Wednesday, 21 May 2014

KUTOKA MADHABAHUNI ICC: HATUA MUHIMU ZA KUPOKEA MUUJIZA WAKO

Mhubiri: Mch. Raphael Kitine (Mchungaji Kiongozi I.C.C)

MSTARI MKUU: Yohana 5:8

I. UTANGULIZI:

 A. Maana Halisi ya Muujiza.
* Ni Hali ya Mungu kuingilia kati kwa Nguvu Kuu :
> Ni tukio linalotokea kinyume cha kanuni/sheria za asili, na linaangaliwa kama tendo la Mungu.
* Matukio yanayostaajabisha (Yanayoshangaza):
> Ni tukio linalostaajabisha zaidi ya jambo lililo tarajiwa.
*  Mungu anataka kutubariki katika kila eneo la maisha yetu; Kiroho, Kimwili, Kiuchumi n.k
* Lakini tatizo lipo kwa Wakristo wengi kutojua ni namna gani wapokee miujiza yao toka kwa Mungu.
* Ili tuweze kupokea miujiza yetu, na tuishi katikati ya baraka na uwepo wa Mungu, ni LAZIMA tuelewe, na tuweze kufanyia kazi HATUA MUHIMU ZA KUPOKEA MIUJIZA YETU.

 B. FAIDA/UMUHIMU WA MIUJIZA KATIKA MAISHA YETU :
> Imani zetu zitakua na kuzidishwa maradufu na zaidi.
> Tutajisikia vizuri kuwepo ndani ya Nyumba ya Mungu. Matendo 3:6-9,
> Miujiza huwavuta watu wengi kwa Yesu. Yohana 2:23

II. HATUA ZA KUPOKEA MUUJIZA WAKO:

A. Mtambue na umkubali Mungu kuwa ndio chanzo cha kila kitu chako. Wafilipi 4:6
> Tafuta uelekeo na maelekezo ya Mungu kabla hujaomba Muujiza wako.
> Haja zako na mahitaji yako yajulikane kwa Mungu, kwa njia ya maombi.
> Pata taswira ya wazi ya kila unachotaka kutoka kwa Mungu; unapaswa kuwa na maono sahihi ya kile unachokitaka toka kwa Mungu.

B. Geuza hali ya kifo inayokuzunguka. 2 Korintho 1:9
> Amini kuwa Mungu anaweza kufanya mambo yote. Yeremia 32:27
> Shetani akikukumbusha mambo mabaya, mkumbushe mambo mazuri ambayo Mungu amekutendea katika maisha yako.
> Amini kuwa Mungu akiahidi Muujiza, hakuna mtu, kitu wala jambo linaloweza kukuzuia kupokea isipokuwa ni wewe mwenyewe binafsi.

C. Anza kufanyia kazi/ Mazoezi vitu ambavyo hukuweza kufanya kabla. Yohana 5:8
> Usiruhusu hali ya kutilia shaka au hofu kuhusu hitaji lako kama litafanikiwa au halitafanikiwa.
> Unachotakiwa kufanya, ni kujiamini kuwa umeshafanya sehemu yako sasa unasubiri Mungu akufanyie Muujiza wako.

D. Shuhudia Jambo ambalo Mungu amekufanyia. Marko 5:19
> Mungu hutubariki ili tuwe mfano kwa wengine, anataka watu wengine waione nuru kupitia sisi. Luka 8:16
> Ufalme wa shetani haupendi kuona watu wakishuhudia matendo mema ya Mungu aliyowatendea.
> Kwa kadri unavyoshuhudia matendo Makuu ambayo Mungu amekutendea, ndivyo Mungu atakavyozidi kukubariki zaidi.

III. HITIMISHO:
> Ni wakati wako sasa kutendea kazi somo hili, ili uweze kupokea Muujiza wako. Chukua hatua sasa.

MUNGU AKUBARIKI.





2 comments:

  1. God bless you for a wonderful teachings!
    Barikiwa!

    ReplyDelete
  2. Ninashukuru sana kwa somo hili, ki ukweli wengi tumekuwa tukikimbilia miujiza bila kujua hatua muhimu tunazotakiwa kuzifuata. Matokeo yake tunaangukia kwenye imani potofu.

    ReplyDelete