Thursday, 31 July 2014

MKUTANO WA INJILI ICC SABASABA WAANZA RASMI LEO

Leo hii Waamini wa ICC Sabasaba tumekutana katika Viwanja vya ICC Sabasaba kwa ajili ya kuanza rasmi Mkutano wa Injili, ambao unaendeshwa na Idara ya Uinjilisti ya Kanisa.

Kabla ya Muhubiri kusimama, Mch. Ruth Kyando alisimama kutoa maneno ya utangulizi.


Muhubiri wa Mkutano huu ni Mchungaji na Mwinjilisti Omega Kipemba.

UJUMBE: UKIWA KATIKATI.
MAANDIKO
: Yohana 6:15-22; Kutoka 6:9.

Akihubiri kwa upako wa hali ya juu, alisema kwamba ukiwa katikati ya shida, adha, taabu, mateso na dhiki, mtu hukata tamaa na kuona hakuna tumaini wala msaada. Lakini unapaswa kufahamu kuwa Yesu yupo kukusaidia na kukukwamua kutoka katika hali uliyonayo.


Mchungaji na Mwinjilisti Omega Kipemba akiwa Jukwaani akihubiri.

Somo hili ataendelea nalo kipindi chote cha Mkutano, tafadhali usikose. Karibu Bwana aseme nawe ukiwa katikati ya hali yoyote unayopitia.

Kwaya ya Kanisa ya Patmo pia walihudumu katika siku ya leo.

Baadhi ya watu waliofika kwenye Mkutano wakiwa katika kipindi cha kusifu.

Usikose kesho. Mungu akubariki.

No comments:

Post a Comment