ni uzinduzi wa Audio Album ya Kwaya Kuu ya Kanisa ICC, Patmo Christian Singers. Uzinduzi wa Albamu hii inayoitwa 'NYAMAZA' utafanyika Jumapili ya Tarehe 07/06/2015 kuanzia saa saba mchana katika Ukumbi wa Sekondari ya Lugalo, Watu woooote mnakaribishwa. Albamu hii imebeba nyimbo nyingi zenye ujumbe muhimu sana utakaokusaidia katika maisha yako ya kimwili na kiroho.

Unaweza Kujiuliza NYAMAZA maana yake nini!!??

Wimbo huu unatufundisha wapendwa kukaa kimya endapo utatukanwa, utadharauliwa au kudhihakiwa. Huna haja ya kujitetea au kujipigania. Unapaswa kunyamaza kimya ili BWANA WA MAJESHI, YESU KRSISTO wa Nazareth ajitwalie utukufu. Kunyamaza ni dawa, kunyamaza ni Hekima, kunyamaza ni ishara ya unyenyekevu mbele za Mungu. Nyamaza kimya, ili Bwana ajitwalie utukufu.

Ukipata taarifa hii, tafadhali mjulishe na mwenzako. Mungu Akubariki.
Zifuatazo ni baadhi ya picha mbalimbali za Wana-Kwaya ya Patmo ICC, Siku waliyotangaza rasmi kuhusu uzinduzi wa Albamu yao ya Nyamaza..
Katibu wa Kwaya ya Patmo, Mr. Nico William akihamsisha kuhusu Uzinduzi wa Albamu ya Nyamaza. Kwambaali ni Wanakwaya wa Patmo na Mch. Raphael Kitine akimsikiliza kwa umakini.

Wanakwaya ya Patmo wakiwa katika Pouz nje ya Ukumbi wa Sabasaba (Enzi hizo ICC-Sabasaba)

Wanakwaya wa Patmo wakiwa tayari kwa Huduma katika Madhabahu ya ICC

Hapo sasa ni pouz za kikazi zaidi.

Tafadhali sana usikose tukio hili muhimu sana na la kihistoria kwa Kwaya yetu.

No comments:

Post a Comment