Jumapili ya jana (27/07/2014) imekuwa ni ya kihistoria kutokana na jinsi Ibada ilivyotawaliwa na uwepo wa Nguvu za Roho Mtakatifu mwanzo mwisho. Ibada zote mbili alihudumu Mchungaji Kiongozi wa ICC Mch. Raphael Kitine, Ibada hizi zilikuwa ni hitimisho au kilele cha Wiki ya Pentekoste ambapo Kanisa lilikuwa katika maombi ya kufunga kwa Wiki nzima.
Hata muonekano wa Mchungaji kiongozi ulikuwa wa kitofauti kwani alipigilia suti moja ya ukweli, tshirt na kofia ya Jubilee ya miaka 75 ya Kanisa la T.A.G. Akitoa ufafanuzi kuhusu mtoko huo Mchungaji Kitine alisema kuwa tukio la leo linaendana sambamba na malengo ya Jubilee ya miaka 75 ya Kanisa la T.A.G.
Mch. Raphael Kitine akiwa sambamba na Mtafsiri wake Mr. Edom Fungo katika Ibada ya kwanza ambayo huendeshwa kwa lugha ya Kiingereza ICC.
Katika Ibada ya kwanza ambayo huendeshwa kwa lugha ya Kiingereza na kutafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili, Mch. Kitine alifundisha somo lenye Ujumbe "BABTISM BY THE HOLY SPIRIT". Ki ukweli uwepo wa Nguvu za Roho Mtakatifu ulishuka live bila chenga. Katika Ibada ya Pili Mch. Kitine aliendelea kuhudumu somo hilo alilitafsiri kwa Kiswahili somo hilo "UBATIZO WA ROHO MTAKATIFU". Yaani upako uliokuwepo ilikuwa ni balaa, haijalishi ulihudhuria Ibada ya kwanza au hukuhudhuria, ni full kushandaraiz mwanzo mwisho.
Pastor Kitine akifundisha kwa vitendo kuonesha mshindo utakaotokea leo Ibadani, hata cjui kofia alivua saa ngapi.
Kama ilivyo ada, Timu ya kusifu na kuabudu ilikuwepo kutimiza wajibu wake.
Kanisa zima lilishiriki vyema katika Ibada hii ya kusifu na kuabudu.
Patmo Kwaya nao walikuwepo pia, yaani kilichotokea hakielezeki.
Kwaya ya Patmo wakiwa Madhabahuni tayari kuhudumu.
Patmo waliimba wimbo unaoitwa Roho Mtakatifu, aisee Roho Mtakatifu alishuka kiukwelii wao wenyewe miguu ikaanza kunyong'onyea wakajikuta chini mmoja baada ya mwingine.
Ikabidi Mchungaji Kiongozi Mch. Raphael Kitine achukue kipaza na kuingilia kati kuendeleza wimbi la Roho Mtakatifu.
Kujua kilichotokea waweza kufungua link zifuatazo:
https://www.youtube.com/watch?v=K_AEIhI4Dk4
https://www.youtube.com/watch?v=p4OUZttlKZ8
http://iringacentralchurch.blogspot.com/2014/07/patmo-choir-icc-roho-mtakatifu-2.html
Upande wa muziki Vijana walijipanga ipasavyo.
Karibu sana ICC ubatizwe na Roho Mtakatifu.
No comments:
Post a Comment