Thursday, 31 July 2014

MKUTANO WA INJILI ICC SABASABA WAANZA RASMI LEO

Leo hii Waamini wa ICC Sabasaba tumekutana katika Viwanja vya ICC Sabasaba kwa ajili ya kuanza rasmi Mkutano wa Injili, ambao unaendeshwa na Idara ya Uinjilisti ya Kanisa.

Kabla ya Muhubiri kusimama, Mch. Ruth Kyando alisimama kutoa maneno ya utangulizi.


Muhubiri wa Mkutano huu ni Mchungaji na Mwinjilisti Omega Kipemba.

UJUMBE: UKIWA KATIKATI.
MAANDIKO
: Yohana 6:15-22; Kutoka 6:9.

Akihubiri kwa upako wa hali ya juu, alisema kwamba ukiwa katikati ya shida, adha, taabu, mateso na dhiki, mtu hukata tamaa na kuona hakuna tumaini wala msaada. Lakini unapaswa kufahamu kuwa Yesu yupo kukusaidia na kukukwamua kutoka katika hali uliyonayo.


Mchungaji na Mwinjilisti Omega Kipemba akiwa Jukwaani akihubiri.

Somo hili ataendelea nalo kipindi chote cha Mkutano, tafadhali usikose. Karibu Bwana aseme nawe ukiwa katikati ya hali yoyote unayopitia.

Kwaya ya Kanisa ya Patmo pia walihudumu katika siku ya leo.

Baadhi ya watu waliofika kwenye Mkutano wakiwa katika kipindi cha kusifu.

Usikose kesho. Mungu akubariki.

Wednesday, 30 July 2014

UZINDUZI WA WIKI YA UINJILISTI ICC. Marko 16:15

WIKI YA UINJILISTI ICC YAZINDULIWA KIANA YAKE LEO.

Siku ya leo, Kanisa la ICC limezindua rasmi Wiki ya Uinjilisti kwa Waamini wote kukutana Kanisani, kupeana maelekezo na kusambaa mitaani kwenda kuhubiri Injili.
Wiki ya Uinjilisti inatimiza agizo kuu alilotuachia Bwana Yesu kabla hajapaa kurudi mbinguni kuketi mkono wa kuume wa Mungu. Marko 16:15-20.
Baada ya uzinduzi huu wa leo, kuanzia kesho (31/07/2014) hadi Jumamosi (02/08/2014) kutakuwa na Mkutano Mkubwa wa Injili katika Viwanja vya Sabasaba Iringa kuanzia saa kumi kamili Jioni. Atakayehubiri katika Mkutano huu Mkubwa wa Injili ni mpakwa mafuta wa Bwana, Mchungaji na Mwinjilisti Omega Kipemba.
Wagonjwa na wenye shida mbalimbali wataombewa. Karibuni wote, wewe upataye Ujumbe huu tafadhali mjulishe na mwenzako

Picha za Baadhi ya Waamini wa ICC waliofika leo Kanisani kwa ajili ya uzinduzi wa Wiki ya Uinjilisti.



PNEUMATOLOGY

By.  Rev. Omega Kipemba.

I. MEANING OF PNEUMATOLOGY:
  • It is the study of the person and the work of the Holy spirit.
  • Is the theological discipline that focuses only on the Holy spirit.
  • This discipline is allover the Bible.
II. PROMISES OF THE HOLY SPIRIT
* Jn 14;16-18
"And I will ask the Father, and he will give you another Counselor(comforter, Helper, Intercessor, Advocate, Strengthener, Standby) that he may remain with you forever"(Amp).

".. that he may remain with you forever
  • The word Remain in Greek is Meno, in John's gospel occurs 41 times and in his epistles occurs 26 times . 67 Times in all.
  • The word “Meno” means; abide, dwell, remain, continue, endure, tarry, be present and abide still.

