Wednesday, 30 July 2014

WIKI YA UINJILISTI ICC YAZINDULIWA KIANA YAKE LEO.

Siku ya leo, Kanisa la ICC limezindua rasmi Wiki ya Uinjilisti kwa Waamini wote kukutana Kanisani, kupeana maelekezo na kusambaa mitaani kwenda kuhubiri Injili.
Wiki ya Uinjilisti inatimiza agizo kuu alilotuachia Bwana Yesu kabla hajapaa kurudi mbinguni kuketi mkono wa kuume wa Mungu. Marko 16:15-20.
Baada ya uzinduzi huu wa leo, kuanzia kesho (31/07/2014) hadi Jumamosi (02/08/2014) kutakuwa na Mkutano Mkubwa wa Injili katika Viwanja vya Sabasaba Iringa kuanzia saa kumi kamili Jioni. Atakayehubiri katika Mkutano huu Mkubwa wa Injili ni mpakwa mafuta wa Bwana, Mchungaji na Mwinjilisti Omega Kipemba.
Wagonjwa na wenye shida mbalimbali wataombewa. Karibuni wote, wewe upataye Ujumbe huu tafadhali mjulishe na mwenzako

Picha za Baadhi ya Waamini wa ICC waliofika leo Kanisani kwa ajili ya uzinduzi wa Wiki ya Uinjilisti.



No comments:

Post a Comment