 III. HIS WORKS TO THE CHURCH
A. Regeneration
  • Freligh, defines regeneration as that supernatural and immediate change fashioned by the Holy Spirit in the nature of the person who receives the Lord Jesus Christ.
 NB:The form of the church in any age is prescribed by the Holy Spirit.
  •  It is not an evolutionary change, but a revolutionary one (pp 55).
  •  It is the act which is done by God to a believer and it takes place within the nature of a man himself.
  • The word regeneration occurs twice in the bible,  Mathew: 19:28, and Titus 3:5. 
  • According to these scriptures regeneration is regarded as being reborn.
> This word Regeneration,in Greek is Palingenesias.
> In relation to the nature of man, it includes the various expressions used for eternal life which are;
  • New birth, (Jn 3:3)
  • Spiritual resurrection (Eph 2:6),
  • New mind (1 Cor 2:16): We do not reason about the word of God we obey it. 
  • Sons of God (Jn 1:12): A Christian with power and the desire to accomplish something can do anything." 
  • Made alive (Rom 8:11) 
  • Translation into the kingdom (2 Pet 2:9)
Rev. Omega Kipemba (RHS) alongside with his Translator Mr. Edson Ishengoma (LHS).

Monday, 28 July 2014

SOMO LA UBATIZO WA ROHO MTAKATIFU

By. Rev. Raphael Kitine (Mchungaji Kiongozi - ICC)

Maandiko: Mdo 1:4-5.

I. UTANGULIZI -MAANA YA UBATIZO WA ROHO MTAKATIU
  1. Ni tendo la kuzamishwa na kujaa Roho Mtakatifu. Mdo 1:4, 2:4.
  2. Ni tofauti na kuzaliwa mara ya pili. Yn 20:22; Mdo 2:4, 8:12, 1:4.
  3. Ni kipawa cha Nguvu kutoka kwa Mungu. Lk 24:49; Mdo 1:8; Lk 1:35.
  4. Ni ahadi kwa wote waaminio. Mdo 2:4, 39.
II. UMUHIMU WA UBATIZO WA ROHO MTAKATIFU.
  1. Imeagizwa katika maandiko. Ef 5:18, Mdo 1:4-5.
  2. Ni chanzo cha Nguvu za Kiroho:
    • Katika Huduma ya Yesu Kristo. Mdo 10:38; Lk 4:1.
    • Katika Huduma ya Kanisa la kwanza. Mdo 1:8, 2:4, 4:31, 33.
III. JINSI YA KUBATIZWA NA ROHO MTAKATIFU.
A. MASHARTI YA KUBATIZWA NA ROHO MTAKATIFU.
  1. Lazima uzaliwe mara ya pili. Yn 14:17; 3:5-7.
  2. Upende kujazwa na Roho Mtakatifu. Mt 5:6; Rm 15:16; 1Kor 6:11, 7:37.
  3. Mtii Mungu. Mdo 5:32.
B. HATUA TATU ZA KUPOKEA ROHO MTAKATIFU.
  1. Karibia kwa ujasiri katika kiti cha neema. Ebr 4:16.
  2. Mwombe Mungu akujaze Roho Mtakatifu. Lk 11:10, 13.
  3. Msifu Mungu kwa Imani. Mk 11:24; Lk 24:53.
C. USHAHIDI WA KUBATIZWA NA ROHO MTAKATIFU.
  1. Kunena kwa lugha. Mdo 2:3, 10:45-47, 19:1-6.
  2. Ishara hizi zitafuata ukitembea katika Roho:
    •  Kuwa na uwezo wa kutenda kazi za Yesu. Yn 14:16-18, 16:14.
    • Kuhisi uwepo wa Mungu. Yn 14:16-18.
    • Kusikia vibaya kuhusiana na dhambi. Yn 16:7-11.
    • Kuwa na uwezo wa kushuhudia. Mdo 1:8.
    • Kuwa na ujasiri. Mdo 2:14-41.
    • Kujisikia kumpenda Mungu na watu. Rm 5:5.
    • Kuwa na uwezo na hamu ya kuomba na kuwaombea wengine. Rm 8:26-27.
    • Madhihirisho ya karama za Roho Mtakatifu. 1Kor 12:1-11.
IV. HITIMISHO - MAMBO MUHIMU KATIKA KUBATIZWA NA ROHO MTAKATIFU.
  1. HAMU: Uwe na hamu ya kubatizwa na Roho Mtakatifu.
  2. IMANI: Amini kuwa unapokea Roho Mtakatifu sasa. Ebr 11:16; Mk 11:24.
  3. MSIFU BWANA: Bwana anaonesha uwepo wake wakati wa sifa. Mdo 4:31.
  4. JIWEKE CHINI YA MUNGU: Jitoe kwa Bwana kila kitu kiakili na kimwili. Rm 6:13, 12:1.



LESSON ON THE BAPTISM OF THE HOLY SPIRIT

By. Rev. Raphael Kitine (Senior Pastor ICC)

Leading Scriptures: Acts 1:4-5.

I. INTRODUCTION - THE MEANING OF THE BAPTISM BY THE HOLY SPIRIT
  1. Is an act of being immersed and filled with The Holy Spirit. Acts 1:4, 2:4.
  2. It is different from being born again. John 20:22; Acts 2:4, 8:12, 1:4.
  3. It is God's providence of Power. Luke 24:49; Acts 1:8; Luke 1:35.
  4. It is a Promise for all who beleieve. Acts 2:4, 39.
II. IMPORTANCE OF THE BAPTISM BY THE HOLY SPIRIT.
  1. It is scriptural commanded. Ephesians 5:18, Acts 1:4-5.
  2. It was a source of spiritual strength:
    • In the ministry of Jesus Christ. Acts 10:38; Luke 4:1.
    • In service of the early Church. Acts 1:8, 2:4, 4:31, 33.
III. HOW TO BE BAPTIZED BY THE HOLY SPIRIT.
A. TERMS FOR BEING BAPTISED BY THE HOLY SPIRIT.
  1. Must be born again. John 14:17; 3:5-7.
  2. Must desire to be filled with the Holy Spirit. Mt 5:6; Rm 15:16; 1Cor 6:11, 7:37.
  3. Must submit to God. Acts 5:32.
B. THREE STEPS OF BEING BAPTISED BY THE HOLY SPIRIT.
  1. Approach boldly at the throne of grace. Hebr 4:16.
  2. Pray to God to fill you with the Holy Spirit. Luke 11:10, 13.
  3. Praise God by faith. Mk 11:24; Luke 24:53
C. EVIDENCE OF BEING BAPTISED BY THE HOLY SPIRIT.
  1. Speaking in tongues. Acts 2:3, 10:45-47, 19:1-6.
  2. These signs shall acompany you as the Spirit dwells in you:
    •  Being able to do the works of Jesus. John 14:16-18, 16:14.
    • Feeling the presence of God. John 14:16-18.
    • To be conscious against sin. John 16:7-11.
    • To acquire capacity to be witness for Gospel. Acts 1:8.
    • Feel confident. Acts 2:14-41.
    • Acquire love for God and for people. Rm 5:5.
    • Acquire ability and desire to pray and intercede for others. Rm 8:26-27.
    • Manifestations of the gifts of the Holy Spirit. 1Kor 12:1-11.
IV. CONCLUSION - KEY ISSUES ON THE BAPTISM BY THE HOLY SPIRIT.
  1. APETITE: Have a desire to be babtized by the Holy Spirit.
  2. FAITH: Believe that you are going to receive the Holy Spirit now. Hebr 11:16; Mark 11:24.
  3. PRAISE: The Lord shows His presence during the moments of praising Him. Acts 4:31.
  4. YIELD BEFORE GOD: Submit yourself before the Lord in everything i.e mentally, physically and spiritually. Rm 6:13, 12:1.



MAFURIKO YA ROHO MTAKATIFU ICC

Shalom!
Jumapili ya jana (27/07/2014) imekuwa ni ya kihistoria kutokana na jinsi Ibada ilivyotawaliwa na uwepo wa Nguvu za Roho Mtakatifu mwanzo mwisho. Ibada zote mbili alihudumu Mchungaji Kiongozi wa ICC Mch. Raphael Kitine, Ibada hizi zilikuwa ni hitimisho au kilele cha Wiki ya Pentekoste ambapo Kanisa lilikuwa katika maombi ya kufunga kwa Wiki nzima.

Hata muonekano wa Mchungaji kiongozi ulikuwa wa kitofauti kwani alipigilia suti moja ya ukweli, tshirt na kofia ya Jubilee ya miaka 75 ya Kanisa la T.A.G. Akitoa ufafanuzi kuhusu mtoko huo Mchungaji Kitine alisema kuwa tukio la leo linaendana sambamba na malengo ya Jubilee ya miaka 75 ya Kanisa la T.A.G.


 Mch. Raphael Kitine akiwa sambamba na Mtafsiri wake Mr. Edom Fungo katika Ibada ya kwanza ambayo huendeshwa kwa lugha ya Kiingereza ICC.

Katika Ibada ya kwanza ambayo huendeshwa kwa lugha ya Kiingereza na kutafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili, Mch. Kitine alifundisha somo lenye Ujumbe "BABTISM BY THE HOLY SPIRIT". Ki ukweli uwepo wa Nguvu za Roho Mtakatifu ulishuka live bila chenga. Katika Ibada ya Pili Mch. Kitine aliendelea kuhudumu somo hilo alilitafsiri kwa Kiswahili somo hilo "UBATIZO WA ROHO MTAKATIFU". Yaani upako uliokuwepo ilikuwa ni balaa, haijalishi ulihudhuria Ibada ya kwanza au hukuhudhuria, ni full kushandaraiz mwanzo mwisho.

Mch. Raphael Kitine akihudumu katika Ibada ya pili, huku Wana ICC wakifuatilia kwa umakini mafundisho hayo.

Pastor Kitine akifundisha kwa vitendo kuonesha mshindo utakaotokea leo Ibadani, hata cjui kofia alivua saa ngapi.

Kama ilivyo ada, Timu ya kusifu na kuabudu ilikuwepo kutimiza wajibu wake.


Kanisa zima lilishiriki vyema katika Ibada hii ya kusifu na kuabudu.


Patmo Kwaya nao walikuwepo pia, yaani kilichotokea hakielezeki.
 Kwaya ya Patmo wakiwa Madhabahuni tayari kuhudumu.

Patmo waliimba wimbo unaoitwa Roho Mtakatifu, aisee Roho Mtakatifu alishuka kiukwelii wao wenyewe miguu ikaanza kunyong'onyea wakajikuta chini mmoja baada ya mwingine.

Ikabidi Mchungaji Kiongozi Mch. Raphael Kitine achukue kipaza na kuingilia kati kuendeleza wimbi la Roho Mtakatifu.


Kujua kilichotokea waweza kufungua link zifuatazo:
https://www.youtube.com/watch?v=K_AEIhI4Dk4
https://www.youtube.com/watch?v=p4OUZttlKZ8
http://iringacentralchurch.blogspot.com/2014/07/patmo-choir-icc-roho-mtakatifu-2.html

Upande wa muziki Vijana walijipanga ipasavyo.

Karibu sana ICC ubatizwe na Roho Mtakatifu.

Rev Kitine Maombi

Rev Kitine Maombezi

Patmo Choir ICC Roho Mtakatifu 2

Patmo Choir ICC Roho Mtakatifu 1

Patmo Choir ICC Yatendeni Mambo yote

Friday, 25 July 2014

RATIBA YA IBADA ZA KESHO JUMAMOSI - ICC (26/07/2014)

* Kwa siku ya kesho Jumamosi kutakuwa na mabadiliko kidogo ya muda wa Ibada kama ifuatavyo:
Saa 08:30 Mchana hadi 09:30 Alasiri - Mazoezi ya Kwaya;
Saa 09:30 Alasiri hadi 11:00 Jioni - Ibada ya Maombi;
Saa 11:00 Jioni na kuendelea ni Mazoezi na Maombi ya Timu ya Kusifu na kuabudu.

Ukiona taarifa hii mjulishe na mpendwa mwenzako.
Mungu akubariki.

MAOMBI YA LEO ICC (25/07/2014)

* Mambo ambayo tumeombea leo na tutaendelea nayo hadi kesho jioni ni:
I. UJAZO WA NGUVU ZA ROHO MTAKATIFU;
II. KUOMBEA KANISA LA T.A.G - I.C.C;
1. MAFANIKIO KATIKA MIPANGO YA KIROHO 2014.
> Kukua kwa Kanisa Kiroho na kiidadi;
> Mafanikio katika mipango ya Mikutano, Semina, Wiki za Maombi, Mikesha n.k;
> Mafanikio ya kuwa na Ibada zenye Nguvu ya Mungu.
2. MAFANIKIO KATIKA MIPANGO YA KIMAENDELEO 2014.
> Mafanikio katika Mpango wa Ujenzi wa Kanisa {Kibali cha Ujenzi na fedha za Ujenzi}
> Mafanikio ya kuwa na mradi wa Kanisa.
III. MAHITAJI MENGINEYO.

* Kumbuka kuwa saa kumi na moja alfajiri hadi saa kumi na mbili asubuhi tutaendelea na maombi ya mtandao kwa pamoja. Kila mtu atafanya maombi haya mahali alipo.
Mungu akubariki.

Thursday, 24 July 2014

Maombi ya Leo (24/07/2014)

* Mambo ambayo tumeombea leo na tutaendelea nayo hadi kesho jioni ni:
I. UJAZO WA NGUVU ZA ROHO MTAKATIFU;
II. KUOMBEA KANISA LA T.A.G;

ii. Mafanikio katika Mpango Mkakati  wa Miaka 10 ya Mavuno.
> Kila kilichokusudiwa kifanikwe;
> Mafanikio makubwa kimaendeleo ya kiroho na kimwili;
> Mafanikio katika ongezeko la Makanisa;
> Mafanikio katika ongezeko la Watumishi;
> Mafanikio katika miradi ya Kanisa.
III. MAHITAJI MENGINEYO.

* Kumbuka kuwa saa kumi na moja alfajiri hadi saa kumi na mbili asubuhi tutaendelea na maombi ya mtandao kwa pamoja. Kila mtu atafanya maombi haya mahali alipo.
Mungu akubariki.

Iringa Central Church Youtube

Shalom!
Sasa unaweza kupata matukio mbalimbali ya ICC kupitia youtube:
Just google: Iringa Central Church youtube
http://www.youtube.com/channel/UCKqoRia_Aqbv3HfbYSNJYJg
 http://www.youtube.com/watch?v=EZ1zbBgsrkk
 
Ubarikiwe.

Au bofya viunganishi vifuatavyo;
http://www.youtube.com/channel/UCKqoRia_Aqbv3HfbYSNJYJg

http://www.youtube.com/watch?v=EZ1zbBgsrkk

Wednesday, 23 July 2014

MAOMBI YA LEO ICC (23/07/2014)

* Mambo ambayo tumeombea leo na tutaendelea nayo hadi kesho jioni ni:
I. UJAZO WA NGUVU ZA ROHO MTAKATIFU;
II. KUOMBEA NCHI YETU TANZANIA;

ii. Mafanikio katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2014 na Uchaguzi Mkuu 2015.
> Uchaguzi uwe huru na wa haki;
> Tupate Viongozi waadilifu wenye uchungu na rasilimali za Nchi;
> Tupate Viongozi wenye hofu ya Mungu;
> Kukemea roho za mafarakano, ugomvi n.k.
III. MAHITAJI MENGINEYO.

* Kumbuka kuwa saa kumi na moja alfajiri hadi saa kumi na mbili asubuhi tutaendelea na maombi ya mtandao kwa pamoja. Kila mtu atafanya maombi haya mahali alipo.
Mungu akubariki.

Tuesday, 22 July 2014

MAOMBI YA LEO ICC (22/07/2014)

* Wiki hii ni ya maombi ya kufunga ICC ambayo tumeanza jana na tutamaliza Jumamosi. Mambo ambayo tumeombea leo na tutaendelea nayo hadi kesho jioni ni:
I. UJAZO WA NGUVU ZA ROHO MTAKATIFU;
II. KUOMBEA NCHI YETU TANZANIA;

i. Mafanikio katika mchakato wa katiba mpya.
> Bunge maalum la katiba;
> Katiba yenye kuruhusu uhuru wa kuabudu na kuhubiri injili;
> Katiba isiyoruhusu matendo ya kidhalimu, mfano Ushoga.
III. MAHITAJI MENGINEYO.

* Kumbuka kuwa saa kumi na moja alfajiri hadi saa kumi na mbili asubuhi tutaendelea na maombi ya mtandao kwa pamoja. Kila mtu atafanya maombi haya mahali alipo.
Mungu akubariki.

Monday, 21 July 2014

WIKI YA MAOMBI ICC (21 - 26/07/2014)

Shalom!

* Wiki hii ambayo imeanza leo kutakuwa na maombi ya kufunga (Kufunga na Kuomba) kwa Waamini wote wa ICC. Tutakuwa tunakutana Kanisani kila siku jioni kuanzia saa kumi na nusu hadi saa kumi na mbili na robo. Watu wote mnakaribishwa.

* Maombi ya Leo yalikuwa ni Ujazo wa Nguvu za Roho Mtakatifu na Utakaso. Maombi haya yataendelea hadi kesho jioni tutakapokutana tena Kanisani.

* Kumbuka kuwa saa kumi na moja alfajiri hadi saa kumi na mbili asubuhi tutaendelea na maombi ya mtandao kwa pamoja. Kila mtu atafanya maombi haya mahali alipo.
Mungu akubariki.

Sunday, 20 July 2014

Udhihirisho wa Nguvu za Roho Mtakatifu Ibadani ICC

Shalom!
Mungu ni mwema wakati wote. Roho wa Bwana ameendelea kuhudumia watu wake katika Ibada zote mbili za ICC siku ya leo.

Ibada ya kwanza inayoendeshwa kwa lugha ya Kiingereza alihudumu mpakwa mafuta wa Bwana Mch. Omega Kipemba, ambaye kwa sasa yupo likizo anasoma Chuo cha Theolojia kilichopo Nairobi Kenya. Alifundisha Ujumbe wenye kichwa cha habari "PNEUMATOLOGY".  He defined Pneumatology as the study of the person and the work of the Holy Spirit. The leading scriptures were from the book of John 14:15-18. He also defined Pneumatology as the theological discipline that focuses only on the Holy Spirit. This discipline is covered all over the Bible from the book of Genesis to the book of Revelation. Other sciptures Mathew 19:28; Titus 3:5; John 3:3; Eph 2:6, more deatails about this subject will be available here later. Stay tuned, Usitoke usiondoke.
Mch. Omega Kipemba akiwa na Mtafsiri wake Mr. Edson Ishengoma wakichimbua madini ya ukweli toka kwenye mgodi wa Roho Mtakatifu.

Ibada ya pili inayoendeshwa kwa lugha ya Taifa alihudumu Mtumishi wa Bwana Mch. Ruth Kyando ambaye naye yupo likizo, anasoma Chuo Cha Biblia Dodoma.  Yeye alifundisha Ujumbe wenye kichwa cha habari "ROHO MTAKATIFU",  Maandiko: Mwanzo 1:2; Mk 1:10-11; Mt 28:19; Yohana 14:16, 26-27; 16:8-13. Somo kamili utalipata hapahapa. Ndio maana nikasema ni Ibada ya Udhihirisho wa Roho Mtakatifu, kwani Ibada zote mbili Watumishi wa Bwana wamefundisha Jumbe zenye maudhui yanayofana ingawa kila mmoja lifundisha kadri Roho wa Bwana alivyomuwezesha.
Mch. Ruth Kyando akiwa madhabahuni ICC, kidigitali zaidi lakini Roho Mtakatifu anajidhihirisha.

Kama ilivyo kawaida, Ibada ya Sifa hutangulia kabla ya mahubiri. Katika Ibada zote mbili Timu ya Kusifu na Kuabudu ilifanya vyema katika kuliongoza Kanisa kwenye Sifa na Kuabudu.
Timu ya Kusifu na Kuabudu ya ICC ikiwajibika ipasavyo Madhabahuni.

Kwaya ya Kanisa PATMO nao walihudumu katika Madhabahu ya ICC.
Patmo Christian Singers (PCS) ya ICC wakifanya yao Madhabahuni.

Kanisa zima kwa ujumla lilishiriki vyema katika kumsifu na kumuabudu Mungu katika Roho na kweli.

Baada ya Ibada ya Kusifu na Kuabudu, ilifanyika Ibada ya Maombezi iliyoongozwa na Mchungaji Kiongozi wa ICC Mch. Raphael Kitine kwa kushirikiana na Wachungaji waliohudumu Ibada zote za leo na Wazee wa Kanisa.

Upande wa muziki, Mwl. Alpha aliwaongoza vyema vijana wake Amani na James.

Matukio yalichukuliwa na Mr. Gerlad, dawati la IT kama kawaida Mr. Mkea na Sir ECHA waliwajibika ipasavyo

Kumbuka kuanzia Jumatatu (21/07/2014) hadi Jumamosi (26/07/2014) ni Wiki ya Maombi ya Kufunga kwa Kanisa zima. Tutakuwa tunakutana Kanisani kila siku kuanzia saa kumi na nusu jioni.

Karibu sana ICC, Mungu akubariki.